Watakaoshindwa Kidato cha Pili kuendelea cha Tatu

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Mfumo wa elimu yetu unaonekana kuwa na matatizo mengi na ubora wake unaendelea kwenda chini. Moja ya matatizo ni kwamba kila waziri wa elimu anayekuja anakuja na mambo mapya na hivyo tunakosa 'continuity'.

Enzi za utawala wa amu ya tatu tuliona jinsi waziri wa elimu alivyovuruga mfumo wa elimu yetu kwa kubadilisha 'sylabus' na kuondoa michezo mashuleni. Enzi za awamu ya kwanza kulikuwa na michezo na kilimo (bustani/mashamba) mashuleni. Siku hizi sijui kama michezo na kilimo vipo bado.

Katika awamu ya nne tumeanza pia kuona mabadiliko, ambayo, kwa mtazamo wangu, hayataboresha elimu yetu bali yataiangamiza kabisa.

Kuwapo kwa mtihani wa kidato cha pili uliwapa wanafunzi msukumo wa kujifunza kwa vile walijua wasipofanya hivyo hawataingia kidato cha tatu - yaani, hawataendelea na masomo ya sekondari.

Tumesikia waziri mwenye dhamana ya elimu amesema kuanzia sasa mtihani utakuwa tu kuwapima wanafunzi na ufundishaji wa waalimu lakini watakaoshindwa wataruhusiwa kuendelea na kidato cha tatu.

Lakini kuwafanya wanafunzi watakaoshindwa mtihani wa kidato cha pili kuendelee na kidato cha tatu kutawafanya wanafunzi wengi wajisahau na kudhani kidato cha nne, tano na sita ni mbali na matokeo yake yatakuwa kushindwa zaidi.

Kitu muhimu cha kufanya katika kuinua kiwango cha elimu yetu, ambayo kwa kweli, inaendelea kwenda chini ni pamoja na kuboresha maslahi ya waalimu, kuwatayarisha waalimu na wanafunzi kwa namna bora zaidi - kutowafundisha namna ya kujibu maswali bali kuwafundisha kuelewa wanachofundishwa ili wakiulizwa maswali waweze kujibu vizuri na kuwepo mazingira yatakayowawezesha kujifunza kwa juhudi na maarifa.
 
Back
Top Bottom