TCRA yaipa onyo kali TBC1 kwa kosa la Ubaguzi wa kusoma habari za Magazetini

klorokwine

JF-Expert Member
Nov 4, 2014
378
27
MAMLAKA ya mawasiliano nchini (TCRA) imekipa onyo kali -kituo hicho kwa kitendo chake cha kubagua kusoma taarifa zinazohusiana na vyama vya siasa. Hukumu hiyo ilitolewa leo jijini Dar es Salaam na kamati ya maudhui ya utangazaji, katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Walter Bugoya wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo

Bugoya amesema kamati hiyo imebaini TBC one imekiuka sheria ya utangazaji ya mwaka 2005 -pamoja na sheria ya uchaguzi ya mwaka 2015 baada ya kufanya upendeleo wa vyama katika taarifa zake kwenye kipindi.

Amedai katika kipindi cha Jambo Tanzania kilichorushwa tarehe 15 mwezi huu majira ya saa 12 asubuhi hadi saa tatu,katika kipingele cha uchambuzi wa magazeti ambapo mtangazaji wa kipindi hicho alikuwa anayasoma magazeti huku akiruka kusoma habari kuu husika.

Amesema Mtangazaji huyo alipokuwa anachambua gazeti la Majira na Nipashe alidanya umma jambo ambalo amedai ni kosa. Bugoya ametaja makosa hayo ni wakati- mtangazaji huyo alipokuwa anasoma Gazati la Majira -ukurasa wake wa mbele alisema habari kubwa ni "CCM yazidi wambua wanaomfuata lowassa" wakati habari -kubwa ilikuwa inasomeka hapo ni ile inayosema "Mbeya kwafurika"huku picha ya gazeti hilo likionyesha picha ya umati watu pamoja na mgombea wa Urais wa chadema Edward lowassa akihutubia.

Amesema mtangazaji huyo pia alifanya kosa jengine kama hilo pia wakati akisoma Gazeti la Nipashe ambapo alisema Habari iliyopewa uzito wa kipekee ni- "Mbalawa atoa sheria ya mitandao"- ambapo habari iliyopewa uzito ilikuwa ni ile ilikuwa "Mafuriko Mbeya" na sio aliyokuwa anaisoma yeye.

Amesema baada ya Kamati yake kubaini makosa hayo waliwasiliana na mkurugenzi wa TBC one Bwana Mshana ambao mkurugenzi huyo alitoa utetezi wake kwenye kamati hiyo akisema mtangazaji huyo ajafanya kosa kwakuwa alikuwa ajaridhika na taarifa zilizokuwa zimeandikwa kwenye magazeti hayo.

Sanjari na hayo Mshana alizidi jitetea akidai kuwa hata mtangazaji huyo -hata asingesoma habari ile lakini picha iliyokuwa inaonekana kwenye magazeti hayo teyari mtazamaji alikuwa ashajua kwahiyo amedai haikuwa na ulazima wa kusomwa.

Bugoya amesema baada ya kusikiliza upande wa TBC one ndio wakabaini kituo hicho kilikiukaka sheria ya utangazaji ya Mwaka 2005 ambayo inavitaka vituo vyote vya utangazaji nchini kuripoti taarifa kwa kutokuwa na upendeleo wowote.

Amesema Kamati imefikia uamuzi wa kuipa onyo kali kwa TBC one na endapo wakiendelea basi Mamlaka hiyo haitasita kuwachukulia hatua kali zaidi.

Hatua hii imekuja baada ya wanachama wa JamiiForums kuilalamikia TBC1 katika hii thread=>
TBC yadanganya, hatua stahiki zichukuliwe .

Wakati huo Magic FM imetozwa Mil 2.5.

Magazeti ya leo Jumamos 29/08/2015 yameandika
;

Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), imetoa onyo kali kwa Shirika la Utangazaji (TBC1) kwa kuchambua vichwa vya habari vya magazeti kwa upendeleo.

Kadhalika Redio ya Magic FM imepewa onyo kali huku ikitakiwa kulipa faini ya Sh milioni 2.5 baada ya kukiuka maadili ya utangazaji kupitia kipindi chake cha 'Morning Magic'.

Uamuzi huo ulitolewa jana jijini Dar es Salaam katika mkutano wa waandishi wa habari wakiwemo wawakilishi kutoka TBC1 na Magic FM, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Wolter Byoga, alisema TBC1 kupitia kipindi chake cha Jambo Tanzania, katika kipengele cha uchambuzi wa magazeti kilikuwa kikiruka habari kubwa na kusoma ndogo.

