No! 1991 ilikuwa, Sifa nyingine ya Charlz ni namna alivyokuwa akiwa nick name wachezaji, na kuwaelezea kiasi kwamba hata sisi wa nje ya Dar tulihisi kama vile tunawaona na pia hata simulizi zake za hapa na pale, mfano aliposema kuna mchezaji alikwenda kupiga penalt akapiga fyongo na mpira ukatoka ukawa wa kurusha badala ya goal kick. Niliishiwa mbavu kwa kicheko1993 kama sijakosea
Mimi 10 bora wangu ni hawa:
1.Mshindo Mkeyenge
2.Omary Jongo
3.Dominick Chilambo
4.Charles Martin Hilary
5.Barthlomeo Komba
6.Ahmed Jongo
7.Salim Mbonde
8.Abdallah Idrisa Majura
9.Mikidad Mahmoud 'Brother Mick" na
10.Abdul Ngarawa
Kikubwa zaidi walichokuwa nacho hao tunowasifia ni uwezo mkubwa waliokuwa nao wa kutambua matukio hata kabla ya mwamuzi kupuliza filimbi, mfano atakwambia offside kabla hata refa hajapuliza filimbi, faulo zote walikuwa wanazijua na wapi zitaelekezwa, move za magoli wanaziona na nyingine huzaa goli, mfano mechi ya Pamba na Anse Bailou ya ushelisheli, ile ya goli 12-0,Chilambo (RIP), anasema goli la tisa hilo naliona,wakati huo Nico Bambaga yupo katikati ya uwanja na mpira na kweli inakwenda kuwa goli.WanaJF,mmetosheka na kuridhika kuwa hawa waliotajwa ni watangazaji bora wa mpira Tanzania?
aah Huko Kenya Lenard Mambo Mbotela ' kadenge ina mupira ,kadenge inakwenda,kadenge napiga njenga lakini golikipa Tairus Omondi nakamata.
e bwana eheee, hao ndo wenyewe, wewe hata sasa silikila bbc ulimwengu wa soka, utapendaaaaamechi ya Simba na Villa mtangazaji alikuwa Charles Hillary na alipoanza kutaja kikosi cha Villa ilikuwa balaa kwani kabla hajafika kwa sentahafu kule mpira ulikuwa umeshaanza na ghafla akakatiza kutaja kikosi cha Villa kisha akapiga yowe la Goooooooooooooooo....halafu akasema ''namna gani pale...ni goal Kick...alikwenda vizuri sana pale Majid Musisi, lakini Frank Kasanga Bwalaya alisimama imara pale...namna gani pale Jamhuri kihwelu Mrema alikuwa kazubaa''....halafu akaendelea kutaja kikosi
jamani nimefurahi sana.. tatizo hawa vijana wa siku hizi, wanachakachua sana, ahwan ubunifu.....No! 1991 ilikuwa, Sifa nyingine ya Charlz ni namna alivyokuwa akiwa nick name wachezaji, na kuwaelezea kiasi kwamba hata sisi wa nje ya Dar tulihisi kama vile tunawaona na pia hata simulizi zake za hapa na pale, mfano aliposema kuna mchezaji alikwenda kupiga penalt akapiga fyongo na mpira ukatoka ukawa wa kurusha badala ya goal kick. Niliishiwa mbavu kwa kicheko
Mkuu, huyo namba 10, ni noma. Mwaka 1982 Challenge Cup, Stars ya Jeff Allan Hudson pale Nairobi, mechi na Ethiopia, tuko mbele 1 - 0, mara kona inapigwa na Ethiopia wanasawazisha. Akasema la la la.....aaa, goo..... kum...............mae wamerudisha!
bigup sana wandugu. Asante kwa aliyeleta thread maana wachangiaji bila yeye msingetupa nyepesi nyepes kama hizi.
Si mnamkumbuka Dada Halima Mchuka...Yule mtangazaji wa mpira wa kwanza wa kike hapa Tanzania!, siku hizi hasikiki katika kituo chake cha kazi, Zamani Redio Tanzania na sasa TBC Taifa kwa sababu alipata maradhi ya kupooza upande wa kulia miaka minne iliyopita. Katika mahojiano yake na mtangazaji kutoka Mlimani TV, Halima amesema alisaidiwa sana na Mr. Mchata(RIP) katika kufanikisha ndoto zake za kuwa mtangazaji wa kike wa mpira wa miguu. Ameongeza kuwa mechi yake ya kwanza ilikuwa kati ya SIMBA na YANGA...Dada Halima anaendelea kuuguza maradhi yake ya kupooza akikaa na Ndugu yake huko Mikocheni...na bado ana imani kuwa atarudi katika hali yake ya kawaida ili andelee na kazi yake ya utangazaji.....WanaJF naomba tumkumbuke katika sara dada yetu Halima Mchuka apone haraka ili afanikishe lengo lake kuu la kuwa mtangazaji bora wa kike Duniani kama alivyotamka mwenyewe.
Source: Mlimani TV/Jarida la habari/22-05-2011...