Kaya Nogu Sabho Ndamu
Member
- Sep 4, 2016
- 44
- 28
Jamani wandishi wa habari, leo hii ni mara ya pili nasikia mkiweka mada zisizo na maana kwenye chombo cha habari e-fm.
Mfano leo nimesikia mnajadili habari kuhusu wanawake weusi na wanawake weupe kanda ya ziwa, kwanini mwanamke mweupe anatolewa mahari kubwa kuliko mweusi. Waendesha mada ni Gerald Hando, Adera, na wengine.
Maoni yangu hii mada iondoeni haraka iwezekanavyo kwa sababu zifuatazo:
1. Haina maana wala haijengi jamii ila inatengeneza matabaka kati ya weusi na weupe, jambo hili mnaliona kama ni dogo lakini linasababisha psychological tortures kwa wasiofahamu na kujifahamu. Unapo weka mada yoyote kwenye chombo cha habari jiulize swali naweka mada hii so what? Ninavyoona swali hili halikuzingatiwa na waanzisha mada hivyo nashauri itolewe na isisikike tena. Tukiendekeza mambo haya mtaleta mada za mwanamke mnene na mwanamke mwembamba, msukuma na mmakonde haya mambo hayafai
2. Nashauri kina mama wanawake wakemee mada za namna hii hazina maana ila ni kuwadhalilisha tu.
3. Michael Jackson alifikia sehemu akajibadilisha akawa na pua ndefu na nyembamba kwa sababu ya mambo kama haya ya kijinga. Walikuwa wanamwambia anapua nene naye akaona bora atafute pua nyembamba.
Mwisho naomba hawa walioanzisha mada hii wahakikiwe vyeti vyao.