Watano mbaroni Dar wakihusishwa na mauaji ya RPC Barlow

Napenda conclusion za wabongo! Yaani kwa kuwa mtu aliuawa akiwa demu basi chanzo ni mapenzi tu!
Na polisi wamefurahi. wanajua itakuwa rahisi kuficha chanzo halisi cha tukio hilo.
Si ajabu jeshi lingeingia kwenye kashfa kubwa ingebainika kuwa Barlow na wakubwa wengine polisi wanahusika na ujambazi au uuzaji na uingizaji wa silaha.
Hapo ni mwanza, kumbukeni Darwin Nightmare!
 
kaka nakubaliana na wewe kwamba hawa jamaa issue ikiwausu wao au wakubwa wenye mamlaka katika nchi yetu wanachakarika haraka sana lakini kwa wengine inakuwa tofauti hebu vikiria maslani issue ya ulimboka si walijidai hawahusiki na wakaahidi kuwatafuta wahusika na kuwafikisha mbele ya sheria lakini hadi leo kiko wapi wamekaa kimya hata ulimboka aliporejea akiwa mzima hawajaenda kumuhoji kujua ilikuwaje kama sehemu ya uchunguzi wa hilo tatizo sasa wanajeuri gani ya kudai kuwa hawakuhusika? mbona issue ya baro ambeye aliuwawa na watu wasiofahamika wameza kuifanyia kazi na kuwatia wahusika mbaroni ndani ya muda mfupi sana?

Mkuu:Unauhakika waliokamatwa ndio wahusika wa kweli???
 
Nilisema hili haliwashindi polisi. Sasa tujiulize kama simu tu imeweza kufanikisha kukamatwa wahusika wote hadi simu iliyoibiwa siku ya tukio imepatikana. Nini kinashindiakana kupatiakana kwa watuhumiwa wengine kwa kutumia sayansi hiyo hiyo. Kabla ya Insp. Kuuwawa tulisoma sinza kuna dereva taksi aliuwawa asubuhi, tangu tangazo hilo hadi leo polisi wanachunguza majibu yatakuja siku dunia inaangamia.

Jeshi la polisi linataka kutuaminisha nini? Ikizingatiwa kuwa ajira za polisi ni last resort ya failures katika mfumo wa elimu ya Tanzania. Unless mtu anishawishi kuwa hali imebadilika kuna kuna the so called vipnaga wanaenda polisi baada ya elimu zao, bado nazindi kuamini wengi wa polisi wetu ni failures katika mfumo wetu wa elimu na wame opt kuchukua ajira hizo kwa upendelea maalumu baada ya kukosa pa kwenda. Nilipomaliza form six nilishauriwa kwenda polisi lakini baada ya kuchaguliwa kwenda chuo kikuu niliondoka bila kujali nilikuwa nimetumiakia kipindi gani na hilo lilitokea kwa wengin tu, walibaki wale ambao hawakuwa na pakwenda.
 
Wakubwa wetu kwa kupenda uroda. Barlow kimsingi amelipa deni lake kwa kupenda kudandia vya wenzake wakati ana vyake. Kabila hili kwa anko na kaka wamezidi. Utamsikia mtu akisema huyu ni anko au kaka kumbe hawara yake. Endeleeni kuumbuka kwa ujanja ujanja wenu uchwara. Au ndiyo kudumisha mila?
 
[h=2][/h]IJUMAA, OCTOBA 26, 2012 12:00 NA JOHN MADUHU, MWANZA

*Yumo mwanamke mmoja, wanaume wanne

JESHI la Polisi nchini, limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano wanaodaiwa kuhusika na kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mwanza, marehemu Liberatus Barlow. Pia jeshi hilo limefanikiwa kukamata bunduki iliyotumika kumuua kamanda huyo.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, aliwambia waandishi wa habari jijini Mwanza jana kuwa, watuhumiwa hao walikamatwa jijini Dar es Salaam ambako walikimbilia baada ya mauaji.

Katika mkutano huo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Said Mwema, naye alikuwapo.

Aliwataja waliohusika na mauaji hayo ambao bado wako jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda Mwanza, kuwa ni Muganyizi Peter (36) ambaye alitajwa na wenzake kuwa ndiye aliyefyatua risasi iliyomuua Kamanda Barlow.

Watuhumiwa wengine ni Chacha Mwita (50), Majige Marwa (48), Edward Kasutwa ambaye umri wake bado haujafahamika na mwanamke mmoja, Bhoke Mwita (42).

Pamoja na idadi hiyo, alisema Jeshi la Polisi bado linawasaka watuhumiwa wengine wawili waliokuwa katika tukio hilo.

Kwa mujibu wa DCI Manumba, kabla ya tukio hilo la mauaji, watuhumiwa hao ambao ni majambazi walikuwa wamefanya matukio matatu ya ujambazi katika maeneo tofauti jijini Mwanza kwa kupora vitu mballimbali kabla ya kukutana na Kamanda Barlow.

