Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 22,492
- 33,051
TUWAJUE WASWAHILI NA USWAHILI WAO
Sifa kuu ya Waswahili ni uungwana.
Hebu tuwajue Waswahili na Uswahili wao.
Picha ya kwanza inawaonyesha Waswahili katika Baraza la Wazee wa TANU mwaka wa 1957.
Picha ya chini yake inamuonyesha Mswahili Mzee Mshume Kiyate akimvisha kitambi kumfariji Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere baada ya kurejea madarakani kufuatia maasi ya Tanganyika Rifles mwaka wa 1964.
Picha inayofuatia inamuonyesha tena kulia Mswahili Mzee Mshume Kiyate kamshika mkono Julius Nyerere, pembeni ya Nyerere ni Waswahili Wazaramo Makisi Mbwana na Mzee Mwinjuma Mwinyikambi.
Hii ilikuwa mwaka wa 1962 siku ya kupiga kura ya Rais nafasi iliyokuwa ikigombewa na Julius Nyerere (TANU) na Mswahili Mluguru Zuberi Mtemvu (Congress).
Picha inayofuatia ni safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere UNO mwaka wa 1955 kulia ni Mswahili Msukuma Bi. Chiku bint Said Kisusa, Mswahili Mndengereko Bibi Titi Mohamed, Bi. Mwamvita Mwinyamani, Julius Nyerere, Mswahili Mchagga Lucy Lameck na Bi. Tatu bint Mzee.
Picha ya mwisho nimeipa jina ''Wamanyema Wanne na Mzanaki Mmoja.''
Ningeweza kuipa jina: ''Waswahili Wamanyema Wanne na Mzanaki Mmoja'' lakini itakuwa sijamtendea haki Mwalimu Nyerere kwa sababu yeye akijinasibu sana na Uswahili kufikia hadi kutunga mashairi na kuvaa kofia ya mkono.
Picha hii ilipigwa 1956 Dodoma Train Station: Kulia ni Haruna Iddi Taratibu, Saadan Abdu Kandoro, Julius Nyerere, Sheikh Mohamed Ramia na Iddi Faiz Mafungo.
Hawa Waswahili kuwaeleza historia zao inahitaji kitabu kizima.
Katika picha hizi kuna Mswahili Mdigo Dossa Aziz, Mswahili Mrufiji, Said Chamwenyewe, Sheikh Issa Nasir, Mshume Kiyate, Mswahili Mmashomvi Jumbe Tambaza, Mswahili Mzanzibari Sheikh Suleiman Takadir, Mswahili Mmanyema Mweka Hazina wa kwanza wa TANU na Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika Iddi Faiz Mafungo mkusanya fedha na mratibu wa safari ya Nyerere UNO 1955, Mswahili Msukuma Bi. Chiku mke wa Mswahili Mwarabu Shariff Abdallah Omar Attas aliyewaleta wanawake katika TANU, kwa kuwataja wachache na machache yao.
Waswahili hawa watu waungwana kwa tabia na hulka kwa kila hali.
Walifanya makubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika wakiwa bega kwa bega na Julius Nyerere lakini walizizuia ndimi zao kueleza waliyofanya.
Hawakupata kueleza michango yao hadi wanaingia kaburini.
Leo hawathaminiwi na si wengi wanaowajua wazalendo hawa.
Hawa ndiyo Waswahili wa Tanganyika na Uswahili wao.
Lipi baya walilofanya?