Watangazaji waache unafiki

Watangazaji waache unafiki

Technologiest

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2017
Posts
3,727
Reaction score
4,060
Habari za jioni wanajukwaa!
Leo natiririka hapa kuwazungumzia hawa wanataaluma wanaojita prizentaz,hasa wa redio tena Redio moja hapa mjini cjui inatangazia mawinguni eti,hasa hawa wa kipindi cha jioni nadhani kuna kacheo wanafukuzia ama laa watakua makada wakubwa! Kimsingi kama wameamua kuwa makada wajikite huko ama laa wafanye kazi yao kwa maadili ya kazi sio kupenda kushabikia na kujipendekeza ili waonewe huruma! Kipindi kizima hakuna mada ya msingi ya kujadili ila kuwakejeli watumishi ambao wanachodai sio hisani bali haki yao kisheria kulingana na mikataba waliyosaini! Ila niseme tu ukiona mwenzako ananyolewa zako tia maji,leo watumishi wanalia kesho itakua zamu yao hakuna alie salama!
Mimi kama Mtanzania mwenye utimamu siwezi kufurahia maslahi ya Watumishi yanavyopigwa teke kwani natambua nahitaji huduma kutoka kwa hao hao Je,nitahudumiwa vzr na mtu mwenye msongo wa mawazo? Huyo huyo anadaiwa pango,karo,mchango,dukani nk bila shaka attention ya kunihudumia itatoweka pia naweza kupata huduma mbovu,nadhani kama wanahabari walipaswa kuchambua kwa kina mambo kabla ya kushabikia otherwise matokeo ya kinachopandwa kitavunwa na kila Mtanzania wa maisha ya kawaida na chini kwakua huduma zote ikiwamo afya&elimu tunategemea hapahapa nchini na sio nje.
 
Huwa namshangaa sana kiporomoko anavojitahidi kufafanua mambo asiyoyajua ili kumfurahisha sizonje.hilo jahazi linapoteza wasikilizaji.
 
Mwanzoni mitaani wengi walifurahia wapiga dili kutumbuliwa. Na sasa wameshajua kuna walakini kwenye suala hili la kuwapunja maslahi watumishi. Maana zile ajira binafsi za ufundi,ushonaji,uashi,biashara,ujasiriamali,n.k sasa hazipo tena baada ya watumishi kupunguza matumizi ya lazima na ziada.

Bahati mbaya Mkulu anadhani bado ni kiki kwa wasio watumishi kuwabana watumishi ambao yeye anaona ni kama tabaka nyonyaji. Wamebaki wachache wasioelewa kama hao watangazaji.
 
We ulikuwa ujui wapiga dili wazuri hao,tena naomba hicho kipindi kingekuwa na maswali tuwaulize,wananajifanya wanajua sana mambo kumbe seti tupu tu hao jamaa
 
Tatizo akina Jerry Muro na Pascal Mayala wapo wengi wanaishi kutegemea post za kuteuliwa kwa kujipendekeza kwa Makonda.
Baada ya Zirro kupanda cheo kwa kumkingia kifua Makonda kwenye kwenye kampeni yake ya kula rushwa kwa kusingizia watu madawa ya kulevya kila mtu anafikiri kwamba Makonda ni daraja ili uteuliwe na rais
 
Huwa namshangaa sana kiporomoko anavojitahidi kufafanua mambo asiyoyajua ili kumfurahisha sizonje.hilo jahazi linapoteza wasikilizaji.
Umri wake na anachobwabwaja aibu tupu!
 
Mwanzoni mitaani wengi walifurahia wapiga dili kutumbuliwa. Na sasa wameshajua kuna walakini kwenye suala hili la kuwapunja maslahi watumishi. Maana zile ajira binafsi za ufundi,ushonaji,uashi,biashara,ujasiriamali,n.k sasa hazipo tena baada ya watumishi kupunguza matumizi ya lazima na ziada.

Bahati mbaya Mkulu anadhani bado ni kiki kwa wasio watumishi kuwabana watumishi ambao yeye anaona ni kama tabaka nyonyaji. Wamebaki wachache wasioelewa kama hao watangazaji.
The time will tell! Nawadiss sana mbwa hawa
 
We ulikuwa ujui wapiga dili wazuri hao,tena naomba hicho kipindi kingekuwa na maswali tuwaulize,wananajifanya wanajua sana mambo kumbe seti tupu tu hao jamaa
Sure! Ndomana hawaruhusu msg zozote kama wenzao wengine wanajua watayaoga
 
Afrika bado tupo level ya production for consuption
Hapo lazima ukishiba unawaza kutafuta tena kwa ajili ya mlo ufuatao ila sio production for surplus.
 
Tatizo akina Jerry Muro na Pascal Mayala wapo wengi wanaishi kutegemea post za kuteuliwa kwa kujipendekeza kwa Makonda.
Baada ya Zirro kupanda cheo kwa kumkingia kifua Makonda kwenye kwenye kampeni yake ya kula rushwa kwa kusingizia watu madawa ya kulevya kila mtu anafikiri kwamba Makonda ni daraja ili uteuliwe na rais
Kila jambo lina mwisho wake
 
Yaani wale watu wazima huwa wanajadili upumbavu na kushabikia mada za kipuuzi pamoja na matusi. Ni km 'gogozembe' tu! Heri wale wa ndinga mpya town eadrive.
 
Back
Top Bottom