Wataalamu wa Kuchoma mbuzi, Mnatumia njia gani kuifanya nyama kuwa Laini na Aina ya Viungo?

Dringia

Member
Sep 17, 2016
72
61
Wakuu habarini za Mida,

Nahitaji msaada kwa wale wataalamu wa kuchoma nyama ya mbuzi huwa inakua lain na yenye ladha. Naombeni tupeane maujuzi jinsi ya kuchoma na aina ya viungo vya kutumia.

Nilijaribu kuchoma majuzi ikawa ngumu kama nini
 
Unaweza kuichoma na mafuta tu bila viungo na ikawa tamu na laini moto usiwe mkali weka moto mdogo iive taratibu nyama ya mbuz ni laini
 
Iweke viungo unavyohitaji
Bila kusahau tangawizi
Kisha nyunyizia mafuta ya kula kidogo tu hakikisha yote imeingia
Kisha ifunike kwa muda wa dk 15 viungo vikolee

Baada ya hapo iweke jikoni
Hakikisha nyama unaifunika ili ipate mvuke
Unaweza tumia foil au hata sufuria tu unaifunika kwa juu
Jitahidi kuigeuza marakwa mara
 
Wakuu habarini za Mida,

Nahitaji msaada kwa wale wataalamu wa kuchoma nyama ya mbuzi huwa inakua lain na yenye ladha. Naombeni tupeane maujuzi jinsi ya kuchoma na aina ya viungo vya kutumia.

Nilijaribu kuchoma majuzi ikawa ngumu kama nini
Unatumia jiko la aina gani kuchomea? Maana ishu inaanzia hapo
 
Back
Top Bottom