Wastara: Sipo kwa ajili ya kujiuza

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
wastara1.jpg


Staa wa Bongo Movie, Wastara Juma ambaye siku za karibuni aliomba talaka kutoka kwa mume wake amefunguka na kusema yeye sio mtu wa kujiuza, bali ni mtu ambaye anajijali na kujitunza.

Wastara alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWS ambapo inasemekana kwa sasa kuna wanaume kibao ambao wanajitokeza kumtaka baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama cha CCM (UVCCM) Taifa ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma.

Msanii huyo amesema kuwa ni kweli wapo wanaume wengi wanaojitokeza kumtaka na wengine wakija na ahadi ya ndoa lakini bahati mbaya wanaume hao wanakuja wakati yeye haitaji kuwa na mtu kutokana na jinsi alivyoumizwa.

“Mimi si mali ya mtu na wala sipo kwa ajili ya kujiuza, lakini ukweli ni kwamba wapo wanaume wa aina nyingi ambao wanakuja na kunitaka wengine wanakuja wakitaka ndoa kabisa na wengine unakuta kweli wanania ya dhati kabisa lakini wanakuja wakati mimi sijisikii kuwa na mwanaume, maana kitu kwa kitendo alichonifanya Sadif hakijaniweka sehemu nzuri” alisema Wastara.

Source: eatv
 
tatizo nini wastara mama?ulimbukeni na dharau ndo zinawaponzaga nyinyi bongo movie wa like,nlikupenda ulivojiheshimu kpind na sajuki,ila kashfa zako za kubadilisha mabwana na wame za watu ndo zinakuponza,na utaandamwa na mzimu wa sajuki mpk basi
 
tatizo nini wastara mama?ulimbukeni na dharau ndo zinawaponzaga nyinyi bongo movie wa like,nlikupenda ulivojiheshimu kpind na sajuki,ila kashfa zako za kubadilisha mabwana na wame za watu ndo zinakuponza,na utaandamwa na mzimu wa sajuki mpk basi
Sasa ataishije mjini hapa asipobadili badili??

Mjini msingi kiuno....
 
Sasa ataishije mjini hapa asipobadili badili??

Mjini msingi kiuno....[/QUO ila kweli ukiangalia % kubwa ya hao wanaoitwa supa staa wa like bongo ni mambo yao yanafanana ktk mahusiano,yule aliolewa Dubai na yule jamaa,mshkaj alipopigwa ndani,kazaa na dancer wa dangote,duh,c angembebea mimba Mme wa ndoa? wanacheza na mungu hawa dada zetu ( viapo vya ndoa) mbele ya mashahidi,mwingine anabadili dining kila kukicha kisa kuolewa,Mara mkristo,Mara karud uislam? wawe na msimamo bana.
 
Back
Top Bottom