Watangazaji wetu kwanini hamjifunzi majina/maneno fulani yanatamkwaje?

RRONDO

RRONDO

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2010
Messages
35,325
Points
2,000
RRONDO

RRONDO

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2010
35,325 2,000
Unakuta mtangazaji Kwa kujiamini kabisa anatamka BALE(Kiswahili) badala ya beil. Au Lesesta(Leicester) badala ya kusema leista.

Leo nimemsikia mtangazaji gwiji wa michezo anatamka Brighton HoVE Kiswahili hove. Hii timu inaitwa Brighton & Hove(inatamkwa hov(u).

Hii timu ipo mji unaitwa Brighton and Hove City mji uliopatikana Kwa kuunganisha mji wa Brighton na Hove.
 
Richard

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Messages
10,362
Points
2,000
Richard

Richard

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2006
10,362 2,000
Bado narudia,sijaona kosa kubwa la mtangazaji wa kiswahili,nilichogundua tunataka mswahili atamke kwa lafudhi ya nchi husika,hilo haliwezekani kwa sababu hata mzungu (kulingana na taifa lake)hawezi tamka maneno ya kiswahili kwa lafudhi ya kiswahili lazima atagongagonga lafudhi,ndio maana kuna mataifa j wanaita h,eg mtangazaji mmoja aliyekuwa redio one alikuwa anaitwa josef ndamalya,kwenye taarifa ya habari anajitambulisha kama josef ndamalya,,kwenye mipasho utasikia anajiita hozee ndamalya
Unafahamu kwamba hata hao wazungu wa Uingereza au kwingine wakitaka kutamka jina kikamilifu huwa wanauliza hata ubalozi wa nchi husika?

Hivyo majina ya kichina, kikorea au mengine yakiwa magumu kutamka basi wenzio huomba msaada wa ubalozi husika na kujifunza kutamka hilo jina.

Hili ni jambo la kawaida kabisa kufanywa na watu wenye uelewa.

Halafu watangazaji wa redio khasa wa mpira si vibaya wakawa wanajifunza haya majina kwani huleta burudani pia wakisikika kuyatamka, wanaonekana wanafahamu na wana uelewa na hata mzungu akisikia atatamani kusikiliza hivyohivyo.

Kutamka jina hakuendani kabisa na mambo ya lafudhi unayoongolea.
 
RRONDO

RRONDO

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2010
Messages
35,325
Points
2,000
RRONDO

RRONDO

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2010
35,325 2,000
Unafahamu kwamba hata hao wazungu wa Uingereza au kwingine wakitaka kutamka jina kikamilifu huwa wanauliza hata ubalozi wa nchi husika?

Hivyo majina ya kichna, kikorea au mengine yakiwa magumu kutamka basi wenzio huomba masaada wa ubalozi husika na kujifunza kutamka hilo jina.

Hili ni jambo la kawaida kabisa kufanywa na watu wenye uelewa.

Halafu watangazaji wa redio khasa wa mpira si vibaya wakawa wanajifunza haya majina kwani huleta burudani pia wakisikika kuyatamka, wanaonekana wanafahamu na wana uelewa na hata mzungu akisikia atatamani kusikiliza hivyohivyo.

Kutamka jina hakuendani kabisa na mambo ya lafudhi unayoongolea.
Boss nimegundua watu wana uelewa mdogo sana. Kuna mpumbavu mwingine eti kafungua thread kujibu nilichoandika.
 
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Messages
6,128
Points
2,000
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2018
6,128 2,000
Unakuta mtangazaji Kwa kujiamini kabisa anatamka BALE(Kiswahili) badala ya beil. Au Lesesta(Leicester) badala ya kusema leista.
Leo nimemsikia mtangazaji gwiji wa michezo anatamka Brighton HoVE Kiswahili hove. Hii timu inaitwa Brighton & Hove(inatamkwa hov(u). Hii timu ipo mji unaitwa Brighton and Hove City mji uliopatikana Kwa kuunganisha mji wa Brighton na Hove.

Hili tatizo lipo sana. Huwa nawaambia watu wajaribu kuwasikiliza wenye lugha zao vipi wana yatamka maneno yao. Hii ipo mpaka kwenye lugha yetuya Kiswahili.
 
Richard

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Messages
10,362
Points
2,000
Richard

Richard

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2006
10,362 2,000
Boss nimegundua watu wana uelewa mdogo sana. Kuna mpumbavu mwingine eti kafungua thread kujibu nilichoandika.
Zipo "tools" au zana na njia kadha wa kadha za kujifunza hivyo hii mada yako umeleta wakati sahihi na mahala sahihi maana wengine hata Kiswahili tu ni shida.

