Wataalamu wa biogas mje huku

Wataalamu wa biogas mje huku

laii

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2016
Posts
853
Reaction score
1,120
Hii nishati ya biogas niliisikiaga kitambo sana na kwa mara ya kwanza niliiona kwa masista na mabrother wa Kikatholic kule Kilacha, ya kwao inatokana na mavi ya n'gombe,japo nasikia mavi ya wanyama wengine kwa mfano nguruwe hutumika pia.
Swali nikitaka project hii ya biogas lazima niwe na mifugo nyumbani kwangu,au naweza kununua mbolea ya wanyama na kuijaza kwenye yale mashimo yanayotengenezwa kwa ajili ya kutoa gas hii na nikapata gas bila matatizo.
Vipi mavi ya binadamu hayafaii???
Nakaribisha maoni, ushauri wa kitaalamu
 
Habari picha
images-1.jpeg
images.jpeg
Schematic-diagram-of-the-simple-unheated-biogas-digester-The-diluted-manure-water_Q640.jpeg
 
Mbolea fresh inafaa zaidi kuliko iliyokauka au iliyokaa muda mrefu lakini sio lazima.
Kwa hiyo kwa wale wanaotumia mifugo yao wenyewe wanakuwa na advantage ya kupata mbolea ambayo iko fresh, tofauti na wale ambao wananunua maana inakuwa imekaa kwa muda na baadhi ya gesi zinakuwa "zimeyeyukia hewani".

Kinyesi cha mwanadamu ni kizuri sana, tatizo linakuja kwenye sheria za nchi maana kitaalamu kinyesi cha mwanadamu kinabeba maradhi mengi sana yanayomuathiri mwanadamu.

Sidhani kama watu wa afya na mazingira wanaweza kukuruhusu kukitumia, maana unaweza kusababisha milipuko mizito sana ya magonjwa kwa watu na ikawa tatizo kwa wengine, labda kama una mitambo ya kuhakikisha kuwa unaua vimelea vyote vya magonjwa kabla ya kuitumia.

All in all sio lazima kutumia kinyesi tu ili kuzalisha umeme kwa njia hio, kwa teknolojia ya sasa unaweza kutumia pia matakataa ya jikoni au kifupi anything organic ambacho kinaweza kuoza haraka.

Fuatilia humu JF kuna nyuzi zinazungumzia sana hili.
 
Mie nilikuwa nataka kujua kutengeneza huo mtambo kwa kutumia pipa la plastic mfano hilo hapo juu, unaweza pata gas ya kutosha?
 
Tatizo la watalamu wa Tanzania wana bei ghali Sana!! Wakenya wanakutengenezea Kwa bei rahisi tu.
 
Mie nilikuwa nataka kujua kutengeneza huo mtambo kwa kutumia pipa la plastic mfano hilo hapo juu, unaweza pata gas ya kutosha?
Kutosha kwa gesi kunaendana na matumizi yako binafsi hakuna anayeweza kukuhakikishia. Kama unaishi karibu na machinjio au mfugaji utaishi kwa raha, pipa imara la plastiki linafaa na ukubwa ulingane na matumizi yako.
 
Nina Ng'ombe 5 na familia ya watu 8, kama kawaida kunapikwa mara 3 kwa siku. unafikiri pipa la lita 300 linatosha? nimeangalia kwny youtube nimeona pia wengine wanaweka maji kwenye pipa la pili kisha gas inayozalishwa kutoka pila la kwanza inaingizwa humo kwenye pipa la 2, nini faida yake kiufundi?
 
Nikipata elimu nzuri kuhusu biogas ndugu zangu,ntafuga hata n'gombe mmoja wa maziwa nipate maziwa na hii biogas.Naamini ntapata faida sana.

NAFUATILIA KWA MAKINI, majibu ya wadau
 
Mbolea fresh inafaa zaidi kuliko iliyokauka au iliyokaa muda mrefu lakini sio lazima.
Kwa hiyo kwa wale wanaotumia mifugo yao wenyewe wanakuwa na advantage ya kupata mbolea ambayo iko fresh, tofauti na wale ambao wananunua maana inakuwa imekaa kwa muda na baadhi ya gesi zinakuwa "zimeyeyukia hewani".

Kinyesi cha mwanadamu ni kizuri sana, tatizo linakuja kwenye sheria za nchi maana kitaalamu kinyesi cha mwanadamu kinabeba maradhi mengi sana yanayomuathiri mwanadamu.

Sidhani kama watu wa afya na mazingira wanaweza kukuruhusu kukitumia, maana unaweza kusababisha milipuko mizito sana ya magonjwa kwa watu na ikawa tatizo kwa wengine, labda kama una mitambo ya kuhakikisha kuwa unaua vimelea vyote vya magonjwa kabla ya kuitumia.

All in all sio lazima kutumia kinyesi tu ili kuzalisha umeme kwa njia hio, kwa teknolojia ya sasa unaweza kutumia pia matakataa ya jikoni au kifupi anything organic ambacho kinaweza kuoza haraka.

Fuatilia humu JF kuna nyuzi zinazungumzia sana hili.
Bro uko sahihi sana,kasoro hapo kwenye kinyesi cha mtu:Jibu ni kuwa kinyesi cha mtu kinapitia action ya enzymes nyingi sana kuanzia mdomon hadi kwenye colon hivyo kina assimilation i.e uptaken ya nutrients kuinhia kwenye damu ni kubwa au iko effective sana kiasi kwamba kinyesi kinakua hakina kabisa nutrients,zaidi ya residuals
Na kumbuka biogas inategemea sana nutrients zifanyiwe anaerobic process ndo gas itoke,so kwa wanyama vyakula vyao vinapitia enzymes wachache sana ndo maana ng'ombe akinya hapo yakua kama bado majani kidogo si kama binadmu,so ukichukua kinyesi cha ng'ombe ukakiweka kwenye bioreactor kinatoa gas nyingi kwa sababu ya hizo nutrients.
Nilisha run hii project mkui,kwa binadamu gas kidogo sana kama kilo 4 kwa mwezi mzima kwa watu 8 wanaokunya.
Unaweza kunisahihisha
 
Back
Top Bottom