Watano mbaroni Dar wakihusishwa na mauaji ya RPC Barlow

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
KIKOSI maalumu cha vyombo vya usalama chini ya Jeshi la Polisi, kimewatia mbaroni jijini Dar es Salaam watuhumiwa watano muhimu wa mauaji ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow.

Habari za uhakika kutoka vyanzo vyetu vya ndani zimethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao muhimu ambao wanatarajiwa kuhojiwa na kusafirishwa kwenda Mwanza kushitakiwa.



damu-barlow.jpg

Gari aina ya HILUX (T 777 BFY) linalodaiwa hayati RPC Liberatus Lyimo Barlow wa Mwanza, alikuwa akiendesha siku mauti yake yalipomkuta kwa kuuawa papo hapo kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni MAJAMBAZI Kitangiri Jijini Mwanza Tar 13/Oktoba/2012.

Hii ni developing story kutoka - Watano mbaroni Dar wakihusishwa na mauaji ya RPC Barlow | Fikra Pevu

IJUMAA, OCTOBA 26, 2012 | NA JOHN MADUHU, MWANZA


*Yumo mwanamke mmoja, wanaume wanne


JESHI la Polisi nchini, limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano wanaodaiwa kuhusika na kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mwanza, marehemu Liberatus Barlow. Pia jeshi hilo limefanikiwa kukamata bunduki iliyotumika kumuua kamanda huyo.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, aliwambia waandishi wa habari jijini Mwanza jana kuwa, watuhumiwa hao walikamatwa jijini Dar es Salaam ambako walikimbilia baada ya mauaji.

Katika mkutano huo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Said Mwema, naye alikuwapo.

Aliwataja waliohusika na mauaji hayo ambao bado wako jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda Mwanza, kuwa ni Muganyizi Peter (36) ambaye alitajwa na wenzake kuwa ndiye aliyefyatua risasi iliyomuua Kamanda Barlow.

Watuhumiwa wengine ni Chacha Mwita (50), Majige Marwa (48), Edward Kasutwa ambaye umri wake bado haujafahamika na mwanamke mmoja, Bhoke Mwita (42).

Pamoja na idadi hiyo, alisema Jeshi la Polisi bado linawasaka watuhumiwa wengine wawili waliokuwa katika tukio hilo.

Kwa mujibu wa DCI Manumba, kabla ya tukio hilo la mauaji, watuhumiwa hao ambao ni majambazi walikuwa wamefanya matukio matatu ya ujambazi katika maeneo tofauti jijini Mwanza kwa kupora vitu mballimbali kabla ya kukutana na Kamanda Barlow.

Alisema kwamba, watuhumiwa hao walifanya ujambazi kwa kuvamia Baa ya New Tuliza iliyopo eneo la Rumala majira ya saa nne usiku kwa kupora pombe na simu za wateja na kuondoka.

"Baadaye walivamia super market na kupora vitu mbalimbali na baadaye kumvamia mama mmoja na kumpora simu.

"Baada ya tukio hilo, ndipo walikutana na Kamanda Barlow na kumuua kwa kumpiga risasi shingoni kwa kutumia bunduki aina ya short gun na kufariki papo hapo.

"Walipokutana na Kamanda Barlow, watu hao walikuwa wakielekea Kitangiri kupumzika na walipomulikwa na taa za gari la kamanda, walimvamia wakati kamanda akigeuza gari na kuanza majibishano.

"Tukio hilo lilimfanya Kamanda achukue redio yake kwa ajili ya kutoa taarifa kwa wasaidizi na hapo ndipo walipomuua na haya ni kutokana na maelezo yao baada ya kuwahoji," alisema.

Akizungumzia namna polisi walivyofanikiwa kuwatia nguvuni watuhumiwa hao, alisema Jeshi la Polisi liliamua kujipanga kikamilifu kwa kuunda vikosi mbalimbali vya ukamataji na kuhoji pamoja na kikosi cha kufuatilia matukio yote muhimu ya simu ndani na nje ya nchi.

Alisema kuwa, polisi walifanikiwa kupitia kikosi cha mawasiliano, kukamata simu iliyokuwa ikitumiwa na mwanamke aliyekuwa na Kamanda Barlow ambayo iliporwa na majambazi hayo wakati wa tukio na baadaye kuanza kutumiwa na mwanamke mmoja jijini Dar es Salaam.

"Baada ya polisi kumfuatilia mwanamke huyo, alitoa ushirikiano ambao ulifanikisha kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa jijini Dar es Salaam na walikutwa na silaha hiyo.

"Inasemekana pia watu hao walikuwa wamehusika na tukio la uporaji wa fedha katika kiwanda kimoja jijini Dar es Salaam.

"Baada ya kuwakamata watuhumiwa hao, walikiri kuhusika na tukio hilo la mauaji ya Kamanda Barlow pamoja na kukiri kuhusika na matukio mbalimbali ya mauaji na uhalifu katika maeneo mbalimbali hapa nchini," alisema DCI Manumba.

Naye IGP alisema Jeshi la Polisi bado liko imara na limeimarika zaidi baada ya tukio hilo na kuonya kuwa halitawaonea huruma wahalifu.
 
