Utafiti: Watanzania asilimia 80 wataka Bunge ‘Live’

Utafiti: Watanzania asilimia 80 wataka Bunge ‘Live’

Tunkamanin

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2015
Posts
955
Reaction score
867

Kwanza niwapongeze waliofanya mchakato huu wa kufanya utafiti, ili kujua uhalisia wa mambo kwa wananchi wa tanzania. Hongera watu wa tume ya haki na utawala bora, mmeonesha ushujaa na ukakamavu wa kutafuta ukweli na kuuweka hadharani, hivi ndivyo inavyopaswa kuwa; kuwapitia wananchi na kujua kama wanachukuliaje suala zima la bunge kuwa gizani, na je faida ni nyingi kuliko hasara zake? nimeipenda pia slogan iliyokaa kwenye kichwa cha utafiti, OUR COUNTRY OUR PARLIAMENT
wito kwa viongozi wengine, wajaribu kutafiti baadhi ya mambo yanayofanywa na serikali yetu ili kujua kama raia wanayachukuliaje,
Nchi hii ni yetu sote:

=============


TAASISI ya Twaweza imetoa matokeo ya utafiti wake, ambapo imebainika kuwa asilimia 79 ya Watanzania wamepinga uamuzi wa Serikali wa kusitisha matangazo ya moja kwa moja (Live ) ya Bunge.

Katika maoni yao, wananchi hao wamedai kuwa ni haki yao ya msingi kufahamu kinachoendelea katika vikao mbalimbali vya Bunge.

Utafiti wa taasisi hiyo umefanywa katika maeneo tofauti ya Tanzania Bara kupitia mpango wake wa Sauti za Wananchi.

Akitoa taarifa ya matokeo ya utafiti huo jana jijini Dar e Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze, alisema suala hilo limeonekana kutokuungwa mkono na wananchi wengi.

“Asilimia kubwa ya Watanzania wanapinga uamuzi wa Serikali wa kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge. Suala hili limeonekana kugusa hisia za watu wengi na maamuzi haya ya Serikali yakionekana kutoungwa mkono.

“Katika utafiti huu wananchi nane kati ya 10 wanapinga uamuzi wa hali inayodhihirisha kutoungwa mkono kwa hatua hiyo,” alisema Eiyakuze.

Akizungumzia sababu walizozitoa wananchi wanaotaka matangazo ya Bunge yarushwe moja kwa moja, Eiyakuze alisema asilimia 46 walisema yanawafanya waweze kufuatilia utendaji wa wabunge waliowachagua kwa kuwa huko ndio walikowatuma.

“Asilimia 44 wanasema ni muhimu kwa sababu wananchi wanahaki ya kufahamu kinachoendelea bungeni, asilimia 29 wanasema matangazo ya moja kwa moja yalikuwa yanaaminika zaidi kwa watazamaji na wasikilizaji kuona na kusikia wenyewe kile kinachoendelea tofauti na mfumo wa kurekodi ambapo kuna baadhi ya mambo yanahaririwa.

“Asilimia 16 walidai kuwa inafursa mwananchi kupata taarifa sahihi badala ya kuzisoma kwenye magazeti huku asilimia 16 nyingine wakisema inawasaidia wanachi kufuatilia mijadala ya Bunge kwa wakati”, alisema Eiyakuze.

Pamoja na hali hiyo mkurugenzi huyo alisema katika utafiti huo asilimia 92 ya wananchi walisema kuna umuhimu wa vipindi vya Bunge kurushwa moja kwa moja kupitia Luninga na redio bila kujali gharama zilizoelezwa kuwa ndio chanzo cha kufikia uamuzi huo.

“Asilimia 88 walisema vipindi vya Bunge virushwe ‘Live’ bila kujali gharama ukilinganisha na asilimia 12 ambao waliona ni muhimu suala la bajeti likazingatiwa,” alisema.

Mkurugenzi huyo alisema asilimia 80 wanaona matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni ni muhimu kama yalivyo na asilimia 20 wakisema fedha hizo zitumike kwenye huduma nyinge za jamii.

Akizungumzia suala la vyombo vya habari vya binafsi kuruhusiwa kurusha matangazo hayo, Eiyakuze alisema wananchi wanaunga mkono vyombo hivyo kuruhusiwa iwapo Serikali imeshindwa kumudu gharama.

Utafiti huo pia umeonesha Watanzinia wanne kati ya kumi wamewahi kuangalia matangazo ya moja kwa moja kupitia Luninga na sita kati ya kumi wamesikiliza kupitia redio.

