WATAALAM WA PRINTER TAFADHALIi

Mshumaaa

Senior Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
156
Reaction score
17
Nna Printer Kyocera Fs 1920. Tangu nibadilishe wino matatizo ndipo yalipoanzia yaani imegoma kabisa na mimi naipenda sana kwa sababu enzi zake ilikuwa inapiga kazi si mchezo. Kwa sasa nimekwama kabisa nahitaji msaada wenu wadau. Natanguliza shukrani za dhati wakuu.
 
Inagoma kivipi? haiwaki au haifanyi kazi? unayo CD ya driver yake? jaribu ku repair kwa kutumia CD Driver yake hiyo Printer Kyocera Fs 1920
 
Inagoma kivipi? haiwaki au haifanyi kazi? unayo CD ya driver yake? jaribu ku repair kwa kutumia CD Driver yake hiyo Printer Kyocera Fs 1920

Kuwaka inawaka vizuri tu. Na cd driver yake nshapoteza nimejaribu kui-google nimechemka. Nilifikiri tatizo ni Pc nikaiformat ndo nikaharibu kila kitu kwa hiyo sasa ninakaa nayo kama pambo tu. Nitashukuru sana kaka kama utanisaidia maana ilikuwa inapiga kazi sana. Mi nahisi wino nilioweka labda feki.
 
Kikubwa hapo ni drivers mkuu. Kama ulishapoteza drivers, jaribu kuingia kwenye website ya Hiyo company ya printer yako. Then uidownload halafu ufanye installation.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…