Wataka kusoma China? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wataka kusoma China?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Kilongwe, Dec 15, 2008.

 1. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Jamani nakumbuka huu ndio muda ambao wanafunzi wengi ambao wanataka kuja kusoma China huwa wanajaza fomu na kutafuta vyuo huku,sasa katika kuwasaidia watanzania wenzangu na watu wengine,nimedesign hii website ambayo nadhani itakuwa na information za kumwaga kuhusu vyuo vya China hususan hapa Wuhan mji wa elimu na ndio wenye wanafunzi wengi,nikiwa pia kama kiongozi wa watanznaia ninajua tabu ambazo watu huzipata kuanzia kutafuta chuo hadi siku ya kufika kutokana na lugha kuwa utata.
  hivyo kama unaweza kutembelea hii website www.fostiw.com au ukaenda kwenye hii link Fostiw-Education
  Unaweza kuwasiliana webmasters ambao wote ni watoto wa nyumbani.(Mimi na Mzee Jesse)
  Kila la kheri wakuu.Lazima ipo siku kitaeleweka tu.
   
 2. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 135
  Naogopa tetemeko! LOL!
   
 3. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #3
  Dec 15, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kinacho nishangaza ni kwa nini Wachina ndiyo soko kuu la vyuo katika nchi za Magharibi na hasa UK?. Elimu ya China ina kiwango kinachotakiwa hasa kwa maendeleo ya Tanzania ya leo?, Je kwa nini vitu vingi fake vinavyochomwa moto bongo vinatoka China?.

  Ninajua kutakuwa na vyuo vizuri tu China ila tuwe makini na selection ya vyuo huko, maana hata nchi za magharibi kuna vyuo vyenye grade ya chini. Ila bado sijapata jibu la wachina kujazana vyuo vya UK bado.
   
 4. h

  halikuniki Member

  #4
  Dec 15, 2008
  Joined: Aug 6, 2007
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni kweli kabisaaaaa,hili lazima lifanyiwe kazi
   
 5. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #5
  Dec 15, 2008
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa tuwe wadadisi na haya mavyuo ya ughaibuni. Manake vipo vingi ambavyo ni feki kabisa.
   
 6. Kilongwe

  Kilongwe JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 424
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Wakuu hili ni haswaa,wachina wapo tata sana,elimu yao imekaa kimtegomtego,nina maana ukiivagaa tu umeumia,Ni kweli kuna wachina wengi hujazana nje,na hii ni kwa sababu kuu mbili,
  Moja,nchi huwa inawapeleka watu nje kwenda kuiba ujuzi then kurudi nao nyumbani,na wengi wanaopelekwa na serikali ni watu wa Phd au Masters,huwezi kusikia undergraduate kapelekwa nje na serikali kwani wenyewe wanaamini kuwa kumjua adui yako ni moja ya ushindi.
  Pili.Kwa china ili uingie vyuo vilivyo kwenye kumi bora,kama hichi ninachosoma na upate kozi murua,kusema kweli ni kazi ya ziada,ndio maana ukiwaona wachina hapa wa zile kozi tamu kama Computer ,telecom,MIS,...huwa kama mibwege hii kutokana na mzigo unaowakabili na ushindani.sasa wale watoto wa wenye hela wanaona isiwe tabu ni bora nimpeleke mwanangu nje.
  La mwisho, wachina ni wasanii,kama haupo makini unaweza ukajikuta unapelekwa chuo sicho au wakikupeleka chuo kizuri basi unapewa kozi za ajabu,la msingi ni kujua haya kabla hujaja ndio maana nikawaalert watu mapema.
  Kama utaweza kukabiliana na haya yote,mimi naona kwa fani za science,unaweza kuja China kwani jambo zuri ni kuwa kama unajua kichina vizuri,basi wao material yapo wazi sana kwa watu wao,centers zipo kibwena,nina hakika 100% utatoka ukiwa fiti tena ukizingatia kwa mwendo tunaoenda ni kuwa zaidi ya 50% ya technology yetu tunawategemea wachina,hivyo lazima wapatikane watu ambao wanawaelewa wachina vzuri.
  Ila usisahau,kusoma china kimtindo kunahitaji kujizira ili uweze kufikia lengo kwani wazugaji ni wengi na wanakatisha tamaa saaaaaaaaaaaana.penye nia pana njia wakuu.
   
Loading...