Wasusi waaswa kutumia program ya Darling Hair kujiendeleza

Wasusi waaswa kutumia program ya Darling Hair kujiendeleza

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
810
Reaction score
1,086
Wasusi mbalimbali nchini wameaswa kutumia programu maalumu ya kampuni ya Darling Hair inayojlikana kama ‘Loyalty’ kujiendeleza kutokana na zawadi wanazoshinda.
IMG-20260915-WA0013.jpg

Hayo yamesemwa katika hafla ya kusherekea miaka miwili ya programu ya Loyalty katika ukumbi wa Sinza Deluxe ambapo wasusi mbalimbali kutoka maeneo ya Tabata, Mbezi, Kimara na maeneo ya jirani walijumuika na kufanya shughuli mbalimbali kama mziki, michezo, kula pamoja na kujishindia zawadi mbalimbali.

“Programu hii sasa ina miaka miwili na tayari tumeona makubwa ambayo imetufanyia kama wasusi kwani baadhi yetu tumeongeza mitaji na wengine ambao walianza kama wasusi wa kuajiriwa sasa wana saluni zao baada ya kujishindia vifaa mbalimbali vya saluni,” alisema Salma Hamadi kutoka Tabata.

Aliipongeza kampuni ya Darling kwa kuwajali wasusi nchini na kuwakutanisha kila mwaka kwa nia ya kuwapongeza na kuwazawadia kwa kazi nzuri.

Kwa upande wake Doreen Didas wa Mbezi Mwisho aliwataka wasusi kuendelea kukusanya lebo kwa wingi ili wajiwekee nafasi ya kushinda zawadi nyingi zaidi na kubwa kwa nia ya kutanua biashara zao zaidi. “Unaweza kuwa musi mdogo tu lakini Darling Hair wakakusaidia kukua pole pole kupitia program hii ya loyalty,” alisema.

Msusi mwingine, Shantel Mushi wa Tabata Mawenzi alisema, “Natamani wasusi wote waijue program hii ya Loyalty kwani Darling wamekuja na kitu cha kipekee chenye faida kubwa mno kwa wateja yaani sisi wasusi. Ambao hamjajiunga mmechelewa sana ila bado mna nafasi ya kujiunga na kunufaika kama sisi.”

Naye Angel Ngita wa Tabata pia, alitoa wito kwa wasusi kuwa wavumilivu na kulenga kupata zawadi kubwa ambazozitawaongezea mitaji. “Mimi leo nimeshinda lakini sichukui zawadi hii naendelea kukusanya pointi ziwe nyingi ili nipate kitu kikubwa zaidi, nimeingia kwenye program hii na malengo ili niweze kujiendeleza,” alisema.

Christina Mbando wa Tabata naye alishukuru Darling Hair kwa kuwa karibu na wasusi na kuwakutanisha na kuwafuatilia kila hatua jambo ambalo limewafanya wasusi wapige hatua kubwa kimaendeleo. “Hakuna kampuni inafanya kama Darling Hair tunawaomba wasiachie programu hii ili wasusi tuendelee kunufaika zaidi.”

Mwakilishi wa Darling Hair, Daniel Kisusange alisema kampeni hiyo ya Loyalty inatarajia kuhamia miakoani ili wasusi wa mikoa mbalimbali nao wafikiwe. “Tunawaomba mjiandae tunakuja huko maana kampeni hii ni ya nchi nzima na lengo ni kuendelea kuwafikia wasusi wengi zaidi,” alisema.



Alifafanua kuwa walianza na wasusi 5000 katika mwaka wa kwanza lakini sasa hivi wameshasajili zaidi ya 10,000 ambao wananufaika na program hii ya loyalty inayolenga kuwanyanyua wasusi wadogo wadogo ili wapate mitaji ya kujiajiri wenyewe.

Alitoa wito kwa wasusi waendelee kutumia program hiyo kujitanua zaidi kwani ni mpango wa kudumu wa kampuni hiyo.
IMG-20260915-WA0014.jpg
IMG-20260915-WA0012.jpg
IMG-20260915-WA0015.jpg
IMG-20260915-WA0015.jpg
IMG-20260915-WA0012.jpg
 
Back
Top Bottom