Wataalamu wabainisha madhara kutomaliza dozi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
1612189216713.png

Matumizi ya dawa yasiyozingatia muda uliopangwa yameelezwa kuingilia ufanisi wa kiambatahai kilichomo kwenye dawa husika ambacho husababisha athari mwilini.

Kiambatahai hicho huwekwa katika kila dawa inayotengenezwa ambacho ndicho hutibu ugonjwa ndani ya muda uliopangwa.

Wataalamu wa uchunguzi wa ufanisi wa dawa wa maabara ya Mamlaka ya Dawa na Vifaatiba (TMDA) jijini Mwanza wameeleza hayo hivi karibuni.

Kaimu mkuu wa maabara ya TMDA, Bugusu Nyamweru alisema dawa inapaswa kutumika kulingana na maelekezo kutoka kwa mtaalamu na si vinginevyo.

Alisema kuna hulka kwa wagonjwa wengi kupitiliza muda wa kutumia dawa au kutomaliza dozi na baadhi kuzibakiza kwa ajili ya matumizi ya baadaye kwamba yote ni makosa yanayosababisha zishindwe kufanya kazi.

“Kiambatahai kina muda wa kukaa ndani ya dawa na kuna ukomo wa matumizi, unapoisha wastani wa asilimia 10 ya kiambatahai hicho hupungua.

“Ile asilimia 90 inakuwa na uwezo wa kutibu lakini tunakuwa hatujui asilimia 10 iliyopungua imebadilika kuwa nini, labda imekuwa sumu hivyo kile kinachoharibika kinaweza kuleta madhara,” alisema.

Hata katika dawa za maji, alisema “ikishafunguliwa, haitakiwi kubaki kwa sababu inaweza kuleta madhara. Tunahimiza watu wazingatie matumizi ya dawa kwa usahihi kabla ya kwisha muda wake kuepusha athari zinazoweza kumpata mgonjwa ukiwamo usugu wa vimelea vya magonjwa,” alisema.

Mchunguzi wa dawa, Haruni Kapilya alisema wanazo mashine tofauti za kupima ikiwamo ‘distiller solution’ inayofanana na tumbo la binadamu.

“Ili dawa ifanye kazi ni lazima ichunguzwe kiambatahai kilichomo ndipo iingie sokoni kwani bila kufanya hivyo kuna uwezekano baadhi ya wafanyabiashara wakaingiza dawa ambazo hazina kiambata na kusababisha madhara kwa watumiaji,” alisema.

Mashine hiyo alisema ni muhimu katika kuchunguza dawa kwa kupima uzito na kiambata kilichomo kulinganisha na viwango vinavyotakiwa na kukubalika kimataifa.
 
Wengine hatumalizi dozi, tukiona tunaanza kupona imeisha hiyo

Na bado tunadunda
 
Back
Top Bottom