Watangazaji wa aina hii ni janga la taifa

Chona

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
523
360
Si kawaida yangu kumattack mtu personally ila kwa hili nimeshindwa kujizuia. Nilipata msituko baada ya kusikiliza vidokezo vya habari kwenye taarifa ya habari ya leo 30 july 2013 saa 2 usiku iliyotangazwa kwenye kituo cha redio cha Radio One.
Kisa chenyewe ni kwamba mtangazaji wakati anatangaza akatamka kuwa 'Mogan Tsvanjilai mgombea uraisi Zimbabwe amesema kuwa kama atashinda kiti cha uraisi ATAlipiza kisasi kwa hasimu wake Robert Mugabe. Baada ya kusikiliza taarifa kamili nikagundua kutokana na maelezo yake kuwa ilitakiwa atamke HATalipiza kisasi. Kiukweli mwanzo nilistuka . Nikajiuliza kwanini Mogani Tsvanjelai alipize kisasi! Kumbe watangazaji wetu hawapo makini licha ya kwamba wanasoma.
Swali, Je ni uzembe wa mtangazaji? Au ni mfumo mbovu wa elimu yetu kiasi kinachomfanya mtu asione kuwa kuna tofauti ya kimatamshi nahivyo kuleta tofauti ya maana kwa maneno hayo.
 
Ni kweli sametime wanakosea sana ktk kutangaza kwao... Msamehe ndo watangazaji wa shule za kata hao.
 
Ukosefu wa umakini na ubovu wa Elimu yetu Kaka. tuvumiliane tu mkuu ndo tumefika hapo.
 
Kaka wewe ni mhamiaji nchi hii? Inawezekana ile kali ya naibu waziri wa Elimu,Mh Philipo A.Mulugo ulikuwa hujahamia bado nchi hii!!( Ilikuwa Oktober 2012,aliposema Tanganyika ilitokana muungano wa Zimbabwe na Pemba aliongea kwa lugha inaoyofanana na kingereza!)
 
Ukosefu wa umakini na ubovu wa Elimu yetu Kaka. tuvumiliane tu mkuu ndo tumefika hapo.

Ukitaka kujua ni majanga kiukweli anza na spelling check kwenye magazeti ya kiswahili na kumalizia na matamshi yao.Anza tu na neno kuahirisha usikie au kuona wanavyoliandika.watu wasio makini unaweza kuwa-judge kwa vitu vidogo sana!
 
Ukitaka kujua ni majanga kiukweli anza na spelling check kwenye magazeti ya kiswahili na kumalizia na matamshi yao.Anza tu na neno kuahirisha usikie au kuona wanavyoliandika.watu wasio makini unaweza kuwa-judge kwa vitu vidogo sana!

Shughuli ilikuwa pale ilipizama meli ya MV spice islander, kila mtangazaji alikuwa anatamka kivyake hilo jina, hasa hilo neno 'islander' limesumbua watangazaji wengi sana.
 
Back
Top Bottom