Wataalam naomba msaada wenu ktk haya nataka kujiajiri.(kuwamjasiliamali) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wataalam naomba msaada wenu ktk haya nataka kujiajiri.(kuwamjasiliamali)

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by LEGE, Oct 29, 2011.

 1. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2011
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  Natanguliza shukran zangu.Mim nikijana wa miaka 24 nimechoka na maisha ya kufanya kazi za kuunga unga na huku nyumban nimeacha ekari kibao za ardhi zikiota nyasi bila kutumiwa.Namambo mengi sana ninayotaka kwenda kuyafanya bush 1 kufuga wanyama mbalimbali hasa nataka kuanza na wanyama ambao kwa kipindi kifupi niwe nishawauza iliniweze kufanikisha upanuaji wamalengo yangu. Mifugo ninayo tarajia kuanza nayo ni kuku hasa kienyeji,nguruwe.Vile vile nampango wakuchoma mkaa na tofari na kuziuza kwan eneo lipo la kutosha maji yapo kuna mto kuni zipo za kumwaga nazan hivi 2ndiyo vitakavyo kuwa chachu kubwa ya mtaji wangu huo.
  Vile vile nampango wakutengeneza mabwawa ya kuhifadhi maji sehem ntakamo kuwa nachimba udongo watofari na malengo yangu ya mabwawa hayo ni kuhifadhi maji ya kumwagilia na ikiwezekana ntafuga samaki.
  Vile vile na mpango wa kulima mazao ambayo yatakuwa ni vyakula vya mifugo yangu kama alizeti,maboga na mahindi n.k
  ninamengi sana ninayo yawaza yakuyafanya shida yangu kubwa ni wapi ntapata elim ya awali japo nianzapo shughuli hizi niziendeshe kisomi kidogo na cyo kufanya kienyeji.
  Nipo tayari kama kunamtu anatoa elim au sehem wanatoa elim nisome.Kingine nategemea zaidi kujitegemea na cyo kutegemea mfano km nichakula cha kuku na nguruwe niproduce mwenyewe na cyo kununua.
  Naomben sana wadau msaada wenu nategemea baada ya 5yrs na mim niwe japo nauwezo hata wakumiliki japo 5milion.
  Maeneo yapo mengi sana nimeamua kurudi kijijin nikaitendee haki ardhi huku mjini kunawenyewe.
  Hata kama mtu atakuwa na wazo tofauti la kunishauri juu ya hayo niliyoandika ntashukuru sana.
  Vilevile kama kuna m2 atakuwa na vitab au majarida yaliyozungumzia jinsi ya ufugaji ntashukuru sana akinisaidia kuyapata au kunielekeza wap ntayapata.

  Kuajiriwa sasa basi wahindi wanatuzarau sana nakutufanyisha kazi kama punda.

  Uwezo ninao nguvu ninayo na nia pia ninayo.

  Nawashukuru wote mtakao nipa michango yakunijenga na kunipa morali zaidi
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  good spirit

  anza na kidogo chochote kile, support itakuja tu baadae baada ya muelekeo kuanza kuonekana

  nakutakia mafanikio mema
   
 3. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  LETE
  Nakupongeza kwa maamuzi unayoelekea kuyachukua. La kwanza, la haraka na la msingi ambalo nakushauri ni wewe kujifanyia tathmini ya kina pamoja na mazingira unamotarajia kufanyia biashara yako. Zoezi hili litakuwezesha kubaini UWEZO wako ni mkubwa ktk maeno gani na wapi una UDHAIFU. Na kwa upande wa Mazingira itakusaidia kubaini FURSA zinazoweza kufanikishwa iwapo UWEZO wako utatumiwa vema. Na pia utajua HATARISHI zinazoweza kuvuluga mipango yako. Ukiyajua haya yote mwanzoni kabisa inakusaidia kuweka mipango madhubuti ya kuondoa UDHAIFU, kukabiliana na HATARISHI pale zitakapojitokeza huku ukitumia vema UWEZO wako kuziteka FURSA kwa mafanikio. Nakutakia mwanzo mwema na wenye mafanikio.
   
 4. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tembelea kwenye chombo husika,
  gonga hapa.
  GSHAYO
   
Loading...