Watano mbaroni Dar wakihusishwa na mauaji ya RPC Barlow

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
KIKOSI maalumu cha vyombo vya usalama chini ya Jeshi la Polisi, kimewatia mbaroni jijini Dar es Salaam watuhumiwa watano muhimu wa mauaji ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow.

Habari za uhakika kutoka vyanzo vyetu vya ndani zimethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao muhimu ambao wanatarajiwa kuhojiwa na kusafirishwa kwenda Mwanza kushitakiwa.




Gari aina ya HILUX (T 777 BFY) linalodaiwa hayati RPC Liberatus Lyimo Barlow wa Mwanza, alikuwa akiendesha siku mauti yake yalipomkuta kwa kuuawa papo hapo kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni MAJAMBAZI Kitangiri Jijini Mwanza Tar 13/Oktoba/2012.

Hii ni developing story kutoka - Watano mbaroni Dar wakihusishwa na mauaji ya RPC Barlow | Fikra Pevu

 
Wamemuongeza mchezaji wa zamani wa simba? Maana yupo wa yanga Fumo Felisian ili ngoma iwe draw.
 
mmh! hapa liyekuwa hawara wa dorothy lazima awe mtuhumiwa namba moja.
ila ukweli uzinzi ni kitu kibaya hasa kama tayar ushakuwa na commitment na mtu.
 
Quran inasema 'usiikaribie zinaa'

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
na kila zinaa mtu aifanyayo lazima aje kuilipia tu.manake quran inasema siku mzinzi akifa atafufliwa akiwa na nyuchi zote alizo tumikia akiwa hai na hizi zitaota usoni mwake sasa sijui itakuwaje iyo siku lol!

siitamani hata kidogo manake...................mmmh!
 
Hili polisi wanaliweza kwa kuwa ni la mwenzao na wanajua madhambi yao na wabaya wao.Lakini uchunguzi kwa vifo vya raia wengine siku zote unaendelea na kufutia mara tukio lingine linapotokea.

Tanzania kisiwa cha amani kwa wenye mamlaka, lakini sasa kinageuka kuwa kisiwa cha mauaji ya kila mtu bila kujali cheo au utajiri alionao mtu.
 
wanavyosema watuhumiwa muhimu wanamaana gani? je walitaraja kuwa hao ndio wawe watuhumiwa? walikuwa wanatafutwa kwa matukio mengine pia? naona kama wanataka kuanda move nyingine!
 
Kwanini damu ipo sehemu za chini tu za gari?

Nahisi alipigwa risasi wakati mlango ukiwa umefunguliwa.

Kuna hata uwezekano walitumia silaha yake mwenyewe

Kama statement ya Dorothy itatofautiana sana na hayo basi kuna kitu hapo
 
Kwanini damu ipo sehemu za chini tu za gari?

Nahisi alipigwa risasi wakati mlango ukiwa umefunguliwa.

Kuna hata uwezekano walitumia silaha yake mwenyewe

Kama statement ya Dorothy itatofautiana sana na hayo basi kuna kitu hapo

Always Damu inatoka kwa pressure ila haikuweza Kuruka kwani nadhani Nguo alizovaa zilizuia na hivyo kuchuruzika kuelekea chini!!
 
mmh! hapa liyekuwa hawara wa dorothy lazima awe mtuhumiwa namba moja.
ila ukweli uzinzi ni kitu kibaya hasa kama tayar ushakuwa na commitment na mtu.

Zinaa inaitwa kosa kuu.Maana dhambi nyingine zote mtu huzifanya nje ya mwili wake au
kwakushirikisha kiungo flani tu,lakini zinaa unaushirikisha mwili wako wote.
 
Always Damu inatoka kwa pressure ila haikuweza Kuruka kwani nadhani Nguo alizovaa zilizuia na hivyo kuchuruzika kuelekea chini!!

Inatoka kwa pressure ni kweli na kama nguo zilizuia tusingeona hivyo vimatone vidogovidogo kwenye mlango upande wa kulia kwa chini hapo chini ya hicho cha kupandishia kioo cha dirisha
 
Quran inasema 'usiikaribie zinaa'

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Biblia inaagiza tuikimbie zinaa!!!

“Do you not know that the unrighteous will not inherit the kingdom of God? Do not be deceived; neither the immoral, nor idolaters, nor adulterers, nor sexual perverts, nor thieves, nor the greedy, nor drunkards, nor revilers, nor robbers will inherit the kingdom of God.” (1 Corinthians 6:9-10)
 

Mbona umeguna mpendwa?
 

Best hapo "nyuchi....." umepiga vibaya! Ngoja uamsho waje! Shauri yako......
 
Jamani tupatieni majina manake nilisikia kwa mbali majina kama mwita, Bhoke, Marwa, etc. Mwenye majina yaliyotajwa atupeperushie hapa tafadhali.
 
Mbona umeguna mpendwa?

hivi ukipanga nyumba ya mganga utauliza kwann nanuka uvumba? nitafufuka nazo 200 za kizungu, kiarabu, kiswahili na kihindi. pia nene, nyembembe, fupi kwa ndefu kubwa kwa ndogo. wewe mwenzangu je?
 
Wamemuongeza mchezaji wa zamani wa simba? Maana yupo wa yanga Fumo Felisian ili ngoma iwe draw.

Unashauri aongezwe nani kati ya hawa? Geoge Masatu, Hussein Masha na Maftaha? Kwani kuna mechi ya veterani mzee mpaka wa balance? Fumo amehusika vipi embu lete habari zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…