Wataalamu wa ndoto mnisaidie hili

Thailand

JF-Expert Member
Nov 15, 2019
262
778
Habarini za muda huu ndugu!
Nipende ku declare interest kwanza; kwamba mimi sio mwamini wa Ndoto kabisa za usiku.
Imekuwa mara kwa mara naota naimba yaani Mimi ni Mwimbaji wa levo za juu kabisa. Nimekuwa nikipuuzia sana hii ndoto kwa sababu mimi najionaga sina kipaji cha kuimba Muziki halafu siwezi harakati za mziki kwa sababu kwa sasa nina miaka 30 hivyo naona nishapitwa na muda wa ku hustle kwa ajili ya mziki.

Cha kushangaza jana usiku pia nimeota naimba, wimbo hakika ulikuwa mzuri sana. Ajabu aliyekuwa ananifundisha kuimba wimbo huo ni kiongozi aliyejitambulisha kwamba ni Yesu. Wimbo nilikuwa naimba ulikuwa wa kumsifu Mungu: hakika wimbo huu nilikuwa nikiuimba kwa ufanisi mkubwa. Lakini kiongozi (Yesu) huyu aliniambia kuna kijana kutoka Morogoro na mwingine ambaye jumla tutakuwa watatu tukiimba kwa viwango vya juu sana.
Ajabu wimbo ambao nimeuimba kwa ufanisi usiku, nikiamka asubuhi si ukumbuki hata kidogo.
Wadau nisaidieni tafsiri ya hii ndoto.
 
Mara kadhaa miaka ya nyuma nilikuwa nikiota ndoto za aina hiyo,
mpaka mara kadhaa nilikuwa nikiamka naweza kuyakumbuka yale mashairi kwa kiasi fulani.
Nilipochunguza vizuri ni maisha / mazingira niliyokuwa naishi.
Kwa kawaida ndoto unazoota zinatokana na historia / zilizo au zinazohifadhiwa kwenye ubongo.
 
Unaacha kuota ndoto kama za Lema, zenye mashiko unabaki kuota mandotondoto tu.
 
Habarini za muda huu ndugu!
Nipende ku declare interest kwanza; kwamba mimi sio mwamini wa Ndoto kabisa za usiku.
Imekuwa mara kwa mara naota naimba yaani Mimi ni Mwimbaji wa levo za juu kabisa. Nimekuwa nikipuuzia sana hii ndoto kwa sababu mimi najionaga sina kipaji cha kuimba Muziki halafu siwezi harakati za mziki kwa sababu kwa sasa nina miaka 30 hivyo naona nishapitwa na muda wa ku hustle kwa ajili ya mziki.

Cha kushangaza jana usiku pia nimeota naimba, wimbo hakika ulikuwa mzuri sana. Ajabu aliyekuwa ananifundisha kuimba wimbo huo ni kiongozi aliyejitambulisha kwamba ni Yesu. Wimbo nilikuwa naimba ulikuwa wa kumsifu Mungu: hakika wimbo huu nilikuwa nikiuimba kwa ufanisi mkubwa. Lakini kiongozi (Yesu) huyu aliniambia kuna kijana kutoka Morogoro na mwingine ambaye jumla tutakuwa watatu tukiimba kwa viwango vya juu sana.
Ajabu wimbo ambao nimeuimba kwa ufanisi usiku, nikiamka asubuhi si ukumbuki hata kidogo.
Wadau nisaidieni tafsiri ya hii ndoto.
Sa ushasema huwa huamini ndoto za usiku
 
Ndoto ni kupumzika tu kwa akili. Wewe ni muimbaji kama unavyosema kwa hiyo kuota unaimba si jambo la ajabu.

Mara nyingi tunaota yale tunayoyawaza mara kwa mara.
 
Mimi naona umeshika Sana dini, na Roho mtakatifu yupo Dani yako akiimba ndani yako, mshukuru Mungu
 
Soon utafanya colabo na P diddy, kikubwa uje tukupige chale za matakoni ili ndoto itimie
 
Ok. Mimi mwenyewe huwa inanitokeaga mara nyingi. Tofauti tu mimi huwa sifundishwi na mtu,ila naimba wimbo wangu mzuri tu. Wimbo huwa unajirudia rudia kwenye ndoto ingine. Mimi pia napuuzia hiyo ksbb ya umri pia. Lakini mimi nina uwezo kile ninachoota,nikiamka muda huo huo nikikusudia kukiweka kwenye kumbukumbuku naweza

Hivyo basi nakushauri kwa umri wako unaweza kuimba,fanya hivi sasa,fanyia mazoezi uamke ukiwa usingizini unaota,jitahidi kaa na simu karibu. Ukianza kuimba ndotoni amka,ukiamka ule wimbo uliokuwa unaimba na melod havipotei muda huo huo. Imba vile vile ukijirecord kwenye simu. Usijali hata kama unaimba bila mpangilio au hata kama unaimba vibaya. Muhimu hapo uipate melody tu. Mpangilio wa nyimbo utaupata baadae ukianza kuwa serious. Ukimaliza kujirecod zima simu,lala. Ukiota tena fanya hivyo. Siku ya siku fuatilia hizo melody uone kama zinakuja sawa.

Nina uhakika ukiweza hilo zoezi utafikia patamu.

Mimi nimejipa mazoezi ya kuweza kuamka nikiwa katikati ya kuota kama ndoto ni mbaya. Najitahidi sana nijisukume niamke
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom