Watangazaji wa Clouds wengi wao hawana taaluma kabisa

Watangazaji wa Clouds wengi wao hawana taaluma kabisa

Kwenye kipindi cha leo tena, wakiwa wanaongelea suala la vifo vilivyotokea Moshi kwa Mwamposa, Maoni ya watangazaji Geah Habibu na Mussa Hussein yamenishangaza sana, wameshindwa kuficha hisia zao za kuonyesha wapo upande gani wa kidini na kutoa maoni ya kishabiki.

Geah Habibu na Mussa Husseni wanadai eti Serikali iingilie kati madhehebu yote ya kikristo yaliyoibuka hivi karibuni yafungwe, yabaki madhehebu ya zamani tu (Roma na Lutheran), hawakuishia hapo wakadai pia Babu wa Loliondo naye aliwahi kuwa kiongozi wa dini ya Kikristo hapo sijui anamaanisha nini.

Watangazaji wengi wa bongo hawana uweledi wanaongozwa na mihemko sana, wanavyosema hakuna mafuta ya upako huko wanaingilia masuala ya kidini, yapo au yasiwepo ilitakiwa waongee kiuweledi sio kiushabiki.

Sent using Jamii Forums mobile app


Hawajakosea kwani wasanii wengi dizaini ya kina tapeli Mwamposa, Gwajima, wako wengi mno na wanazidi kupotosha watu tu. Corona imeingia Tanzania sasa, umesikia mchungaji yeyote kati ya hawa kaja na tiba? Ikiisha corona utawasikia wako bize kufufua misukule na kuponya watu kwa njia ya mafuta ya upako. This is utterly stupid, HAKUNA mchungaji wala nabii yeyote hapa duniani aliye mkweli, wote ni matapeli tu na wasanii wakubwa na hii corona ndiyo imewaumbua kishenzi. Yet kwa ujinga, utaona watu bado wanakwenda kuwasikiliza na kugombania mafua ya upako pamoja na kupepewa na upepo wa kisulisuli ili wapate wanaume wakati wenyewe hawana mabwana.
 
Back
Top Bottom