Wastaafu wa Zanzibar

mwanzilishi

Member
Jan 11, 2007
22
0
Kwa nini Viongozi wastaafu wa Zanzibar hawakai Zanzibar? Kuanzia Jumbe, Mwinyi, Salim A Salim n.k. je ni kweli hawapendi kwenda kuishi Zanzibar au kuna kilichojificha? Je wamejenga nyumba zao Dar Es Salaam tu?
 
Salmin yuko zanzibar, Mohammed Gharib bIlali yuko Zanzibar, Marehemu Idrissa Abdul wakil kafia na kuzikwa zanzibar, Marehemu Ramadhan Haji kafia na kuzikwa zanzibar.

Salim ana nyumba zanzibar na anakwenda, Mwinyi ana nyumba zanzibar na anakwenda na mashamba pia, Jumbe yeye mwenyewe kasema kwao si Zanzibar kaamua kujenga kwao na akaandika mtu kwao

maamuzi ya mtu kukaa anapotaka na kuhisi ni wepesi kufanya shughuli zake au mkuu kuna jambo jengine umelificha kama lipo liweke wazi maana njia hii uliopita ni vigumu kuwa kweupeni
 
Kwa nini Viongozi wastaafu wa Zanzibar hawakai Zanzibar? Kuanzia Jumbe, Mwinyi, Salim A Salim n.k. je ni kweli hawapendi kwenda kuishi Zanzibar au kuna kilichojificha? Je wamejenga nyumba zao Dar Es Salaam tu?

Kwa nini Viongozi wastaafu Tanzania hawarudi kwao? Wanang'ang'ania Dar? Kawawa- Kibamba, Sumaye- Dar, Warioba- Dar, Mkapa Dar (emejenga Lushoto pia). n.k!

Kwao ni wapi? Walipozaliwa?
 
Kwa nini Viongozi wastaafu wa Zanzibar hawakai Zanzibar? Kuanzia Jumbe, Mwinyi, Salim A Salim n.k. je ni kweli hawapendi kwenda kuishi Zanzibar au kuna kilichojificha? Je wamejenga nyumba zao Dar Es Salaam tu?

Wakae Zanzibar kwani kwao? viongozi wakuu wastaafu karibia 80% ni majasusi tu, wanajichanganya then wanafanya walilotumwa baadae wakimaliza wanarudi nyumbani kwao.
Huyu mtoto wa Mwinyi kaacha ubunge Mkuranga then kaja Kwahani ZNZ, akistaafu utasemaje! kakimbia au karudi kwao?
Anewei madhali wapo Tanzania sheria inawaruhusu.
Maneno ya Mtu wa Pwani: kama kuna kitu umeficha weka wazi MWANZILISHI
 
Back
Top Bottom