Aidha utafiti huo umeonyesha zaidi ya nusu ya wananchi walosema wameangalia au kusikiliza vipindi vya Bunge wamefanya hivyo ndani ya miezi miwili iliyopita.

Hali ilivyokuwa

Januari mwaka huu, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, alitoa ufafanuzi bungeni kuhusu hatua ya Serikali kusitisha matangazo hayo kupitia Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC).

Miongoni mwa sababu alizozieleza ni pamoja na kuwepo kwa gharama kubwa ya Sh bilioni 4.2 zinazotumika katika uendeshaji wa matangazo hayo ya moja kwa moja kwa mwaka pia watumishi wa serikali kushabikia Bunge badala ya kuendelea na kazi ofisini.

Hatua ya Serikali kusitisha matangazo hayo iliibua mjadala mkubwa bungeni huku Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, (ACT-Wazalendo) akilitaka Bunge kusitisha shughuli zake ili kujadili taarifa hiyo ya Serikali.

Siku chache baadaye kilio hicho cha ukosefu wa fedha za kuonesha matangazo hayo ya moja kwa moja ambacho kimekuwa kikitolewa na serikali, sasa kilipata ufumbuzi.

Hatua hiyo iliyokana na uamuzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari nchini (TMF), kujitokeza hadharani na kueleza kwamba upo tayari kutoa fedha zinazohitajika ili kuhakikisha haki ya Mtanzania kupata habari kupitia TBC haiingiliwi wala kubughudhiwa kwa hoja yoyote.

Endapo Serikali itakubali ombi hilo, wananchi wataendelea kunufaika na vikao vya moja kwa moja vya Bunge tofauti na pendekezo la serikali la kunakili baadhi ya sehemu na kisha kuoneshwa usiku.

Mtanzania
 
Twaweza walisema JPM anakubalika 96% watu waka pinga, leo bunge live twaweza wanasema ukweli. Mmm
 
Huu ni ukweli lakini hii pia inaweza kuwa ni mbinu ya Mkuu wa Kaya kutaka kujirudi baada ya kugundua watu wamemchoka kwa anayoyafanya ila lazima awe na sababu au awe na pa kuanzia katika kujirudi kwake na huenda huu utafiti ndio ukaja kuwa sababu ya kujirudi.

Watasema tumezingatia maoni ya wananchi kurudisha Bunge live kumbe wameshaona wanajiharibia ila walikuwa wanakosa sababu ya kuwaambia wananchi kwanini sasa wanaamua kurudisha matangazo hayo.Hapa Twaweza wameshawasaidia.
 
Hizi fafiti za TWAWEZA hizi! .... hebu waachane nazo zina fifisha uwezo wa TZ kufikiri. Watu wanaacha kutafiti masuala ya maana ili kukuza teknokojia tupate maendeleo wao kutwa kucha kuchukua story za kwenye vijiwe vya kahawa na kuziunganisha halafu wanaita press kuzitangaza eti nao ndio 'utafiti' !
 
Hawa TWAWEZA ni wanafiki wakubwa..

Suala hili walipaswa kuliuliza pale kwenye tafiti zao za mwanzo lakini sasa baada ya kuona jamaa amevurunda kwa kiasi cha kutosha ndio wemeweka huu utafiti ikiwa kama njia ya jamaa kurudi kwenye mstari.

Hii ni kwa sababu haiwezekani kwa utafiti wao mmoja kusema jamaa anakubalika kwa 96% halafu jamaa akiwa na percent kubwa namna hiyo kuwe na 88%ya wanaotaka bunge lirejeshwe. Lazima katika ile 96%pia wengi waliunga mkono bunge lisiwe live.. Ndio kumuunga kwenyewe mkono huko.

Tafiti za kupika kwenye makaratasi na sio kwenda field kwenye reality zitaendelea kuwaumbua sana nyie TWAWEZA...

It's high time mbadilishe na hilo jina lenu.. Mpo kinyume nalo..!!
 
Lakini BORA WASIRUDI KUWA LIVE, maana nasikia kuwa gizani kumewafichia mengi kwani hoja za Wanene wa Chama Tawala Bungeni nasikia ni aibu na fedheha kwa kila kikao.
 
Hii ni hatua nzuri. Hingera. Sababu za kusitisha hazikuwa za kitafiti bali za kimamlaka
 
Magu hatakubali bunge live,sababu majibu yanayotolewa na Jennister Mhagama,Ummy Mwalimu ,Mwijage na.Mwakyembe ni fedheha kwa serikali.

