Watangazaji Mmetuangusha sana!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watangazaji Mmetuangusha sana!!

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by babykailama, Apr 1, 2012.

 1. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nimesikia ITV wakanza kuuliza maswali elekezi mfano "hivi kweli matokeo yatatoka leo au tusubiri hadi kesho"

  Mzee Masako another failure maana mlianza asubuhi kwa kusema hatutatoka hapa mpaka kieleweke. Yaani mmechoka na pia mjue ninyi mmekuwa sehemu ya vurugu. Mwana habari yuko chumbani kwenye kiyoyozi anaamua kwenda kulala je vipi walioko field???
  Nimesikitika sana maana ninyi mngekuwa chombo cha maana hata usiku wote kushauri watu watulie! Nimesikitika sana; Yaani kuambia kuna mabomu ya machozi ninyi mnajitoa ?? Ahaaa nimepata mshtuko sana nanyi wewe Masako na dada yangu.

  Yaani mnachokitangaza ni kama maigizo??


  Je mnajua hasira za wananchi mnaposeema matokeo yahairishwe mpaka kesho? Nani kawambia kuwa Jeshi la Polisi limeshindwa kudhibiti hali?

  Aha Fatuma dada yangu why I trusted you so much !! Rais juzi kaonya na kukumbusha Role ya wanahabari katika kuchochea vurugu! Ebu tafuteni kahawa na chai msilale na ninawaamuru kwa jina la umoja msitoke hapo mlipo tupeni habari na msianze kuwa biased basi. Mfawidi wenu awalipe posho ya kuwa usiku mzima kituoni hii ni kawaida.
   
 2. LOWE89

  LOWE89 Senior Member

  #2
  Apr 1, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  na hao wameanza
   
 3. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Aaarghhh...
   
 4. N

  Ngoiva JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  masako ni ccm damu damu. Nakumbuka Igunga mbona waliganda mwanzo mwisho!
   
 5. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,350
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Masako kwenye kutangaza ccm ilipobahatisha kura nyingi kanatangaza kwa sauti kweli, yaani hicho kibabu kimenibore sana, anyway tym yao inaelekea kutokomea/iko gizani wataondoka hivi punde na magamba yao,
   
 6. cmoney

  cmoney JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 1,224
  Likes Received: 740
  Trophy Points: 280
  ah ah wadau huyo naye magamba mbona nasikia ameshawahi kugombea ccm akatolewa kwe kura za maoni
   
 7. G

  GODWIN KITOMARI New Member

  #7
  Apr 1, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kitaeleweka tuu..
   
 8. Kilahunja

  Kilahunja JF-Expert Member

  #8
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 1,497
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  yan mtu asilale kisa? Labda wabadilishiwe zam nao ni watu na wanachoka.
   
 9. B

  Ba Oasis Member

  #9
  Apr 1, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mtangazaj wao anaeanzia USA kuelekea kikatiti anaambiwa msimamiz kasema wanaeza tangaza kesho anajibu;"itakua vizur wakitangaza kesho". What d hell?
   
 10. m

  mchongi Senior Member

  #10
  Apr 1, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  amenikera kwa sababu kama chombo huru cha habari mnalala ili atuhabarishe nani? eti wametoka wakaweka mizengwe duh tanzania news coverage bado kabisa... TBC hao wala siwahesabu maana wao ni idara ndani ya wizara na ni wasemaji wa serikali ni UMMA.. ebu jifunzeni kwa wenzetu kenya wanavyoreport matukio ya nchi yao kwa ueledi wa hali ya juu.!
   
 11. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  peoples poweerrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
   
 12. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #12
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Yaani hata mimi ingawa ni CCM wameni bore sana. Anayesema wamechoka basi wangetoka tu na waingie wengine waendeleze. Sikiliza kuna sababu kubwa sana za kuendelea.

