Wataalam nishaurini kuhusu solar

emboaba

Senior Member
Oct 5, 2014
143
117
Habari wanajamvi

Nataka ninunue solar kwa matumizi ya kawaida, taa nne, tv na subwoofer ndogo kwa ajili ya magetoni. Sasa naomba ushauri, hivi solar ya 40 watts itatosha!? Na je battery nichukue la ukubwa gan!?

Natanguliza shukrani
 
Nitafute nikuuzie ya watts 100 bei sawa na bure pia ni aina ya polycrystaline ya ujerumani 0715277821 ukitaka na kufanya load analysis nitakusaidia
 
solar ya 40 watts haitoshi.Taja kila kifaa umepanga kiwe "ON" kwa masaa mangap kwa siku halafu nitakutumia specifications za vifaa vyako bureee
 
Kwa matumizi ya kawaida tu nyumbani, fan, taa , tv utahitaji
Panel ya 80/85W
Charger controller 10A
Battery ya 100Ah
Inverter ya 600W.
Friji na pasi havijajumlishwa hapo!!
 
Kwa matumizi ya kawaida tu nyumbani, fan, taa , tv utahitaji
Panel ya 80/85W
Charger controller 10A
Battery ya 100Ah
Inverter ya 600W.
Friji na pasi havijajumlishwa hapo!!
Umepataje hizo results bila kujua total load itakayoendeshwa na battery yako??pia umejuaje panel ya watts 80/85 inaweza charge battery ya 100Ah?? Pia umefikiaje kupata inverter ya 600 watts bila kujua total load?? Maana formula inasema inverter should be greater than the total load by 25-30% na pia umejuaje panel ya watts 80 inaweza toa charging current ya kuweza kucharge battery ya 100Ah wakati formula inasema charging current should be 10% of the battery Ah, sasa ukicheki kwa battery lako la 100Ah the 10% ni 10Amps sasa hiyo panel ya 80/85 watts inauwezo wa kitoa charging current ya 10Amps?? Alsoin order to calculate the panel generation factors (PGF) the following should be considered
1)15% for the temperature above 25°C
2)5% for the losses due to sunlight reflection
3)10% for the losses caused by fixed position of the solar system
4)5% for losses caused by dirt
5)10% allowance for the solar pv module ageing
 
Mi nahitaji solar kwa matumizi ya vifaa na muda ufuatao

TAA
Taa tano ambazo zitawashwa kuanzia saa 1 jioni hadi saa5 usiku, kisha taa mbili zitawaka hadi asubuhi saa12

TV NA RADIO
Tv itawaka wastani wa masaa 10 mchana na masaa kama manne wakati wa usiku, sawa na redio subwoofer

SIMU
Simu itakua inachaji wakati wowote, mchana na usiku

Naomba ushauri wenu wataalamu
 
solar ya 40 watts haitoshi.Taja kila kifaa umepanga kiwe "ON" kwa masaa mangap kwa siku halafu nitakutumia specifications za vifaa vyako bureee


ktk taa nne moja haizmw kuanzia sa 1jion had asubuh..tatu zlzobak ztazmwa sa nne

bufa na tv inategemea uwepo wangu mageton...wastan masaa sita had saba kuanzia kwa siku
 
Nunua solar watt 120 na betri ya N100. Na utumie vifaa vya DC, hapo utawin, ila TV isizidi watt 35 na woofer isizidi watts 25.
 
taa ziwe on ucku kucha, tv na bufa zwe on masaa15 mkuu
utahitaji 1. at least 2 modules za 300watts,12Vdc 2.inverter size chukua 150w or greater 3.battery iwe 12v,300Ah for 1 day kama unataka within 3days uwe unapata umeme bila kuchaji may be mvua zinanyesha nunua 12v,900Ah waweza nunua betri tatu za 300Ah halafu unaziunga parallel
NOTE:kutokana na Power consumption demand yako hakikisha taa zinakuwa 4 kila moja isizid 5W
s,woofer isizid 75 w na tv isizid 30W
 
ktk taa nne moja haizmw kuanzia sa 1jion had asubuh..tatu zlzobak ztazmwa sa nne

bufa na tv inategemea uwepo wangu mageton...wastan masaa sita had saba kuanzia kwa siku
mkuu budget yako ikoje hasa?pv panel na battery ndo bei kubwa zaidi.kama pesa ipo nunua pv panel ya 300w,battery 150Ah waweza ziongeza batterry had 450Ah,inverter 200 or greater,
note:nunua vifaa vilivyo na power rating ndogo
 
Nina sola panel watt 40 betri N33 je naweza ongeza panel watt 40 betri N33 niunganishe kwa pamoja??

natanguliza shukurani
 
Back
Top Bottom