Wabunge wa ccm na naibu spika ni aibu tupu
 
Mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na utawala bora Tom Nyanduga amesema ripoti ya kuzuiwa matangazo ya bunge ya moja kwa moja, kumeathiri sana wananchi
Utafiti huo umehusisha wananchi wa kawaida na wabunge, wananchi wamedai kusitishwa kwa bunge kumeathiri uelewa wao wa kinachoendelea bungeni na nchini kwa ujumla na hawajui wabunge wao wanawawakilisha vipi
 
Mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na utawala bora Tom Nyanduga amesema ripoti ya kuzuiwa matangazo ya bunge ya moja kwa moja, kumeathiri sana wananchi
Utafiti huo umehusisha wananchi wa kawaida na wabunge, wananchi wamedai kusitishwa kwa bunge kumeathiri uelewa wao wa kinachoendelea bungeni na nchini kwa ujumla na hawajui wabunge wao wanawawakilisha vipi

ni kweli
 
Mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na utawala bora Tom Nyanduga amesema ripoti ya kuzuiwa matangazo ya bunge ya moja kwa moja, kumeathiri sana wananchi
Utafiti huo umehusisha wananchi wa kawaida na wabunge, wananchi wamedai kusitishwa kwa bunge kumeathiri uelewa wao wa kinachoendelea bungeni na nchini kwa ujumla na hawajui wabunge wao wanawawakilisha vipi

Hiyo ni taarifa njema kwa CCM maana ndilo lilikuwa lengo lao.
 
MAHITAJI ya wananchi kutaka matangazo ya Bunge la Muungano kuonyeshwa moja kwa moja katika vituo vya televisheni na redio yamezidi kushika kasi, imebainika.

Utafiti uliofanywa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) umeonyesha asilimia 92 ya wananchi wanaona kuna umuhimu wa matangazo hayo ya Bunge kurushwa moja kwa moja huku asilimia 79 wakipinga uamuzi wa Serikali kuyafuta matangazo hayo.

Akizindua ripoti kuhusu kusimamishwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge, Mkurugenzi wa MCT, Pili Mtambalike, alisema hatua hiyo inakandamiza uhuru wa habari na haki ya kupata taarifa.

Katika ripoti hiyo ambayo pia imenukuu utafiti uliowahi kufanywa na Taasisi ya Twaweza ya Dar es Salaam, Mtambalike alisema utafiti huo uligundua kuwa wananchi wengi walioulizwa walilalamika na kusema kuwa baada ya kufungiwa matangazo hayo hawajui kitu gani kinaendelea ndani ya Bunge.

Alisema katika utafiti huo, watu wanane kati ya 10 hawajakubaliana na kufungwa matangazo hayo huku tisa kati ya 10 wanaona kuna umuhimu matangazo hayo yakarudishwa.

“Ripoti hii inapendekeza matangazo hayo yarudishwe yaweze kuwasaidia wananchi wa kawaida kufuatilia mijadala mbalimbali ya bunge.

“Waandishi wa habari za bunge pia wajengewe uwezo waweze kuandika habari hizo kwa weledi mkubwa.

“Ripoti hii inapendekeza pia kuwa kanuni za Bunge zitumike katika kukomesha tabia zisizotakiwa bungeni badala ya kuvilaumu vyombo vya habari vinapokuwa vikitoa habari na kuonyesha kinachoendelea bungeni,”alisema Mtambalike.

Ripoti hiyo imetoa mapendekezo kwa uongozi wa Bunge hilo kutaja hadharani gharama halisi za kurusha matangazo hayo ya moja kwa moja ili wananchi waelewe.

“Tunapendekeza kuwapo mfuko maalum utakaojulikana kama Fedha za Matangazo ya Bunge (BBF) unaojitegemea, ambao utapata fedha kutoka nje na ndani ya Bunge,” alisema Mtambalike.

Ripoti hiyo pia imesema kuwa si kweli kwamba utaratibu wa kurusha matangazo hayo haufanywi na Nchi za Jumuiya ya Madola kama ilivyoelezwa na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye wakati akielezea sababu za kufunga matangazo hayo.

“Katika utafiti huu tumegundua kuna nchi sita duniani ambazo zinaruhusu urushwaji wa moja kwa moja wa redio na runinga kama Australia, Uingereza, Canada, New Zeland na Samoa ambako redio ya taifa inalazimishwa na sheria kutangaza kila siku au kwa wiki, jinsi Bunge linavyofanya kazi yake zake,” ilisema sehemu ya ripoti hiyo.
 
Siasa tuweke pembeni na mambo ya msingi yaruhusiwe, kama TBC1 hawana hela watu binafsi wanaweza kurusha .
 
Back
Top Bottom