Hata kama umesoma au unafanya kazi ya kitaalam kama hivyo ya utangazaji mpira au hata habari unapaswa uwe na uelewa wa namna ya kutamka majina.

Hivyohivyo kwa watu wa external affairs wao ndo kabisa inabidi watafute watu husika wa ubalozi na kijifunza.

Hata mimi nimegundua kuna tatizo kubwa sana la uvivu wa kujifunza na kutaka kuelewa na mtu kukataa kukubali kuwa unakosea mahala.

Ukishakubali unakosea basi unakuwa tayari kujifunza lakini utakuta mtangazaji kusika anajiunga na JF na anaanza kubisha mpaka kuchwee.
 
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Messages
6,128
Points
2,000
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2018
6,128 2,000
Bado narudia,sijaona kosa kubwa la mtangazaji wa kiswahili,nilichogundua tunataka mswahili atamke kwa lafudhi ya nchi husika,hilo haliwezekani kwa sababu hata mzungu (kulingana na taifa lake)hawezi tamka maneno ya kiswahili kwa lafudhi ya kiswahili lazima atagongagonga lafudhi,ndio maana kuna mataifa j wanaita h,eg mtangazaji mmoja aliyekuwa redio one alikuwa anaitwa josef ndamalya,kwenye taarifa ya habari anajitambulisha kama josef ndamalya,,kwenye mipasho utasikia anajiita hozee ndamalya
Hivi lafudhi ndio lahaja au ?

Maana hapa nataka niseme kitu.
 
RRONDO

RRONDO

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2010
Messages
35,325
Points
2,000
RRONDO

RRONDO

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2010
35,325 2,000
Zipo "tools" au zana na njia kadha wa kadha za kujifunza hivyo hii mada yako umeleta wakati sahihi na mahala sahihi maana wengine hata Kiswahili tu ni shida.

Hata kama umesoma au unafanya kazi ya kitaalam kama hivyo ya utanganzaji mpira au hata habari unapaswa uwe na uelewa wa namna ya kutamka majina.

Hivyohivyo kwa watu wa external affairs wao ndo kabisa inabidi watafute watu husika wa ubalozi na kijifunza.

Hata mimi nimegundua kuna tatizo kubwa sana la uvivu wa kujifunza na kutaka kuelewa na mtu kukataa kukubali kuwa unakosea mahala.

Ukishakubali unakosea basi unakuwa tayari kujifunza lakini utakuta mtangazaji kusika anajiunga na JF na anaanza kubisha mpaka kuchwee.
Mkuu umeelezea umuhimu wa nilichoandika kiufasaha zaidi.
 
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Messages
6,128
Points
2,000
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2018
6,128 2,000
Mkuu nisaidie utamkaji wa jina la beki kisiki wa Bayern Munich Matts Hummels. Hilo jina la pili huku kwetu kila mtu anatamka kivyake
Mfano leo umkute mtu asie jua Kiswahili,ukamuandikia tamko "Mbu" katika sentensi hii :
"Hii sehemu kuna mbu wengi sana"
Kisha ukamwambia asome,bila shaka tamko "mbu" atalikosea achilia mbali hayo mengine. Hapa namaanisha lazima urudi kwa wenye lugha yao uangalie wanatamka maneno hayo au kwa yule anae jua lugha husika.
 
Richard

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Messages
10,362
Points
2,000
Richard

Richard

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2006
10,362 2,000
Hivi lafudhi ndio lahaja au ?

Maana hapa nataka niseme kitu.
Lafudhi ni "accent" na lahaja ni "variant".

Ni tofauti ya kutamka neno pamoja na eneo analotoka mtu, na asili yake.

Variant au lahaja ni aina mbalimbali ya matamshi ya neno lakini hayaharibu maana.

Kwa mfano neno Malaria lina kila aina ya matamshi na lahaja.

Hivyo utamsikia sauti mbalimbali na mitindo mbalimbali ya kutamka hilo neno kutoka kwa mtanzania, mmarekani na muingereza.

Hivyo neno "Malaria" akitamka mtanzania utafahamu anatoka Tanzania hali kadhalika mmarekani kutoka Marekani na muingereza kutoka kwa Malkia Elizabeth wa pili.

Nafikiri tuombe msaada zaidi wa wataalam wa ligha au "linguist" kama wapo hapa.

:):).
 
