Wastaafu kupishana lango la Ikulu, kuna nini?

Jan 1, 2016
80
12
Nimeshangazwa Na kushtuka kuona viongozi wastaafu wakiongozwa Na Mh.Kikwete , Mkapa Na Warioba wakipishana kwenye mango la Ikulu kwenda eti " KUMTAKIA HERI YA MWAKA MPYA" Rais Magufuli.Mwingine alienda mbali zaidi akasema "Anaomba Rais amtume kokote" Mie nilidhani Rais huwa anautaratibu Wa kutakiana hero ya mwaka mpya tena Kwa Watanzania wote , hao wastaafu wapumzike tu makwao muda ukifika atawaalika.Na huyo anayetaka atumwe yeye amestaafu Kwa maana apumzike watanzania wapo wengi atapatikana Wa kutumwa mwacheni Rais apumzike jamani.
 
Sasa we unahisi nn? Kwan ni vibaya kwenda kuongeanao? We watakuambia tu tumemtakia heri na nini nanini ila mule ndani yapo mazungumzo ya siri mule hasa huyuu mzee warioba naona kabisa kipo kilichompeleka mule sio bwaja yule kama Sumaye maana atangekuwepo CCM wala sioni angeonda kuongea nn na Ngosha
 
Mkuu hawa wastaafu wameitwa Ikulu na ni haki yao kwenda maana rais ni mwanachama mwenzao mbona wataafu kama kina Kingunge, Sumaye, kila siku wapo na Lowassa hata siku moja ujasema wapumzike makwao
 
Last edited:
Wameenda kumwambukiza utembezi, matusi na kusamehe unapopigwa kelbu
 
Nimeshangazwa Na kushtuka kuona viongozi wastaafu wakiongozwa Na Mh.Kikwete , Mkapa Na Warioba wakipishana kwenye mango la Ikulu kwenda eti " KUMTAKIA HERI YA MWAKA MPYA" Rais Magufuli.Mwingine alienda mbali zaidi akasema "Anaomba Rais amtume kokote" Mie nilidhani Rais huwa anautaratibu Wa kutakiana hero ya mwaka mpya tena Kwa Watanzania wote , hao wastaafu wapumzike tu makwao muda ukifika atawaalika.Na huyo anayetaka atumwe yeye amestaafu Kwa maana apumzike watanzania wapo wengi atapatikana Wa kutumwa mwacheni Rais apumzike jamani.

Mkuu, mbona ni kawaida sana. Hata mtaani kwako kuna nyumba inapata wageni wengi kuna nyumba haipati wageni. Inategemea mwenye mji ana mahusiano gani na watu wanaomtembelea. Bila mahusiano mazuri mtaani hawezi kuwa na mgeni
 
Hao ni wastaafu, walishakuwepo hapo. Wazungu wamasema "Been there done that" kwa hiyo hakuna kigeni. Ila wewe ukienda enda ikulu lazima tuulizane na issue gani na Rais..
 
Nahisi kuna ishu nyeti aidha mkulu ameamua kuwashirikisha kwa maana ya kuomba ushauri au kuna maamuzi mazito mkulu alitaka kufanya sasa wamekwenda kumsihi alegeze kamba. Have a look at the figures Jk, Ben, Jaji na Abdallah hawa wote walikuwepo kwenye timu ya ushindi hivyo nitakuwa wa mwisho kuamini kwamba ni salamu tu mbuuulah!!!
 
kwanini ushangazwe na kushtuka viongozi wastaafu wakienda kumtakia heri ya mwaka mpya jpm. je, hujui kuwa:
bwm alimuibua jpm. ni kijana wake. akiwa kamanda jpm alikuwa askari wa mwamvuli katika kikosi chake. leo jpm ni kamanda, unashangaa na kushtuka nini bwm kwenda ikulu?
jk ndo kamwachia kijiti. ni ajabu kwenda kumpongeza na kumtia moyo ili wapinzani waendelee kuisoma namba miaka 10 ijayo kama ilivyokuwa miaka yake 10 iliyopita?
jsw ni mgodi unaotembea wenye madini ya thamani(hekima, busara, maarifa). bila shaka jpm alijichotea madini ya kutosha yamsaidie mbele ya safari.
usiwe na wasiwasi na wazee hawa kwani si wahuni wa kubadili gia angani hata kuwafanya wengine roho ziwasute na wengine watimue mbio. ni wastaarabu na makini.
katika mikono yao ccm na serikali yake zi salama na ule wimbo 'ccm mbele kwa mbele' tutaendelea kuuimba kwa miaka mingi ijayo.
wastaafu waendelee kwenda ikulu, jpm ni kijana wao.
 
Last edited:
Back
Top Bottom