Watabiri wa hiari vs wa mchongo

Watabiri wa hiari vs wa mchongo

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,882
Reaction score
828,451
Kuna simulizi ya Bible kule Misri kuna fimbo ya muujiza ya Haruni ambapo alipoibwaga chini mbele ya Farao ikageuka nyoka..

Farao alipoona vile naye akawaita wachawi wake wote maarufu nao wakaja na fimbo zao wakazibwaga chini na kugeuka nyoka.. Ila nyoka aliyetokana na fimbo ya Haruni akawala nyoka wote wa fimbo za waganga wa Farao

Je tumejifunza nini hapo?

Mwaka 2011 mtabiri maarufu Tanyanyika ambaye sasa marehemu.. Hayati Sheikh Yahaya.. Alitabiri kitu kuhusiana na urais wa Tanganyika

Kwa hesabu za utabiri wake mwaka huu ndio unatajiwa kutimia...

Baada ya utabiri wake huo zilifuata tabiri nyingine zote zikienda sawa na utabiri mkuu wa sheikh Yahaya.. Tabiri nyingi zaidi zimetolewa mwaka huu mwanzoni

Mamlaka za kisiasa Tanganyika baada ya kuona moto wa tabiri zenye maono sawa unazidi kusambaa ... Zikaamua nazo kutafuta wataburi wake wa mchongo kukinzana na tabiri tangulizi

Watabiri hao wapya na tabiri zao mpya wakijijengea maneno ya kujihami kuwa wao si wanasiasa (as if waliulizwa) kwa mpangilio maalum na wakijifanya kuoteshwa ama kutumwa na mungu wakawa wanazikosoa tabiri tangulizi😂

Mmoja kwa kupitiwa ama kujisahau akaenda mbali zaidi kwa kusema anazifuta tabiri zote za awali katika ulimwengu wa roho😂😂😂😂.. Sijui ni nani alimwongopea kwamba tabiri zinaweza kufutwa kwa kukemewa!
Anyway.. Tabiri zinabaki kuwa tabiri mpaka pale muda wake unapotimia na kuthibitika kama ni NDIO ama ni LA
Hawa watabiri wa mchongo kinachowasumbua ni njaa na wamefanya kazi ya malipo.. Watulie sasa wakati utaamua!
 
downloadfile.png
 
Manabii wenyewe ni kina yule sheghe aliyetamka hadharani kwamba Magufuli ni zaidi ya mtume.
Sheghe aliyemkana mtume kisa vijipesa vya kuhonga mashoga
 
Back
Top Bottom