Wataalamu wa umeme msaada please

Raaj

JF-Expert Member
Feb 10, 2013
205
29
Habarini Ndugu wana jf, mimi nina solar watt 100 betri N70 dry cell ambazo nazitumia kwenye tv na kuwasha taa kama 5 tu tatizo linalofanya nijekuomba ushauri kwenu ni kwamba nyakati za usiku siifaidi kabisa hii tv maana umeme unawahi kuisha yaani kwa usiku maximum ni masaa 3 tu
Nb: natumia inverter kwa ajiri ya tv tu na kwenye kisambuzi natumia direct kutoka kwenye betri vivo hivo kwenye bulb
Naombeni ushauri wenu je hapo tatizo ni nini?
 
waje wakufafanulie nami nipate ujuzi,,,,, alafu ivi kwa kawaida ukishajaza fomu ya maombi ya UMEME huwa ile fomu unakaa nayo mpaka waje wakuwekee umeme kabisa ndo inarudishwa au namna gani?
 
Habarini Ndugu wana jf, mimi nina solar watt 100 betri N70 dry cell ambazo nazitumia kwenye tv na kuwasha taa kama 5 tu tatizo linalofanya nijekuomba ushauri kwenu ni kwamba nyakati za usiku siifaidi kabisa hii tv maana umeme unawahi kuisha yaani kwa usiku maximum ni masaa 3 tu
Nb: natumia inverter kwa ajiri ya tv tu na kwenye kisambuzi natumia direct kutoka kwenye betri vivo hivo kwenye bulb
Naombeni ushauri wenu je hapo tatizo ni nini?
Hiyo tv ni aina gani kwa maana ya ni flat au CRT aka chogo?
 
Kinachooneka ni kwamba wakati unafunga hiyo solar module na battery yako hiyo ya N100 hukufanya analysis kwamba unahitaji backup tym ya kiasi gani na ndio watu wengi mnapopoteaga hapo, kumbe jambo la msingi ni kujua total load yako na masaa unayotaka kutumia hiyo battery yako then ndio unaanza kuperform analysis kupata size ya solar panel na batteries zitakzo weza meet demand ya backup tym yako
 
Habarini Ndugu wana jf, mimi nina solar watt 100 betri N70 dry cell ambazo nazitumia kwenye tv na kuwasha taa kama 5 tu tatizo linalofanya nijekuomba ushauri kwenu ni kwamba nyakati za usiku siifaidi kabisa hii tv maana umeme unawahi kuisha yaani kwa usiku maximum ni masaa 3 tu
Nb: natumia inverter kwa ajiri ya tv tu na kwenye kisambuzi natumia direct kutoka kwenye betri vivo hivo kwenye bulb
Naombeni ushauri wenu je hapo tatizo ni nini?

nadhani mwenyewe ushapata jibu kwamba unapowasha TV usiku ndio battery inaisha mapema. inamaanisha kwakuwa usiku sola haifanyi kazi so battery inakuwa overloaded. ongeza battery ndugu hapo N70 ni ndogo kusustain hiyo TV na vitu vingine.
 
maana yangu ni kwamba mchana situmii tv naacha betri ichajiwe na solar then usiku ndo natumia but moto unawahi sana kuisha
 
Unapofikiria kutumia umeme wa nishati ya jua ni muhimu kuangalia mahitaji yako kwa ukamilifu. Ufahamu vifaa vyako vinakula umeme wa watts ngapi (jumla) kabla hujafunga solar panels na batteries zinazoendeana na mahitaji yako. Inaelekea mahitaji yako ni makubwa kuliko uwezo wa mtambo ulionao. Chunguza kila kifaa kwa kawaida nyuma au chini kuna maandishi yanayoonyesha wattage inayotumika, halafu rekebisha kwa kuongeza batteries na pengine hata solar panels.
 
Alafu aliyeuliza kuhusu fomu ya tanesco ikishajazwa unaipeleka tanesco wanakupangia siku ya kuja surveyor lakini fomu unabaki nayo ila surveyor akishakuja tu kwako anaondoka na iyo fomu
 
Kuna beteri zingine sio nzuri unaweza ukaitumia ndani ya mwaka ikapoteza uwezo.
Kwa sola yako ungenunua beteri ya N120. Beteri zinazodumu ni Rb au Incoi na zinabei ya juu tofauti na nyingine.
 
Habarini Ndugu wana jf, mimi nina solar watt 100 betri N70 dry cell ambazo nazitumia kwenye tv na kuwasha taa kama 5 tu tatizo linalofanya nijekuomba ushauri kwenu ni kwamba nyakati za usiku siifaidi kabisa hii tv maana umeme unawahi kuisha yaani kwa usiku maximum ni masaa 3 tu
Nb: natumia inverter kwa ajiri ya tv tu na kwenye kisambuzi natumia direct kutoka kwenye betri vivo hivo kwenye bulb
Naombeni ushauri wenu je hapo tatizo ni nini?
Kwakifupi unatumia umeme wa betri kazi ya solar panel nikuli charge betri tv yako inatunia umeme mwingi
 
Utangulizi
Tatizo linaweza kuwa kati ya mambo yafuatayo;
1. Battery Haijai
2. Matumizi ni makubwa

Ufafanuzi
1. Battery haijai kwa nini?
Solar panel ya 100W haina uwezo wa kujaza battery ya N70 kama itatumia kutoka 100%-0%. Panel ya 100W itakuwa na uwezo kujaza battery ya N70 kama battery itatumika kwa angalau 50%. Kitaalamu kuna factor inaitwa DoD ambayo inapendekezwa isiwe chini ya 50% kwa battery za lead-acid ili kurefusha maisha ya battery yako.

2. Matumizi ni makubwa
Kama kigezo cha kutumia battery husika kwa 50% kitazingatiwa basi kuna uwezekano wa battery kujazwa na panel hiyo ya 100W. Ikiwa hivi basi, kinachoweza kusababisha battery itumike kwa masaa 3 pekee ni ukubwa wa matumizi ambao huu unategemeana na vifaa vinavyotumika.

Ushauri
Nitafute whatsapp kwa namba 0626409973 nikuvushe hapo
 
Back
Top Bottom