Watangazaji wa Clouds wengi wao hawana taaluma kabisa

Watangazaji wa Clouds wengi wao hawana taaluma kabisa

Heisenberg blue meth

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
1,310
Reaction score
1,633
Kwenye kipindi cha leo tena, wakiwa wanaongelea suala la vifo vilivyotokea Moshi kwa Mwamposa, Maoni ya watangazaji Geah Habibu na Mussa Hussein yamenishangaza sana, wameshindwa kuficha hisia zao za kuonyesha wapo upande gani wa kidini na kutoa maoni ya kishabiki.

Geah Habibu na Mussa Husseni wanadai eti Serikali iingilie kati madhehebu yote ya kikristo yaliyoibuka hivi karibuni yafungwe, yabaki madhehebu ya zamani tu (Roma na Lutheran), hawakuishia hapo wakadai pia Babu wa Loliondo naye aliwahi kuwa kiongozi wa dini ya Kikristo hapo sijui anamaanisha nini.

Watangazaji wengi wa bongo hawana uweledi wanaongozwa na mihemko sana, wanavyosema hakuna mafuta ya upako huko wanaingilia masuala ya kidini, yapo au yasiwepo ilitakiwa waongee kiuweledi sio kiushabiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Geah Habibu, Mussa Husein halafu unalalamika mkuu

Ingawa sishabikii vifo vilivyotokea
 
Hayo n maoni yao hii n nchi ya kidemokrasia kila MTU ana haki ya kutoa maoni kuna sehemu wamevunja katiba?

Pia wewe toa maoni yako sio unalalamika tu au umefurah ndugu zetu kukatishwa maisha kizembe na huyo nabii feki
 
Ni kweli hawakupaswa kuliongelea hilo jambo kwa namna ile ya mzaha na kejeli kwa kiasi kile....angalau Josse Mara alijitahidi ku balance ila hakufanikiwa kutuliza munkari wa mashambulizi yao
 
wajinga jose. mara kawapa mpaka kifungu cha biblia ,kuusu kukanyaga mafuta,,wanaropokaropoka tu
 
Sheria ile inayowataka wawe na walau diploma imeishia wapi? ni watangazaji wangapi wa hiyo redio wana japo diploma au ndio redio ya ma MC?
 
Sheria ile inayowataka wawe na walau diploma imeishia wapi? ni watangazaji wangapi wa hiyo redio wana japo diploma au ndio redio ya ma MC?
Wote hao wamesoma,labda kasoro Jose..kuwa na diploma au degree ya journalism sio guarantee ya wao kuwa 100% professional..

Shida ya Watangazaji wengi bongo ni kujifanya kila kitu wanaweza au wanakijua,mfano,kuchambua habari iwe ni ya kisiasa,uchumi,kijamii,kiimani n.k kitu ambacho ni wrong
 
Watu wamekufa kwa kugombea kukanyaga mafuta ya upako! Kila mtu ana haki ya kuchangia jambo hili. mbona miaka mingi hakukua na mafuta ya aina hiyo.!!
 
Back
Top Bottom