  1.Ukiahidi kitu lazima utimize. Hakuna aliye walazimisha Asubuhi kabisa wao walisema wakati wote watakuwa live mpaka watoe matokeo.

  2.Watanzania wana haki ya kupata habari tena ya muhimu kama hii. Uchaguzi huu si mdogo (ingawa ni mdogo kieneo) Ndio maana hata Rais mstaafu, Waziri mkuu Mstaafu, Mawaziri n.k walifika na kupiga kampeni. Je ITV hamjawahi kushuhuduia vyombo vya wenzetu wanavyo pokezana na kuchambua kwa takwimu ukutani jinsi matokeo yanavyoingia mpaka asubuhi? Je hamjaona watu wako Studio saa zote wanaendelea kuripoti zoezi la uokoaji watu waliokuwa machimboni?

  3. Kila Mtumishi hata Wachezaji, wana ndoto na dhamira za kufanya vyema kazini au katika chochote wakifanyacho kwenye Public ili ikiwezekana wazidi kuaminiwa kwa performance zao. Hivi ninyi hamna ndoto za hivyo? Hamkumbuki Meya wa NY alipanda chati ghafla kwa kuoneka kuwa anajishughulisha bila kuchoka (24/7) baada ya tukio baya la tisa kumi na moja. Hivi mnafikiri kwa nini,vipindi kama 360 au Situation Room n.k vinaheshimika na pia Watangazaji wake wanaheshimika? Hakika kweli nadhani angekuwepo ndg. Gondwe asingetoka na angetumia hata kaprojector (non touch screen) kutujuza kinachoendelea na kuonyesha umahiri wake kama mhitimu wa MA Mass Com!

  4. Mbona Msimamizi wa Uchaguzi mliongea naye wala yeye hakusema kuwa wanasitisha shughuli pamoja na kukiri kuwa kuna fujo za hapa na pale.

  Agrhhh! Ni Watu kama ninyi na yule Mh. wetu aliyeporomosha matusi kweupe (na watu wote sasa wana kile kipande toka You Tube kama ushahidi) mnaofanya tutukanwe kuwa TUNACHAKACHUA KURA HATA KAMA WATU WAMENYUKWA KI-UKWELI.

  Hivi kwa nini tunakosa Mastrategist wanaofikiri nje ya viota vya zamani? Ukweli ni kwamba mazungumzo ya Mzee wetu Masako na mwenzake yalikuwa yachekesha sana hasa wakianza kusema 'Oh! hivi kweli shughuli itaendelea kwa hali hiyo?' LOL, yaani vibomu vitatu tu vya machozi kutawanyisha kundi linaloziuia watu kuleta kura panapojulmlishiwa ninyi mnaanza kulalama. Na kile kichekesho cha eti mmoja wenu gari lake limeanguka sijui mtoni / mtaroni sasa ajali za binafsi nazo ziwe sababu ya kuacha kutoa taarifa. Hivi ninyi mliwahi kucover news kwenye battle ground hata siku moja?

  Mweshimiwa Mengi naona kuna umuhimu wa hawa Wanahabari (na zaidi pia wale wa TBC wakati fulani wapelekwe kwenye mazoezini rasmi ya mazingira ya danger zones yaliyotengenezwa kama huko kwenye makambi ya JKT ili wajifunze maana bila stadi za maisha ya kivita / ktk fujo basi watakuwa wanakimbia ovyo na pia kuumia kizembe sana!
   
 13. m

  mkbcoool Member

  #13
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Igunga walijua watu hawajastukia uhakika walikuwa nao kwamba wamechakachua na kitaeleweka. Weeeeeeeeeeee wamechemsha leo.
   
 14. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #14
  Apr 2, 2012
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wana - Habari watujibu kwa nini wanafanya mambo ya namna hii. Unajua hii ni hujuma kwa namna nyingine sawa na ile ya mtu kupanda jukwaani na kuanza kuporomosha matusi eti niwachane nisiwachane?????
   
Loading...