Wataalamu wa ulinzi naombeni ushauri

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
26,580
48,729
Hapa napoishi tumeingia mkataba na kampuni moja ya kibongo kuhusu suala la ulinzi usiku. Hawa walinzi wanatakiwa kuingia saa kumi na mbili ila wao wanaingia saa yoyote hata saa mbili. Mfano leo hata hajaja na kama hawaji hata hawatoi taarifa hadi upige kwa mwenye kampuni nae anaanza kushangaa afanye mbinu alete mwingine blah blah kibao yaani.

Inaelekea mwenye kampuni hawalipi vizuri kwaiyo wanaacha kazi inabidi abadilishe mara kwa mara.

Hofu yetu ni kwamba kwa wiki eti wanaweza kuja hata watu wanne tofauti tofauti. Sasa sisi hatupendi watu tofauti tofauti waje hapa kwetu maana tunaona kama ni hatari kwetu. Mwenye nyumba ambae ni boss wangu kazini yeye hata hajui hii issue yeye kanikabidhi hapa kila kitu yeye hakai bongo hata kuwalipa nalipa mimi na mkataba nimesaini mimi.

Nimevumilia kumsemea huyu bwana apigwe chini tutafute wengine ila sasa nimechoka naona tu niwe mkweli.

Eti wadau ni sawa walinzi kubadilishwa kila siku jamani?

Walinzi wazuri wanatakiwa waweje ili nikiingia mkataba mpya nitoe hayo masharti maana nimewachoka hawa wananiletea lawama.
 
Mkitaka hivyo tafuteni ambaye hayupo ndani ya kampuni.

Huyu mtamlipa wenyewe kwa jinsi mtavyoelewana.
 
Makampuni yote ya Ulinzi hakuna mlinzi anayelinda eneo moja kwa muda mrefu.

Mkitaka hivyo tafuteni ambaye hayupo ndani ya kampuni.

Huyu mtamlipa wenyewe kwa jinsi mtavyoelewana.
yaani lindo moja wanabadilisha mtu kila siku mkuu? halafu kumbuka sio kwamba wanawafanyia rotation inasemekana wengi wanaacha kazi
 
Kubadilisha mlinzi kwenye lindo ni utaratibu wa kampuni husika ishu ulio isema wengi wanaacha kazi hapo ndo penye utata hapo cha kufanya mwite mwenye kampuni mzungumze nae ili kuvunja mkataba na ndo utafute kampuni nyingine
 
yaani lindo moja wanabadilisha mtu kila siku mkuu? halafu kumbuka sio kwamba wanawafanyia rotation inasemekana wengi wanaacha kazi
Sasa kumbe tatizo umeshalijua kwamba hawapei chao ndo maana wanafanya wanavyotaka piga chini kampuni tafuta ingine.
 
tutawaondoa ila ndo naomba ushauri hao wapya tuwaambie waweje mkuu i mean walizi wazuri wanatakiwa waweje?
Kampuni ya kueleweka na walinzi wake wanajielewa hata wana supervisor ambae anawatembelea lindoni kukagua. Kama hela si tatizo wachukue G4S,Ultimate security,SGA,KK hawana ubabaishaji.

Kuna kampuni nyingine walinzi wao ni wezi balaa, nishalizwa sema kampuni yao walinilipa kuwa makini.
 
asante mkuu
hawa jamaa hata hawakagui inafika saa nne mlinzi humuoni ukipiga simu anakuuliza kwanini hajaja? sasa mimi nitajuaje wabongo ovyo kweli aisee .
 
Jaribu kutafuta kampuni la kigeni me ofsn kwangu nimeweka G4S Securing Solution. Kampun zuli sana. Kama uponahitaji Sema nikuconnect nao.. Kwanza askar wake wasafi kwel.. Na wakalim. Wanakaguliwa kila baada ya masaa mawili inapita patroling yao
 
tutawaondoa ila ndo naomba ushauri hao wapya tuwaambie waweje mkuu i mean walizi wazuri wanatakiwa waweje?
Mimi sio mtaalam wa ulinzi lakini nimewai kuitumia kampuni ya ulinzi muda wa kuingia kazini ni huo huo kumi na mbili sasa kumjua mlinzi mzuri hilo ni jukumu la kampuni lakini wewe kama mteja na hujarizika na utendaji wa mlinzi una haki ya kulalamika kwa kampuni husika ili hatua stahiki zichukuliwe.
 
Jaribu kutafuta kampuni la kigeni me ofsn kwangu nimeweka G4S Securing Solution. Kampun zuli sana. Kama uponahitaji Sema nikuconnect nao.. Kwanza askar wake wasafi kwel.. Na wakalim. Wanakaguliwa kila baada ya masaa mawili inapita patroling yao
asante sana ni sh ngapi kwa mwezi mkuu?
 
Mimi sio mtaalam wa ulinzi lakini nimewai kuitumia kampuni ya ulinzi muda wa kuingia kazini ni huo huo kumi na mbili sasa kumjua mlinzi mzuri hilo ni jukumu la kampuni lakini wewe kama mteja na hujarizika na utendaji wa mlinzi una haki ya kulalamika kwa kampuni husika ili hatua stahiki zichukuliwe.
hawa wabongo hatuwataki tena mkuu wababaishaji sana
 
Back
Top Bottom