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Messages
6,128
Points
2,000
Z

Zurri

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2018
6,128 2,000
Variant au lahaja ni aina mbalimbali ya matamshi ya neno lakini hayaharibu maana.
Upo sahihi kabisa na nina kuunga mkono kwa asilimia mia,ila hapa ulitakiwa uongezee tamko "lugha moja" ili kuleta maana ya wazi zaidi.

Mfano lafudhi huwa imejikita sana katika mtoko wa sauti,mathalani ukimsikiliza mpare akiongea Kiswahili au mchaga utajua kutokana na sauti invyosikika na hii huwa ina athiriwa sana na maeneo husika kama ulivyosema.

Na lahaja inaingia katika lugha moja lakini lugha hiyo inakuwa ina zungumzwa katika mtindo tofauti hasa wa kimsamiati ukiambatana na mtoko wa herufi. Mathalani kuna lahaja ya Kimvita,Kiamu,Kipete,Kipemba,Kiunguja hizi zote ni lahaja za Kiswahili yaani wote wanazungumza Kiswahili,ila tofauti yao unaikuta katika matamshi kadhaa,kama sijapoteza kumbukumbu,mfano "Macho" kwa Kiamu hutamkwa "Mato" na mfano wake.

Nukta yangu ya msingi ni kumwambia yule niliye mnukuu kule juu,na ndio nilichokuwa nataka nikiseme ni kuwa "Lafudhi sio sababu ya kumfanya mtu ashindwe kutamka jina la watu wa lugha kando kwa ufasaha"
 
Richard

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Messages
10,362
Points
2,000
Richard

Richard

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2006
10,362 2,000
Martin Tyler na Peter Drury katika kusuma kwangu padi naskiaga wanasema,

"Wainaldam"
Ila herifi W yatamkwa V na penye A yatamkwa O

Kulitamka kirahisi jina gumu kama hili unatakiwa kulivunja kwa silabasi.

wi-j-nal-d-um hapa umegawa jina kwa silabasi na kwa mishale.

Ukiishaligawa kwenye silabasi unaaza kutamka moja baada ya ingine ili kuliwezea na mwisho kulitamka kikamilifu.

  • W - wuh, silent
  • I - ah-ee, ĭ
  • J - juh
  • N - nuh
  • A - æ, ā, ah, ā-uh, uh
  • L - luh, ul
  • D - duh
  • U - uh, yoo, oo, ů
  • M - muh

Wijnaldum

Duh! kazi ipo, ngoja ninywe maji kwanza.

:) :)
 
Richard

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Messages
10,362
Points
2,000
Richard

Richard

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2006
10,362 2,000
Upo sahihi kabisa na nina kuunga mkono kwa asilimia mia,ila hapa ulitakiwa uongezee tamko "lugha moja" ili kuleta maana ya wazi zaidi.

Mfano lafudhi huwa imejikita sana katika mtoko wa sauti,mathalani ukimsikiliza mpare akiongea Kiswahili au mchaga utajua kutokana na sauti invyosikika na hii huwa ina athiriwa sana na maeneo husika kama ulivyosema.

Na lahaja inaingia katika lugha moja lakini lugha hiyo inakuwa ina zungumzwa katika mtindo tofauti hasa wa kimsamiati ukiambatana na mtoko wa herufi. Mathalani kuna lahaja ya Kimvita,Kiamu,Kipete,Kipemba,Kiunguja hizi zote ni lahaja za Kiswahili yaani wote wanazungumza Kiswahili,ila tofauti yao unaikuta katika matamshi kadhaa,kama sijapoteza kumbukumbu,mfano "Macho" kwa Kiamu hutamkwa "Mato" na mfano wake.

Nukta yangu ya msingi ni kumwambia yule niliye mnukuu kule juu,na ndio nilichokuwa nataka nikiseme ni kuwa "Lafudhi sio sababu ya kumfanya mtu ashindwe kutamka jina la watu wa lugha kando kwa ufasaha"
Tupo pamoja mkuu.
 
troublemaker

troublemaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2015
Messages
6,367
Points
2,000
troublemaker

troublemaker

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2015
6,367 2,000
Ila pes wamewapiga bao sana fifa kwenye watangazaji. Pes watangazaji ni wazuri sana wa supersport3.

Allan na martin wala huwa siwakubali aisee.
haha.
nmemaanisha watangazaji wote kutoka kwenye hizo title mbili za FIFA na PES wote hutamka sawa, "JIOJINO WAINALDAM"
 
Forum statistics

Threads 1,296,485
Members 498,655
Posts 31,249,869
Top