Watanzani hawali magamba, wanataka huduma zitokanazo na fedha zilizoibiwa na mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzani hawali magamba, wanataka huduma zitokanazo na fedha zilizoibiwa na mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WATANABE, Apr 19, 2011.

 1. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Kutokea kuingia madarakani kwa Raisi Kikwete mwaka 2005, vyama vya upinzani vilianza kupiga kelele juu ya kuwepo kwa wizi mkubwa wa fedha za umma hususan EPA, RICHMOND, RADA, MEREMETA n.k hali ambayo kwa kikubwa imedhoofisha kasi na uwezo wa serikali kuwapatia watanzania huduma mbali mbali za kijamii na kiuchumi.

  Mara zote chama tawala CCM ama kimekuwa kikikanusha kuwepo kwa wizi huo na kuwakingia kifua watuhumiwa mbali mbali wa UFISADI huo, ambao wengi wao ni viongoiozi waandamizi wa chama hicho. Mifano hai ya kuwakingia kifua watuhumiwa hao ni pale mgombea urais wa CCM alipozunguka nchi nzima akiwanadi watuhumiwa mbali mbali wa ufisadi, rushwa wakati uchaguzi n.k. kwa kuwaambia wananchi hawa ni wagombea safi kabisa.

  Hivi karibuni CCM imekubali kuwa lipo tatizo la wizi mkubwa wa mali ana raslimai za taifa huitwao UFISADI na imekiri kuwa wahusika wakuu wa Ufisadi huo unaowatesa watanzania ni viongozi wake waandamizi. Na CCM imewataka wajiondoe katika nyadhifa zao ndani ya chama hicho ndani ya siku 90 la sivyo wataondolewa kwa nguvu.

  Aidha wajumbe wapya Sekreterieti ya CCM akiwemo Katibu Mkuu Ndg Wilson Mukama, Katibu wa Uenezi Ndg Nape Nnauye na katibu wa Mambo ya Nje Ndg January Makamba wamekuwa wakifanya mikutano ya hadhara sehemu mbali mbali wakiitambulisha Sekreterieti mpya ya CCM huku wakisisitiza wanaCCM wenye tuhuma mbali mbali za ufisadi wajitoe katika uongozi wa CCM; kana kwamba Mafisadi wakijitoa CCM ndio wananchi wanapata zahanati, watoto wanaosomea chini ya miti wanapata madarasa, waalimu ambao hawana nyumba za kuishi katika vituo vyao vya kazi wanapata makazi, akina mama wanaojifungulia chini na kulala watatu kitanda kimoja kwa ukosefiu wa wodi za wagonjwa na vitanda watapata wodi na vitanda baada ya Mafisadi hao kujitoa CCM n.k

  Kwa hakika kelele tupu za Sekreterieti mpya ya CCM zisizoambatana na vitendo vinatia kinyaa ikizingatiwa kuwa kiasi cha fedha kinachotuhumiwa kuibiwa na watuhumiwa hao wa CCM ni kikubwa; ilihali kiasi cha fedha kinachohitajika kuondao kabisa matatizo sugu yanayowakabili watanzania ni kidogo sana.

  Ni imani yangu kuwa Mukama, Nape na January wanapata ujasiri wa kuwapigia kelee watanza nia wenye njaa kutokana na ukweli kwamba binadamu ameumbwa na udhaifu wa kusahau. Hivyo kama sehemu ya elimu ya uraia ni vyema wapenda mabadiliko wote tukachukua fursa hii kuwakumbusha watanzania wakiwemo Mukama, Nape na January kiasi cha fedha kinachohusika kuibiwa na watuhumiwa hao ambao ni viongozi waandamizi wa CCM na kulinganisha kiasi hicho cha fedha zilizoibiwa na kiwango cha maendelo ambayo yangeweza kupatika endapo fedha hizo zisingeibiwa na badala yake kutumika kuondoa matatizo sugu ya watanzania ambayo si Mukama, Nape na January wanayajua kutokana na wao sasa kuwa watu wa kuanda mashangingi ya zaidi ya Milioni 100 kila mmoja.


  Kwa mujibu wa takwimu mbali mbali hivi sasa darasa moja hapa nchini linagharimu Dola 5,000/= sawa na shilingi Milioni 7.6 katika Exc Rate ya 1,520/=. Hivyo basi Shilingi Bilioni 40 zilizoibiwa na ilizoibiwa na kampuni ya KAGODA kwa ridhaa na ushiriki wa ROSTAM, MKAPA, KIKWETE, MANGULA, MALECELA, LOWASSA N.K zingetosha kujenga vyumb 5,263 vya madarasa na kumaliza kabisa tatizo la uhaba wa madarasa hapa nchini, tatizo ambalo huwalazimu idadi kubwa ya watoto wa Kitanzania kusomea chini ya miti, zaidi 100 katika darasa moja na kukaa chini.

  Ikiwa zahanati moja inagharimu Shilingi Milioni 10, fedha hizo zingetosha kujenga zahanati 4,000 nchi nzima na kumaliza kabisa tatizo la ukosefu wa majengo ya zahanati hapa nchini.

  Nataka Mukama, Nape na January watambue kuwa kitendo cha wao kuteremka kutoka katika mashangingi ya zaidi ya Shilingi Milioni 100 na kuja kuwadhiaki watu ambao ndugu zao wakepoteza maisha kwa kukosa huduma za afya, kunywa maji machafu, watoto wao wanakuwa masikini kwa kukosa elimu n.k kinazidisha hasira za watanzania dhidi ya CCM badala ya kuisafisha.

  Hivi mtu aliyefiwa na mkewe kwa kukosa fedha za kumnunua vifaa vya kujifungulia visivyozidi Elfu 20 ataweza kuelewa lugha wa MAFISADI kujitoa CCM wakale kwa amani fedha walizoliibia taifa.

  Hivi kijana wa kitanzania ambaye anaona dhahiri kuwa ndani ya CCM kuna recycling ya watoto wa vigogo kushika nyadhifa zilzokuwa zikishikiliwa na wazazi wao kutokana na wazazi hao kushiriki ufisadi na kumudu gharama za kuwapatia elimu nje ya nchi huku watoto wa wakulima na wafanyakazi wakikosa madarasa, vitabu, waalimu, mikopo ya elimu ya juu, mlundikano katika elimu ya juu n.k wataweza kuelewa lugha wa MAFISADI kujitoa CCM wakale kwa amani fedha walizoliibia taifa.

  Hivi watoto na wajukuu wa watanzania waliojitoa mhanga kwa hali na mali na kufa wakijenga taifa katika vit ya Uganda, Msumbiji, Zimbabwe, Afrika Kusini n.k wataweza kuelewa vitendo vya baadhi ya wateule wachache kujitwalia Prime Properties zilizokuwa zikimilikiwa na Serikali na kuzitumia kupangisha kwa dola baada ya kitu kiitwacho kuuzwa kwa nyumba za Serikali huku wao wakikosa huduma za wazazi wao waliokufa kwa ajili ya tiafa hili na hivyo kubaki katika lindi la umaskini? Kwani watoto hawa wa viongozi wa Tanzania wana nini cha mno cha kuwazidi watoto wa wakulima, wafanyakazi na maskini wengine?

  Watanzania tunataka kuona sheria zikichukua mkondo wake na MAFISADI wakifikishwa mahakamani na ikiwezekana wakipigwa risasi kama CHINA sio blaha blah za kujitoa ndani ya CCM ukale fedha ulizoiba kwa amani na utulivu.
   
Loading...