Alisema kwamba, watuhumiwa hao walifanya ujambazi kwa kuvamia Baa ya New Tuliza iliyopo eneo la Rumala majira ya saa nne usiku kwa kupora pombe na simu za wateja na kuondoka.

“Baadaye walivamia super market na kupora vitu mbalimbali na baadaye kumvamia mama mmoja na kumpora simu.

“Baada ya tukio hilo, ndipo walikutana na Kamanda Barlow na kumuua kwa kumpiga risasi shingoni kwa kutumia bunduki aina ya short gun na kufariki papo hapo.

“Walipokutana na Kamanda Barlow, watu hao walikuwa wakielekea Kitangiri kupumzika na walipomulikwa na taa za gari la kamanda, walimvamia wakati kamanda akigeuza gari na kuanza majibishano.

“Tukio hilo lilimfanya Kamanda achukue redio yake kwa ajili ya kutoa taarifa kwa wasaidizi na hapo ndipo walipomuua na haya ni kutokana na maelezo yao baada ya kuwahoji,” alisema.

Akizungumzia namna polisi walivyofanikiwa kuwatia nguvuni watuhumiwa hao, alisema Jeshi la Polisi liliamua kujipanga kikamilifu kwa kuunda vikosi mbalimbali vya ukamataji na kuhoji pamoja na kikosi cha kufuatilia matukio yote muhimu ya simu ndani na nje ya nchi.

Alisema kuwa, polisi walifanikiwa kupitia kikosi cha mawasiliano, kukamata simu iliyokuwa ikitumiwa na mwanamke aliyekuwa na Kamanda Barlow ambayo iliporwa na majambazi hayo wakati wa tukio na baadaye kuanza kutumiwa na mwanamke mmoja jijini Dar es Salaam.

“Baada ya polisi kumfuatilia mwanamke huyo, alitoa ushirikiano ambao ulifanikisha kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa jijini Dar es Salaam na walikutwa na silaha hiyo.

“Inasemekana pia watu hao walikuwa wamehusika na tukio la uporaji wa fedha katika kiwanda kimoja jijini Dar es Salaam.

“Baada ya kuwakamata watuhumiwa hao, walikiri kuhusika na tukio hilo la mauaji ya Kamanda Barlow pamoja na kukiri kuhusika na matukio mbalimbali ya mauaji na uhalifu katika maeneo mbalimbali hapa nchini,” alisema DCI Manumba.

Naye IGP alisema Jeshi la Polisi bado liko imara na limeimarika zaidi baada ya tukio hilo na kuonya kuwa halitawaonea huruma wahalifu.

Sasa kwanini FUMO FELICIAN bado wanamshikilia?

Hivi bado huyu mchezaji wa mpira wa miguu wa Timu ya Taifa na Pamba bado wanamshikilia? Vipi yule mwanamke aliyekuwa na kamanda, yeye habari zake zikoje?
 
Je Dr. Ulimboka hakuwa na haki ya kuishi? Je uhalifu uliotendewa Dr. hauna uzito sawa na wa Kamanda Barlow?
 
hongera jeshi kwa kazi nzuri. Lakini jeshi lisijisahaulishe wajibu wake wa kutulinda sisi RAIA, na kushughulikia matukio yetu kama wanavyoshughulikia matukio yanayogusa tabaka la juu
 
Yaani hawa majambazi waliogopa baada ya kumulikwa na Kamanda kuchukua redio call ila hawakuogopa kuacha witness (huyo dada wa kike) bali walimpora simu tu ambayo waliendelea kuitumia bila kuogopa kwamba itakuwa traced ?

Kweli hawa watakuwa amateurs... au things might not be as they seem..
 
  • Thanks
Reactions: FJM

Kwa mujibu wa DCI Manumba, kabla ya tukio hilo la mauaji, watuhumiwa hao ambao ni majambazi walikuwa wamefanya matukio matatu ya ujambazi katika maeneo tofauti jijini Mwanza kwa kupora vitu mballimbali kabla ya kukutana na Kamanda Barlow.

Alisema kwamba, watuhumiwa hao walifanya ujambazi kwa kuvamia Baa ya New Tuliza iliyopo eneo la Rumala majira ya saa nne usiku kwa kupora pombe na simu za wateja na kuondoka.

"Baadaye walivamia super market na kupora vitu mbalimbali na baadaye kumvamia mama mmoja na kumpora simu.

"Baada ya tukio hilo, ndipo walikutana na Kamanda Barlow na kumuua kwa kumpiga risasi shingoni kwa kutumia bunduki aina ya short gun na kufariki papo hapo.

"Inasemekana pia watu hao walikuwa wamehusika na tukio la uporaji wa fedha katika kiwanda kimoja jijini Dar es Salaam.

Naye IGP alisema Jeshi la Polisi bado liko imara na limeimarika zaidi baada ya tukio hilo na kuonya kuwa halitawaonea huruma wahalifu.

Kuna kitu hakiko sawa na maelezo ya polisi. Kwenye red polisi wanaonekana ku-suggest mauaji ya RPC Barlow yalifanywa na majambazi ambao waliokuwa kwenye harakati zao za wizi - wrong wrong time, wrong place theory!