Wamemuongeza mchezaji wa zamani wa simba? Maana yupo wa yanga Fumo Felisian ili ngoma iwe draw.
 
mmh! hapa liyekuwa hawara wa dorothy lazima awe mtuhumiwa namba moja.
ila ukweli uzinzi ni kitu kibaya hasa kama tayar ushakuwa na commitment na mtu.
 
Quran inasema 'usiikaribie zinaa'

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
na kila zinaa mtu aifanyayo lazima aje kuilipia tu.manake quran inasema siku mzinzi akifa atafufliwa akiwa na nyuchi zote alizo tumikia akiwa hai na hizi zitaota usoni mwake sasa sijui itakuwaje iyo siku lol!

siitamani hata kidogo manake...................mmmh!
 
Hili polisi wanaliweza kwa kuwa ni la mwenzao na wanajua madhambi yao na wabaya wao.Lakini uchunguzi kwa vifo vya raia wengine siku zote unaendelea na kufutia mara tukio lingine linapotokea.

Tanzania kisiwa cha amani kwa wenye mamlaka, lakini sasa kinageuka kuwa kisiwa cha mauaji ya kila mtu bila kujali cheo au utajiri alionao mtu.
 
wanavyosema watuhumiwa muhimu wanamaana gani? je walitaraja kuwa hao ndio wawe watuhumiwa? walikuwa wanatafutwa kwa matukio mengine pia? naona kama wanataka kuanda move nyingine!
 
Kwanini damu ipo sehemu za chini tu za gari?

Nahisi alipigwa risasi wakati mlango ukiwa umefunguliwa.

Kuna hata uwezekano walitumia silaha yake mwenyewe

Kama statement ya Dorothy itatofautiana sana na hayo basi kuna kitu hapo
 
Kwanini damu ipo sehemu za chini tu za gari?

Nahisi alipigwa risasi wakati mlango ukiwa umefunguliwa.

Kuna hata uwezekano walitumia silaha yake mwenyewe

Kama statement ya Dorothy itatofautiana sana na hayo basi kuna kitu hapo

Always Damu inatoka kwa pressure ila haikuweza Kuruka kwani nadhani Nguo alizovaa zilizuia na hivyo kuchuruzika kuelekea chini!!
 
mmh! hapa liyekuwa hawara wa dorothy lazima awe mtuhumiwa namba moja.
ila ukweli uzinzi ni kitu kibaya hasa kama tayar ushakuwa na commitment na mtu.

Zinaa inaitwa kosa kuu.Maana dhambi nyingine zote mtu huzifanya nje ya mwili wake au
kwakushirikisha kiungo flani tu,lakini zinaa unaushirikisha mwili wako wote.
 
Always Damu inatoka kwa pressure ila haikuweza Kuruka kwani nadhani Nguo alizovaa zilizuia na hivyo kuchuruzika kuelekea chini!!

Inatoka kwa pressure ni kweli na kama nguo zilizuia tusingeona hivyo vimatone vidogovidogo kwenye mlango upande wa kulia kwa chini hapo chini ya hicho cha kupandishia kioo cha dirisha
 
Quran inasema 'usiikaribie zinaa'

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Biblia inaagiza tuikimbie zinaa!!!

“Do you not know that the unrighteous will not inherit the kingdom of God? Do not be deceived; neither the immoral, nor idolaters, nor adulterers, nor sexual perverts, nor thieves, nor the greedy, nor drunkards, nor revilers, nor robbers will inherit the kingdom of God.” (1 Corinthians 6:9-10)
 
na kila zinaa mtu aifanyayo lazima aje kuilipia tu.manake quran inasema siku mzinzi akifa atafufliwa akiwa na nyuchi zote alizo tumikia akiwa hai na hizi zitaota usoni mwake sasa sijui itakuwaje iyo siku lol!

siitamani hata kidogo manake...................mmmh!

Mbona umeguna mpendwa?
 
na kila zinaa mtu aifanyayo lazima aje kuilipia tu.manake quran inasema siku mzinzi akifa atafufliwa akiwa na nyuchi zote alizo tumikia akiwa hai na hizi zitaota usoni mwake sasa sijui itakuwaje iyo siku lol!

siitamani hata kidogo manake...................mmmh!

Best hapo "nyuchi....." umepiga vibaya! Ngoja uamsho waje! Shauri yako......
 
Jamani tupatieni majina manake nilisikia kwa mbali majina kama mwita, Bhoke, Marwa, etc. Mwenye majina yaliyotajwa atupeperushie hapa tafadhali.
 
Mbona umeguna mpendwa?

hivi ukipanga nyumba ya mganga utauliza kwann nanuka uvumba? nitafufuka nazo 200 za kizungu, kiarabu, kiswahili na kihindi. pia nene, nyembembe, fupi kwa ndefu kubwa kwa ndogo. wewe mwenzangu je?
 
Wamemuongeza mchezaji wa zamani wa simba? Maana yupo wa yanga Fumo Felisian ili ngoma iwe draw.

Unashauri aongezwe nani kati ya hawa? Geoge Masatu, Hussein Masha na Maftaha? Kwani kuna mechi ya veterani mzee mpaka wa balance? Fumo amehusika vipi embu lete habari zaidi.
 
Back
Top Bottom