Wastaafu kubadilishiwa kadi za NHIF

SUTAGI-

JF-Expert Member
Nov 9, 2018
269
511
Kuna zoezi linaendelea nchi nzima kwa wastaafu kuripoti ofisi za NHIF zilizo karibu yao ili wabadilishiwe kadi zao za bima ya afya.

Nilipokea taarifa hii juzi kabla hata ya ripoti ya CAG kuhusu wastaafu na NHIF.

Sina shaka kuwa sababu za kubadili kadi hizo zimelenga kupunguza huduma za afya wanazopatiwa wastaafu kupitia mfuko huo.

Kauli ya Kichere inasadifu ukweli kuwa wastaafu wanaenda kukutana na adhabu ya kupunguziwa huduma kwenye kitita cha mafao ya NHIF.

Huu ni uamuzi wa ajabu sana kuridhiwa na kupitishwa na utawatafuna wengi sana.

Wabunge nyie ni wawakilishi wa wananchi katika hili mkijichanganya mtaumbuka sana na kumbukeni nyie ni rahisi sana kurudi mtaani kuliko hata Mwalimu.

Haiwezekani mnakubaliana kujiongezea mishahara yenu, mnapendekeza wenza wa viongozi wakuu wastaafu walipwe mishahara na fursa lukuki LAKINI wastaafu waliowawezesha kufika hapo mlipo mnawanyanganya hata ile fursa mdogo waliyokuwa nayo.

It's shame kuona mnapitisha kikokotoo kwa wastaafu, mnawanyanganya na fursa ya kupata tiba wakati wameitumikia nchi hii kwa jasho na damu tena kwa kulipwa mishahara midogo.

Wananchi tuamke.. tuwawajibishe hawa viongozi walafi.

Mwalimu, Nesi, Injinia, Karani, Hakimu, Polisi, Daktari, Mhasibu, Watendaji wote amkeni katika hili... Nyote ni wastaafu wategemewa.

Pia soma > CAG: Wastaafu na Wenza Wao wanaigharimu NHIF tsh 84.7 billion kila Mwaka Bila Wao kuchangia
 
  • Thanks
Reactions: apk
Walimu ndio wanasimamia wizi wa Kura za ccm.

Mlipo makazini ukiona mwenzako ananyolewa wewe Tia maji za kwako.

Solution ni kuiondowa CCM tu.
 
Back
Top Bottom