Wastaafu walia na serikali........................... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wastaafu walia na serikali...........................

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Jan 6, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,266
  Trophy Points: 280
  Wastaafu walia na serikali


  na Ambrose Wantaigwa


  [​IMG] BAADHI ya wastaafu waliokuwa watumishi wa serikali katika idara mbalimbali wameitaka serikali kufikiria kubadilisha utaratibu wa malipo yao ya pensheni kulipwa kila mwezi badala ya utaratibu wa sasa wa kulipwa baada ya miezi sita.
  Walidai kuwa utaratibu wa sasa unawasababishia ugumu wa kutekeleza mahitaji yao ya kila siku ikiwemo kupata matibabu kutokana na kupanda gharama za maisha siku hadi siku.
  Wakizungumza na gazeti hili jana mjini Tarime wastaafu hao ambao wengi walionekana kuwa na umri wa kati ya miaka 65-75 walisema awali serikali kupitia hazina ilikuwa na utaratibu wa kuwalipa kila mwisho wa mwezi na kisha baadaye ilibadilisha na kuanza kuwalipa baada ya miezi sita.
  Mmoja wa wastaafu hao ambaye pia ni mwenyekiti wa muda wa umoja huo wilayani hapa, Otuno Bwana, alisema baadhi ya wazee hawana watu wa kuwahudumia mahitaji ya nyumbani kama vile chakula na mavazi na wameishi kama ombaomba licha ya kutoa mchango wao kujenga taifa wakiwa watumishi.
  “Umefika wakati serikali ituangalie kwa macho ya huruma ikiwa pamoja na kusimamia huduma za msingi kama vile matibabu kwetu kwa kuwa tunastahili kupata mgao wa keki ya taifa ambayo kwa nafasi zetu tulishiriki kuitengeneza,” alisema.
  Alisema katika maisha ya mtanzania wa kawaida kiasi cha dola moja ya Kimarekani kwa siku wanashindwa kuhimili makali ya maisha na hivyo kulazimika kuingia mikopo ambayo hujilimbikiza hadi kipindi cha miezi sita na hivyo kulazimika kutumia penseni hizo kulipa.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,266
  Trophy Points: 280
  Kuwalipa mafisadi wa DOWANS ni kitendo cha haraka lakin kuwalipa haki halali wastaafu serikali ya kifisadi hii yapata kigugumizi............
   
Loading...