WASTAAFU NA NSSF

bibinnaa

JF-Expert Member
Jan 17, 2017
1,501
2,000
Natanguliza salaam za kheri kwenu nyote.
Nimekuwa nikilipwa Pension yangu tarehe 25 ya kila nwezi bila matatizo na ndivyo tulivyokubaliana na NSSF wakati nachukuwa malipo yangu ya mwanzo.
Mimi hupokelea pension yangu katika moja ya Ofisi au matawi ya Post Office Dar...miezi kama minne iliyopita wafanyakazi walibadilishwa kitu ambacho ni cha kawaida..wapya waliokuja wanachapa kazi vizuri.Tatizo ni kwamba hatupati pesa yetu hiyo tarehe 25 na tukiwauliza tunajibiwa utaratibu sasa ni tarehe 30.Lakini cha ajabu kama unalipwa chini ya laki moja unaambiwa subiri tukusanye malipo ya wanafunzi tukulipe na una saini katika vocha za NSSF.
naomba wenye habari zaidi watujuze nini kinaendelea.
Staha tafadhali...umri umekwenda.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom