Wataalamu wa lugha thibitisha hili

Mpigamsuli

JF-Expert Member
May 24, 2012
3,885
575
wana jf naomb maon yenu juu ya hili hivii wewe binafsi lugha gan unadhan mtu akifundishiwa ataelewa je n kiswahiliaueng
 
Ni lugha ambayo mtu anaifahamu vizuri. Lugha anayotumia kufikiri, lugha ambayo imejengeka pamoja na viwakilishi vyake toka utotoni mwake. (Viwakilishi ni ile picha inayokujia mara tu usikiapo neno. Mfano unaposikia neno mama mara moja picha ya mama yako mzazi inakujia na unaposikia neno shule mara moja inakujia picha ya shule uliyosoma n.k.). Tatizo hapo Tanzania tunatumia lugha tofauti kufikiri na ile tunayoongea. Na kiswanglish ni dalili kuwa hatufahamu kiswahili wala kiingereza. Kunahitajika juhudi za dhati katika kushughulikia hili likiwa ni moja ya vipengele mhimu katika mstakabali wa elimu yetu nchini.
 
Kiswahili ni lugha rahisi sana kujifunza kuliko kiingereza,kwa sababu kwanza kiswahili hakija jitosheleza kimsamiati kwa hiyo ni rahisi mtu kuielewa misamiati michache iliyopo,sababu nyingine ni maneno mengi ya kiswahili hutamkwa kama yanavyoandikwa isipokua machache sana kama mbu/mmbu/,mbwa/mmbwa/ .Ila maneno mengi ya kiingereza hutamkwa tofauti kabisa na yanavyo andikwa mf:Education/edjukeisn/, cup/kap/, cap/kep/, you/ju:/, nk hvyo humuwia vigumu mtu kujifunza haraka na kuielewa ukilinganisha na kiswahili.
 
Kiswahili ni rahisi kujifunza tofauti na kiingereza kwa mtu gani?? Kwa mtu ambaye lugha yake ya kwanza ni ipi? Je ni kwa wote au kwa watu flani tu. NAOMBA MWONGOZO then nitaendelea.AHSANTE
 
Back
Top Bottom