Lakini kwa mtiririko wa matukio ambayo wamefanya hakuna mahali wameuwa au hata kujeruhi! So, why RPC Barlow yeye alipigwa risasi?

Inawezekana hao watu kweli walihusika lakini pia inawezekana kuna motive 'nzito' kuliko maelezo mepesi ya 'wapora simu na pombe'. Wapora simu na pombe wanatumia silaha? Polisi wavute pumzi, ndio, ni mwenzao lakini waepuke kufanya kazi kwa hasira.
 
IJUMAA, OCTOBA 26, 2012 12:00 NA JOHN MADUHU, MWANZA

*Yumo mwanamke mmoja, wanaume wanne

JESHI la Polisi nchini, limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano wanaodaiwa kuhusika na kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mwanza, marehemu Liberatus Barlow. Pia jeshi hilo limefanikiwa kukamata bunduki iliyotumika kumuua kamanda huyo.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, aliwambia waandishi wa habari jijini Mwanza jana kuwa, watuhumiwa hao walikamatwa jijini Dar es Salaam ambako walikimbilia baada ya mauaji.

Katika mkutano huo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Said Mwema, naye alikuwapo.

Aliwataja waliohusika na mauaji hayo ambao bado wako jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda Mwanza, kuwa ni Muganyizi Peter (36) ambaye alitajwa na wenzake kuwa ndiye aliyefyatua risasi iliyomuua Kamanda Barlow.

Watuhumiwa wengine ni Chacha Mwita (50), Majige Marwa (48), Edward Kasutwa ambaye umri wake bado haujafahamika na mwanamke mmoja, Bhoke Mwita (42).

Pamoja na idadi hiyo, alisema Jeshi la Polisi bado linawasaka watuhumiwa wengine wawili waliokuwa katika tukio hilo.

Kwa mujibu wa DCI Manumba, kabla ya tukio hilo la mauaji, watuhumiwa hao ambao ni majambazi walikuwa wamefanya matukio matatu ya ujambazi katika maeneo tofauti jijini Mwanza kwa kupora vitu mballimbali kabla ya kukutana na Kamanda Barlow.

Alisema kwamba, watuhumiwa hao walifanya ujambazi kwa kuvamia Baa ya New Tuliza iliyopo eneo la Rumala majira ya saa nne usiku kwa kupora pombe na simu za wateja na kuondoka.

"Baadaye walivamia super market na kupora vitu mbalimbali na baadaye kumvamia mama mmoja na kumpora simu.

"Baada ya tukio hilo, ndipo walikutana na Kamanda Barlow na kumuua kwa kumpiga risasi shingoni kwa kutumia bunduki aina ya short gun na kufariki papo hapo.

"Walipokutana na Kamanda Barlow, watu hao walikuwa wakielekea Kitangiri kupumzika na walipomulikwa na taa za gari la kamanda, walimvamia wakati kamanda akigeuza gari na kuanza majibishano.

"Tukio hilo lilimfanya Kamanda achukue redio yake kwa ajili ya kutoa taarifa kwa wasaidizi na hapo ndipo walipomuua na haya ni kutokana na maelezo yao baada ya kuwahoji," alisema.

Akizungumzia namna polisi walivyofanikiwa kuwatia nguvuni watuhumiwa hao, alisema Jeshi la Polisi liliamua kujipanga kikamilifu kwa kuunda vikosi mbalimbali vya ukamataji na kuhoji pamoja na kikosi cha kufuatilia matukio yote muhimu ya simu ndani na nje ya nchi.

Alisema kuwa, polisi walifanikiwa kupitia kikosi cha mawasiliano, kukamata simu iliyokuwa ikitumiwa na mwanamke aliyekuwa na Kamanda Barlow ambayo iliporwa na majambazi hayo wakati wa tukio na baadaye kuanza kutumiwa na mwanamke mmoja jijini Dar es Salaam.

"Baada ya polisi kumfuatilia mwanamke huyo, alitoa ushirikiano ambao ulifanikisha kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa jijini Dar es Salaam na walikutwa na silaha hiyo.

"Inasemekana pia watu hao walikuwa wamehusika na tukio la uporaji wa fedha katika kiwanda kimoja jijini Dar es Salaam.

"Baada ya kuwakamata watuhumiwa hao, walikiri kuhusika na tukio hilo la mauaji ya Kamanda Barlow pamoja na kukiri kuhusika na matukio mbalimbali ya mauaji na uhalifu katika maeneo mbalimbali hapa nchini," alisema DCI Manumba.

Naye IGP alisema Jeshi la Polisi bado liko imara na limeimarika zaidi baada ya tukio hilo na kuonya kuwa halitawaonea huruma wahalifu.

sasa mbona watuhumiwa waliomtesa Dr. Ulimboka hawajakamatwa hadi leo? kwahiyo aakiuawa/akiteswa polisi ndipo inahesabika haki ya mtu imekiukwa na hatua huchukuliwa. kwangu hizi sio habari bali ni ubakaji wa haki za binadamu
 
Back
Top Bottom