Wastaafu kupishana lango la Ikulu, kuna nini?

Wastaafu kupishana lango la Ikulu, kuna nini?

Nimeshangazwa Na kushtuka kuona viongozi wastaafu wakiongozwa Na Mh.Kikwete , Mkapa Na Warioba wakipishana kwenye mango la Ikulu kwenda eti " KUMTAKIA HERI YA MWAKA MPYA" Rais Magufuli.Mwingine alienda mbali zaidi akasema "Anaomba Rais amtume kokote" Mie nilidhani Rais huwa anautaratibu Wa kutakiana hero ya mwaka mpya tena Kwa Watanzania wote , hao wastaafu wapumzike tu makwao muda ukifika atawaalika.Na huyo anayetaka atumwe yeye amestaafu Kwa maana apumzike watanzania wapo wengi atapatikana Wa kutumwa mwacheni Rais apumzike jamani.
nadhani walienda kumwambia aache hii bomoa bomoa bila taratibu maana 2020 haiko mbali.
 
Mkuu hawa wastaafu wameitwa Ikulu na ni haki yao kwenda maana rais ni mwanachama mwenzao mbona wataafu kama kina Kingunge, Sumaye, kila siku wapo na Lowassa hata siku moja ujasema wapumzike makwao
mkuu naona umeamua kugonga penyewe kabisa. waonee huruma hao jamaa maana siku hizi hawana hoja tena. wanatia huruma huku mitaani mbayaaaaa.
 
WAMWAMBIE MDA WA KUPEWA BIMA YA AFYA WATZ WOTE UMEFIKA
 
Bila shaka walienda kumwambia kuhusu bomoa bomoa.
 
Mkuu hawa wastaafu wameitwa Ikulu na ni haki yao kwenda maana rais ni mwanachama mwenzao mbona wataafu kama kina Kingunge, Sumaye, kila siku wapo na Lowassa hata siku moja ujasema wapumzike makwao
Kumbe Lowassa ni Rais??
 
INGEFAA TENA WARUDIE WOTE KWA PAMOJA KUKUTANA NA RAIS. KWA KUJENGA UMOJA WA TAIFA .MMOJAMMOJA WANAMCHANGANYA.
 
Kimsingi viongozi wetu hawajiamini na si wa kweli katika kuongoza Nchi hii !! Ndiyo maana hata vikao vyao na vya kushtukiza shtukiza tu na hakuna kauli inayo tolewa baada ya hapo kwani kimsingi hawajadili Maslahi ya Taifa bali wanakwenda kujadili Maslahi yao na vikundi vyao au Familia zao. Watanzania tukibakia wasindikizaji tu.
 
The problem with you guys mnadhani mnamfahamu sana Magufuri wakati hamumjui! Tatizo lingine mnadhani mnafahamu hii nchi inaongozwaje wakati vile vile hamfahamu! Na kubwa zaidi mnadhani Magufuri ni superman asiyehitaji msaada wa yeyote wakati si kweli. Juzi tu hapa mlianza kukashifu na kutukana watu na kushadadia u-superhero wa Magufuri kwa suspend mradi wa Bagamoyo Port kumbe zilikuwa ni habari za uzushi!
 
R
ais ni binadamu kama wengine, anahitaji maongezi pia na kupata wageni kusihusishwe na mambo mengine.
Hao wazee wastaafu (Mkapa.Warioba na Kikwete) ni wazoefu,wamekuwa katika uongozi miaka mingi zaidi ya Mh raisi Magufuli, ikulu pia wanaijua vizuri zaidi yake,hivyo sio vibaya kushare best practice na watangulizi wako. Hata mtu aliefanya mabaya,yapo mazuri pia ambayo si vibaya kujifunza kwake!
Nafikiri tuwaache wazee hawa waongee na kijana wao,wampongeze pale anapofanya vizuri na wamshauri pia pale wanapoona anatoka kidogo kwenye utaratibu. Huu ndo uongozi bora wa kupokea ushauri pia.
 
Mkuu hawa wastaafu wameitwa Ikulu na ni haki yao kwenda maana rais ni mwanachama mwenzao mbona wataafu kama kina Kingunge, Sumaye, kila siku wapo na Lowassa hata siku moja ujasema wapumzike makwao
Nimependa comparison yako!
 
Uzoefu Wa nini? Hao wazee ndio waliowachosha watanzania Kwa tawala zao za ajabu Huyo mwingine kamteua warioba kuandaa rasimu ya katiba kisha anamruka Na kumkejeli ndio uzoefu huo? Tumewachoka wapumzike
 
Back
Top Bottom