Wataalamu wa Ujenzi Mnasemaje kuhusu aina hii ya Matofali.??

Kipeperushi

Senior Member
Aug 17, 2011
168
31
Hivi karibuni nilibahatika kutembelea wilaya tatu zilizopo katika mkoa wa Mtwara na miongoni mwa mambo mapya kwangu niliyojifunza, hususani katika masuala ya ujenzi, ni matumizi ya matofali yaliyotengenezwa kutokana na mchanganyiko wa cement na udongo wa kichuguu (mfinyanzi). Kinachoangaliwa hapo ni uwezekano wa kupata matofali mengi zaidi kwa mfuko mmoja wa cement pale unapotumia mfinyanzi ikilinganishwa na unapotumia mchanga wa kawaida. Ninachoomba kujuzwa toka kwenu ni usahihi wa mtazamo huu wa uchanganyaji cement na mfinyanzi. Je, unakubalika kisayansi? Na kama inakubalika ratio sahihi ni ipi kwa mfuko mmoja? Natanguliza shukrani zangu kwa mchango wowote wa mawazo toka kwenu.
 

Kipeperushi

Senior Member
Aug 17, 2011
168
31
Lugha ya picha hiyo unaongelea style za mapenzi kwa lugha ya matofali,lmao[/Uko mbali mkuu, naongelea matofali kwa ajili ya ujenzi wa nyuma. Lugha hiyo inayohusisha matofali na mapenzi inatumiwa na kabila gani tena mzee..?]
 

Nzagamba Yapi

Senior Member
Sep 1, 2011
167
70
Shaka we ni mjukuu niombe radhi,huyu kipeperushi haaminiki anyway una ujenzi au? huku hong kong kuna machine za matofali nzuri sana achana na hiyo style ya matofali unayotaka iko outdated kama unataka tuwacliane nikutumie ni ya umeme tofali elfu kwa cku
 

Kipeperushi

Senior Member
Aug 17, 2011
168
31
Shaka we ni mjukuu niombe radhi,huyu kipeperushi haaminiki anyway una ujenzi au? huku hong kong kuna machine za matofali nzuri sana achana na hiyo style ya matofali unayotaka iko outdated kama unataka tuwacliane nikutumie ni ya umeme tofali elfu kwa cku[/Nipe gharama mkuu. nitakuagiza maana haya ya mfinyanzi naona sio issue]
 

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,230
7,153
Shaka we ni mjukuu niombe radhi,huyu kipeperushi haaminiki anyway una ujenzi au? huku hong kong kuna machine za matofali nzuri sana achana na hiyo style ya matofali unayotaka iko outdated kama unataka tuwacliane nikutumie ni ya umeme tofali elfu kwa cku
Si uweke mambo hadharani kaka ili tujue.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom