Wataalam Aviation...hii ni nini?

nzalendo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Posts
12,733
Reaction score
14,160
Pale ndege inapoanza kupaa hukimbia na kupiga kelele.

Ikianza kupaa kuna hatua inafika kunatokea hali ya ukimya na wakati huo huo inakuwa kama vile inakosa nguvu na kuanza kushuka chini kidogo.

Hapo ndipo itageukia kushoto ama kulia....then ndipo unasikia machine zinanguruma nguvu kuongezeka na kuendelea na safari..

Hii inasababishwa na nini kitaalamu.

Pia wakati wa kutua hali kama hiyo hujitokeza...engine zinakuwa kama zimezimwa yaani unatokea ukimya fulani kwa muda then italala ama kushoto au kulia halafu utasikia engine zikinguruma tena hooo chini chini...usawa wa mnazi....touch down...

Hebu wataalam mtutoe hofu....
 
Kuliko kupoteza muda wako kusubiri waje kuongelea simba ya yanga na mengine yasiyohusiana ni bora ungewauliza google nini hutokea kwa ndege during takeoff and landing
 
Katika hali ya kawaida, ndege inapotaka kuruka lazima kuna speed ifikie kwanza ndipo inyanyuke
Chini ya hapo haiwezi kupaa maana haitakuwa na lift ya kutosha. Speed hizi zimegawanyika katika makundi mbalimbali.

Sasa ili ndege iweze kuondoka, lazima itengeneze msukumo wa kutosha/generate thrust. Wakati huu nguvu ya injini huwa juu. Pindi inapokimbia na kupata speed ya kuweza kuanza kunyanyuka, itapanda kwa nguvu ile ile ya injini, na pilot akishaona amegenerate enough lift ndipo hupunguza nguvu ya injini ndipo wewe utahisi kama hali ya ndege kushuka chini kidogo.

Mara nyingi ndege hazifanyi kazi at full power ya injini zinapokuwa hewani.
 
Tumekusikia kwamba unakwea pipa, jf hakuna mnyonge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…