Wastaafu wa EAC wakutana na Luhanjo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wastaafu wa EAC wakutana na Luhanjo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jul 26, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,586
  Likes Received: 82,137
  Trophy Points: 280
  Wastaafu wa EAC wakutana na Luhanjo
  Mwandishi Wetu
  Daily News; Saturday,July 26, 2008 @00:03

  Wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), jana walikutana na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo ili kujadili mustakabali wa malipo yao. Mkutano huo uliitishwa na Luhanjo siku moja baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuzungumzia suala la wastaafu hao bungeni Dodoma.

  Waziri Mkuu aliitaka Wizara ya Fedha na Uchumi kuchapisha taarifa za malipo ambayo serikali imekwisha lipa na hundi ambazo serikali ilizitoa, lakini wastaafu wakashindwa kuzichukua. Jana mchana wastaafu zaidi ya 100 walikusanyika nje ya Ikulu Dar es Salaam na kuchagua wenzao saba ambao waliingia ndani kwa ajili ya kuzungumza na Luhanjo.

  Taarifa ya wastaafu kwa Luhanjo ilimtaka Rais Kikwete kuingilia kati suala hilo na kuchukua uamuzi wa kufuta kesi iliyopo mahakamani ya wastaafu hao na kuwalipa. “Tunaamini uwezo anao wa kuamua kama Rais Museveni wa Uganda alivyowafanyia wenzetu kwa kutoa kesi mahakamani na kuwalipa,” ilisema taarifa hiyo.

  Wastaafu hao waliosema wanaidai serikali kiasi cha Sh bilioni 400, walikuwa wakiwasubiri wenzao kwa hamu chini ya mti karibu kabisa na geti la Ikulu mpaka walipoondolewa. Muda mfupi baada ya wawakilishi hao saba kuingia Ikulu, mmoja wao alitoka nje na kuwajulisha wenzao kuwa wanatakiwa kuondoka eneo lile ili mazungumzo yaweze kuendelea.

  “Ndugu zangu wenzetu huko ndani wamesema hawawezi kuzungumza na sisi kama kuna watu wamejaa hapa nje, tunaomba ama muondoke halafu tuwape majibu baadae au msogee pembeni,” alisema Nathaniel Mlaki. Baada ya tangazo hilo, baadhi ya wastaafu wakaanza kupiga kelele za kukataa, lakini wengine walitii na kusogea upande wa pili wa barabara karibu na Wizara ya Fedha na Uchumi.
   
 2. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli I am down with this, kwa sababu hata mzazi wangu anawadai hela nyingi sana EAC za mafao yake baada ya kuwafanyia sana kazi enzi zile,

  aliniambia kuwa kwa hesabu za sasa anawadai karibu shillingi million 60, yaani I cannot wait kuona the end of this, yaani malipo!
   
Loading...