Alisema mtangazaji alikusudia kuruka habari hizo jambo linaloonyesha upendeleo wakati habari ya siku ya Agosti 15, mwaka huu ikiwa moja ya mjadala mkubwa nchini ilitakiwa kusomwa bila ya kuangalia maslahi ya upande mwingine. Aliongeza Gazeti la Nipashe liliandika "Mafuriko Mbeya" ikiwa na picha ya mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chadema, ilirukwa.

Alisema kamati iliangalia kipindi hicho na kubaini kumefanyika ukiukwaji wa huduma za utangazaji zilizowekwa katika maudhui ya kipindi cha dondoo.

Katika utetezi wao ulioandikwa na Mkurugenzi wa TBC, Clement Mshana, alisema kama Shirika hawapangiwi habari za kusoma na pia picha ambazo zilizokuwa kwenye gazeti zilionekana kama za kutengenezwa.

Byoga alisema kamati haijaridhishwa na utetezi huo na kusisitiza ukiukwaji wa maudhui ya utangazaji na kuwapa onyo kali na kwamba wakirudia watachukuliwa hatua kali zaidi.

Akisoma makosa ya kipindi kilichokuwa kinaendeshwa na Magic FM, Byoga alisema Julai 16, mwaka huu katika kipengele cha paka rangi, walichambua katuni katika moja ya gazeti na kumtaja jina waziwazi mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli, jambo ambalo ni kinyume na sheria ya utangazaji.

Kosa lingine walilifanywa katika kipengele hicho kupitia mtangazaji wake Orest Kawawu, ni kuitafsiri picha hiyo kwa kuihusisha na imani za dhehebu la Katoliki katika kumpata kiongozi wa kanisa hilo ‘Papa' jambo ambalo linaweza kuleta chuki kwa waumini wa dini hiyo.

Watangazaji katika kuendelea kutafsiri katuni hiyo, walisema ule moshi uliochorwa ni mfano wa moshi mweusi unaotoka wakati wa kumtafuta Papa, jambo linaloashiria kwamba aliyependekezwa hafai.
Chanzo: Nipashe
 
Last edited by a moderator:
MAFURIKO ya watu yanayotokea wakati wa mgombea Urais wa vyama vinvyounda UKAWA Edward lowasssa ni kama yameanza kukiponza Kituo cha Tevelevisheni cha TBC one ndivyo naweza kusema baada MAMLAKA ya mawasiliano nchini (TCRA) kukipa onyo kali kituo hicho,kwa kitendo chake cha kubagua kusoma taarifa zinazohusiana na vyama vya siasa.


Hukumu hiyo ilitolewa leo jijini Dar es Salaam na kamati ya maudhui ya utangazaji, katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Walter Bugoya wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo



Bugoya amesema kamati hiyo imebaini TBC one imekiuka sheria ya utangazaji ya mwaka 2005 pamoja na sheria ya uchaguzi ya mwaka 2015 baada ya kufanya upendeleo wa vyama katika taarifa zake kwenye kipindi.

Amedai katika kipindi cha Jambo Tanzania kilichorushwa tarehe 15 mwezi huu majira ya saa 12 asubuhi hadi saa tatu,katika kipingele cha uchambuzi wa magazeti ambapo mtangazaji wa kipindi hicho alikuwa anayasoma magazeti huku akiruka kusoma habari kuu husika.

Amesema Mtangazaji huyo alipokuwa anachambua gazeti la Majira na Nipashe alidanya umma jambo ambalo amedai ni kosa.


Bugoya ametaja makosa hayo ni wakati mtangazaji huyo alipokuwa anasoma Gazati la Majira ukrsa wake wa mbele alisema habari kubwa ni "CCM yazidi wambua wanaomfuata lowassa" wakati habari kubwa ilikuwa inasomeka hapo ni ile inayosema "Mbeya kwafurika"huku picha ya gazeti hilo likionyesha picha ya umati watu pamoja na mgombea wa Urais wa chadema Edward lowassa akihutubia.

Amesema mtangazaji huyo pia alifanya kosa jengine kama hilo pia wakati akisoma Gazeti la Nipashe ambapo alisema Habari iliyopewa uzito wa kipekee ni "Mbalawa atoa sheria ya mitandao" ambapo habari iliyopewa uzito ilikuwa ni ile ilikuwa "Mafuriko Mbeya" na sio aliyokuwa anaisoma yeye.

Amesema baada ya Kamati yake kubaini makosa hayo waliwasiliana na mkurugenzi wa TBC one Bwana Mshana ambao mkurugenzi huyo alitoa utetezi wake kwenye kamati hiyo akisema mtangazaji huyo ajafanya kosa kwakuwa alikuwa ajaridhika na taarifa zilizokuwa zimeandikwa kwenye magazeti hayo.


