Wataalam wa mambo yetu yale inakuaje.... hapa?

Wataalam wa mambo yetu yale inakuaje.... hapa?

charger

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2010
Posts
2,320
Reaction score
1,374
Habari za asubuhi/mchana/jioni wana jamvi.Ninaamini mpaka unapata fursa kupitia uzi basi u mzima.

Nisikuchoshe na story nyingi kama waomba kura.Kilichonileta hapoa leo ni tabia ya ajabu iliyoanza kuoneshwa na vyombo vyetu vya usafiri.Kwa mfano Scania si kawaida kukuta ina vuta tela zaidi ya moja ila siku hizi utakuta scania ina matela matatu hadi matano na wakati gari hilo si treni na jamii ina kiangalia kitendo hiki na kuona kama ni kawaida,au gari zinabadili mwelekeo na kwenda kinyumenyume (Reverse) na abiria wanaonekana kufurahia tu huu utaratibu mpya.

Unakuta gari aina ya Vits au starlet eti nazenyewe zinavuta matela ya tani hata 15 kwa umbali mrefu na watu hawashangai.Gari zina pita tu one way na hakuna anaye jali.Hata kiwango cha nauli nacho kimeshuka sana, sasa sijui ni kwa ajili ya ongezeko la bodaboda au la?

Hata huu utaratibu wa kutumia magurudumu ya tubeless,inaonekana watu wengi wanapenda "tubeless" bila kujua usalama wake.

Je mambo haya ni sawa yakachwa yaendelee au ni dalili ya maendeleo?

KWA YEYOTE ATAKAYE HUSIKA.

WENU MTIIFU CHARGER

Aisee umetumia tafsida ya hali ya juu,nakushauri uweke na maana ya scania,reverse,tubeless,bodaboda n.k
 
Aisee umetumia tafsida ya hali ya juu,nakushauri uweke na maana ya scania,reverse,tubeless,bodaboda n.k

Mkuu Nigga unataka na watoto wa fb wastuke?
 
Mkuu hizi ni zama za uwazi na ukweli,mbona umetumia njia ndefu?
 
Hebu weka picha tuone hayo Matela matano na hiyo Vitz inayovuta tela ndo tutoe maoni yetu
 
Hahahahaaaaaaa nimeipenda sana sana hasa hio ya Vitz vs Scania....siku hizi Mpwa hata Bajaj Nazo zinataka zikikua ziwe kama Scania.....
 
Hahahahaaaaaaa nimeipenda sana sana hasa hio ya Vitz vs Scania....siku hizi Mpwa hata Bajaj Nazo zinataka zikikua ziwe kama Scania.....

Mpwa elli mi sijui huu ujasiri unatoka wapi
 
Kama hatueelewi maneno,ebu tia picha tuone
unaongea mafumbo ya nini?funguka mkuu
 
yaani sasa badala ya kujadili mada umefanya tujadili tafsida......

"Vits au starlet eti nazenyewe zinavuta matela ya tani hata 15"
ila haya matela ya tani 15 kwanini yanapenda vistarlet wakati kuna
scania,volvo
 
mmm yani sijaelewa kabsaaaaaaaaaa.naona hiyo picha ingenisaidia sana...
 
yaani sasa badala ya kujadili mada umefanya tujadili tafsida......

"Vits au starlet eti nazenyewe zinavuta matela ya tani hata 15"
ila haya matela ya tani 15 kwanini yanapenda vistarlet wakati kuna
scania,volvo
inaonekana haya mascania yanavutwa na vitz kwenye mtteremko mkali!!!
 
Back
Top Bottom