Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,400
Bado narudia,sijaona kosa kubwa la mtangazaji wa kiswahili,nilichogundua tunataka mswahili atamke kwa lafudhi ya nchi husika,hilo haliwezekani kwa sababu hata mzungu (kulingana na taifa lake)hawezi tamka maneno ya kiswahili kwa lafudhi ya kiswahili lazima atagongagonga lafudhi,ndio maana kuna mataifa j wanaita h,eg mtangazaji mmoja aliyekuwa redio one alikuwa anaitwa josef ndamalya,kwenye taarifa ya habari anajitambulisha kama josef ndamalya,,kwenye mipasho utasikia anajiita hozee ndamalya
Unafahamu kwamba hata hao wazungu wa Uingereza au kwingine wakitaka kutamka jina kikamilifu huwa wanauliza hata ubalozi wa nchi husika?
Hivyo majina ya kichina, kikorea au mengine yakiwa magumu kutamka basi wenzio huomba msaada wa ubalozi husika na kujifunza kutamka hilo jina.
Hili ni jambo la kawaida kabisa kufanywa na watu wenye uelewa.
Halafu watangazaji wa redio khasa wa mpira si vibaya wakawa wanajifunza haya majina kwani huleta burudani pia wakisikika kuyatamka, wanaonekana wanafahamu na wana uelewa na hata mzungu akisikia atatamani kusikiliza hivyohivyo.
Kutamka jina hakuendani kabisa na mambo ya lafudhi unayoongolea.