Sanjari na hayo Mshana alizidi jitetea akidai kuwa hata mtangazaji huyo hata asingesoma habari ile lakini picha iliyokuwa inaonekana kwenye magazeti hayo teyari mtazamaji alikuwa ashajua kwahiyo amedai haikuwa na ulazima wa kusomwa.


Bugoya amesema baada ya kusikiliza upande wa TBC one ndio wakabaini kituo hicho kilikiukaka sheria ya utangazaji ya Mwaka 2005 ambayo inavitaka vituo vyote vya utangazaji nchini kuripoti taarifa kwa kutokuwa na upendeleo wowote.


Amesema Kamati imefikia uamuzi wa kuipa onyo kali kwa TBC one na endapo wakiendelea basi Mamlaka hiyo haitasita kuwachukulia hatua kali zaidi.

Nyongenza:


Wakati huohuo kituo cha Redio cha Magic FM baada ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA kukipiga faini ya milioni 2.5 pamoja na kupewa onyo kali baada kituo hicho kutangaza taarifa zenye uchochezi wa kidini.
 
huyu bwana clement mshana ni janga kabisa afukuzwe kazi mara moja, analeta ukada kwenye chombo cha uma?

Inaonekana wafanyakazi wa tbc1 wanafanya kazi kwa mashinikizo kutoka kwa mkurugenzi mkuu, bwana mshana,

tbc siyo mali ya bwana mshana na genge lake, tbc na mali yangu mimi na wewe,

hiki ni chombo cha uma. Kinaendeshwa na sisi wananchi kwa kulipa kodi zetu,

sasa hivi tbc imepoteza kabisa mvuto haina hata ladha ya kuangalia, ni habari za ccm mwanzo wa asubui mpaka jioni,

vipindi vyake hovyo kabisa, shirika hili likiendelea kuwa chini ya mshana ni lazima lifilisike kabisa maana litashindwa hata kujiendesha, maana shirika litakua limekosa wateja,

mshana na genge lake wajufunze kwa nchi ya jirani kenya, vyombo vya uma vipo huru, havifungamani na upande wowote viko fair, tofauti na hapa kwetu ni haibu haibu,
 
siku ile niliuliza swali humu kama TBC hawataweza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kudanganya umma lakini sikupata ufafanuzi. kumbe inawezekana! basi iwe mwanzo wa kutofumbia macho mambo ya uongo na upotoshaji wa dhahiri unaofanywa na vyombo vya habari, dola kama polisi au vingine vyovyote

mbarikiwe
 
Kwani UKAWA wameshazindua kampeni? Utaanzaje kutangaza mambo ya chama ambacho hakijazindua kampeni? CCM ilishazindua muda.
Utatangazeje habari za kampeni za chama ambacho hakijazindua? Huyo Bugoya vipi?
 
Asante maana wanakera kuinyesha mahaba niue kwa ccm. Huku wakijisahau kuwa sote ni Watanzania wenye haki sawa. Pia Tbc yetu sote walipa kodi. Siyo Tv ya Chama fulani.
 
TBC1 Imepoteza mvuto kabisa!!!

Mgeni akifika kwangu na kumwagiza mtu yeyote hapa kwangu awashe TV akakosea na kusema aweke TBC 1 basi jibu lake ni moja tu hapa kwetu huwa hatuangalii TBC 1.
 
Kwani UKAWA wameshazindua kampeni? Utaanzaje kutangaza mambo ya chama ambacho hakijazindua kampeni? CCM ilishazindua muda
Usiwe na mahaba niue muda mwingine utaonekana mwehu kwa jamii. Mbona habari za ACT na vyama vingine ambavyo havina nguvu mbona wanazisoma bila tatizo. Wanashindwa nini kusoma za UKAWA? Hiyo ni Television ya Taifa na si ya Ccm.
 
Huo utetezi wa mgurugezi wala siyo utetezi, eti kwavile picha inaonyesha mafuriko basi hakuna haja ya kuisoma hiyo taarifa!

Kwanza kwa kitendo cha kuruka habari kuu iliyobeba gazeti, kinazuia habari hiyo kuenea kwa watanzania walio wengi, pia kitendo hicho kinaharibu biashara ya gazeti husika.

Na tbc1 wala siyo mara yao ya kwanza kufanya hivyo, na hilo kalipio lisiwe upande wa usomaji magazeti tu, bali hata utoaji taarifa wao unaegemea upande mmoja.
 
Back
Top Bottom