HUGO CHAVES
JF-Expert Member
- Mar 25, 2011
- 2,045
- 551
Waswahili husema machozi ya mamba huishia majini.wako wana jamii humu hulia aidha kwa mema kwa mahaba yao na masuala ya jamii .wengi wao machozi huishia majini ningependa kutoa Rai yangu kuwa wasipuuzwe wasikilizwe na hasa wanapotoa maoni yaojuu ya kujenga jamii Bora .mmomonyoko wa maadili upo tusipojiwekea taratibu zetu kuanzia mashuleni jinsi ya kulinda kutunza kuheshimu tamaduni zetu Kama ilivyo kwa wenzetu dunia ya Kwanza Japan wanafundisha maadili yao mashuleni na wako tofauti Sana na nchi nyingine hata vyakula .jinsi ya kuabudu kutunza vitu vya kale kuheshimiana.baina ya Rika na rika.wanaovamia maeneo ya hifadhi hapa nchini hufanya vile kwa uelewa mdogo.tuanzie mashuleni tufundishe nchi yetu inahitaji Nini kwenye jamii hii. Safari hii machozi ya mamba yasiende na maji mungu ibariki nchi yetu na tamaduni zetu.