Sayari ya mars na kupoteza joto lake

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Mars Ina angahewa (atmosphere) jepesi kwahiyo kama Ina angahewa jepesi maana yake hata atmospheric pressure yake ni ndogo Yani mgandamizo wa angahewa

Sasa kunapokuwa na mazingira kama hayo lazima kiwango Cha joto kipungue kwasababu Kwa mujibu wa fizikia Kuna sheria inaitwa pressure law inasema " at constant volume, the pressure is directly proportional to temperature"

Maana yake pressure ikiwa ndogo na joto linakuwa dogo pressure

Mafani mzuri utaona katika Venus, Venus Ina angahewa zito lenye mawingu mazito na hiyo imepelekea kuwe na joto Kali kuliko hata kwenye mercury

Lakini pia angahewa likiwa jepesi linashindwa kuthibiti vitu vinavyo escape kama gas, hivyo gas gas huondoka kutoka katika uso wa Dunia na kwenda maeneo ya juu
Hii sababu inaweza ikajibu swali la kwanini mars Haina maji wakati inaonesha uwepo wa michirizi ya maji hiyo inaonesha kuwa Kwa muda mrefu maji yake yamekuwa yakiondoka kama mvuke na kwenda angani ndio maana imekauka zimebakia barafu tu katika ncha ya kaskazini na kusini

Hivyo basi kuhitimisha hili tunaweza tukasema kuwa
1)hapo mwanzo mars ilikuwa gas mchanganyiko kibao hivyo angahewa yake atleast ilikuwa nzito nzito kiasi Cha kuweza kutunza maji na kuwa na joto Fulani stahiki

2)Kwa kuwa mars Ina gravity ndogo (4N/kg) uwezo wa gravity hii kushikiria mlundikano mkubwa wa gesi ni mdogo hivyo he's zikawa zinapeperukia angani mdogo mdogo ikiwemo na mivuke ya maji

3)baada ya miaka mingi mbele mars ikajikuta imepoteza maji na pia imepoteza kiwango kikubwa Cha gas kutoka katika uso wake

4)pia mars Kwa kuwa ilipoteza ges na kufanya angahewa lake Liwe jepesi mars ilianza kupoteza joto lake na hata kushindwa kutunza kiwango kikubwa Cha joto ambacho inapokea kutoka kwenye jua hivyo ikaanza kuwa na mazingira ya baridi

5)ndio maana hivi Sasa tunaiona sayari ya mars ikiwa Haina maji, ikiwa na anghewa jepesi Huku ikiwa na baridi Kali

Tukiachana na hayo pia uwezekano wa mars kuja kuwa habitable ni mdogo sana Kwa sababu

1)hata tukiyeyusha miamba ya barafu iliyoko kaskazini na kusini Kwa kutumia nuclear bombs Bado sio suluhu sababu maji hayo yatapotelea angani kutokana na angahewa la mars kuwa jepesi

2)mars Haina magnetic field ambazo husaidia kukinga sayari husika na adha za miale mbali mbali kutoka katika jua ambayo miale hiyo huweza kuwa na madhara Kwa wanadam

3)kutokana na angahewa kuwa jepesi Bado itatuhitaji tuwe/tujenge makazi maalumu ambapo tutaishi humo ndani bila kutoka nje sababu Kwa mgandamizo wa angahewa ya mars tukienda kama tulivyo hili joto la mwili wetu litatosha kabisa kutuchemsha na kama hiyo haitoshi Bado blood pressure yetu itaonekana kuwa kubwa na kushindwa ku balance na atmospheric pressure ya mars hivyo mishipa midogo midogo ya kwenye pua, masikio nk itapasuka pasuka na kutupelekea tuvuje damu na kupoteza maisha

Nini Cha kufanya?
Tuendelee kupambana kuirudisha Dunia kuwa na ubora kama ilivyokuwa zamani Kwa kuhakikisha tunatunza mazingira Kwa kupanda miti, kuepeuka hari za vita zinazoleta mchafuko wa hari ya hewa, kuachana na nishati chafu inayochafua mazingira mfano matumizi ya mafuta ghafi ges na makaa ya mawe
Tutafute vyanzo mbadala vya nishati rafiki ya kutuwezesha kuendesha viwanda ili tuepuke uchafuzi wa mazingira

Sababu mpaka Sasa hakuna tumaini la upatikanaji wa mazingira yatakayotuwezesha kuishi katika huu mfumo wetu nje na hii blue dot
Labda kama tutaenda kwenye sayari zingine zilizo katika nyota zingine tuangalie kama Kuna sayari yenye mazingira copy right kama ya duniani hapo sawa ila hiyo safari hatuiwezi sababu kutoka hapa tulipo mpaka kuikuta nyota jirani na sisi iitwayo proxima centauri itatuchukua safari ya miaka 4 na miezi miwili na wiki mbili na hapo ni endapo tutasafiri Kwa speed ya mwanga

Moudyswema
Tanzaniascienceyetu
AstronomyKiswahili

FB_IMG_1675940943940.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom