Wassira,Unatania au Unawakejeli !!

Wassira,Unatania au Unawakejeli !!

wana-Bunda, asubuhi na mapema october 25 mnyoosheni huyo babu akacheze na vitukuu. Mkimpa nafasi safari hii atakwenda bungeni na blanketi akalale kabisa:sleepy::sleepy::sleepy:.
 
Kaaah! Eti hata jembe la mkono watalisahau! Kwa kweli huko ni kuongea kwa kufikiri kwa manani! Mak**o! ni mtu Wa ajabu sana huyu Mzee! Wapi project ya kilimo kwanza!? Sio siri anatia hasira sna! Badala ya kuwaambia wananchi wake issues km pembe za ndovu zilikamatwaje uswis yy analeta blabla hapa!!
 
Leo akiwa anachukua fomu ya kugombea ubunge jimbo la Bunda amewambia wananchi kuwa wamefhamiria kupambana na umasikini na tatizo la ajira kwa vijana ktk miaka mitano.

Wasira anatania au anawakejeli?

Hiyo ni ndoto aliyoota alipoamka kwenye gari mzee kwa kuuchapa huyu
 
Mkuu naluunga mkono. Lakini kama ni bakora alipaswa achapwe siku aliyotangaza nia ya kugombea urais pale aliposema amedhamiria kuondoa kilimo cha jembe la mkono na akiwa rais ataliweka kwenye jumba la makumbusho. Hapo bakora zilipaswa zitembee maana alishindwa vipi japo kuliboresha hilo jembe la mkono angalau litumie batrii za tochi alipokuwa waziri wa kilimo? Licha ya hicho alichokisema kuliweka kwenye jumba la makumbusho....

Analeta maigizo tu, hawezi kuleta mabadiriko yoyote ya maana - binafsi nilimshangaa sana alipo hamishiwa Wizara ya Kilimo kitu alicho fikilia kwanza na kutoa vibari kwa wafanya biashara waingize Sukari!! Hayupo concern na wakulima wa miwa ambao ndio wangeongeza ajila nyingi kwa vijana na kulinda viwanda vyetu vya SUKARI, hilo hakulipa kipa umbele hata kidogo - katupilia mbali hata makubaliano yaliyo kuwa yamefikiwa na Waziri aliye mtangulia baina ya Wakulima wa miwa na wamiliki wa viwanda vya kusindika sukari nchini,sikuona kama alikuwa na nia thabiti ya kulinda viwanda vyetu vya sukari zaidi ya kuwajali zaidi waingiza Sukari nchini, binafsi sikupenda attitude yake towards Sugar Industry in our Country!!

Mtu ungetegemea angechukulia seriously matokeo ya Uchunguzi na mapendekezo mahili yaliyo fanywa na Chuo Kikuu cha Sokoine kuhusu matatizo katika sekta ya Sukari nchini na kuyafanyia kazi fasta, si Wizara wala Waziri mwenyewe hawajiulizi hivi Shirika la Sukari lilianzishwa na Rais Nyerere kwa madhumuni gani - linahachwa kufanya kazi ya udalalai wa sukari i.e kugawa vibali vya sukari kazi hiyo siku hizi ndio imechukuliwa kama ndio core business ya shirika hilo - sekta nyingine muhimu hazipewi kupaumbele - je hii ni bahati mbaya au delibarate move? - someni report ya tafiti ya Chuo Kikuu cha Sokoine kilisema nini kuhusu Shirika hilo la sukari - lipo lipo tu lime-derail kabisa mantiki ya kuazishwa kwake na Baba wa Taifa wakishirikiana na Kanali Kashmir - Kanali yungali ahi kwa nini ahulizwi lilianzishwa kwa madhumini gani hasa.

Wanasiasa bwana!! Wanachekecha na kuona wapiga kura wengi watakuwa ni vijana hivyo wanatoa ahadi za kubuni tu mradi washinde kura na kurudi Bungeni,tuwe wakweli hapa Kilimo nchini kinapewa lip service tu kwa muda mrefu - matrekta wanayo zungumzia kila siku sio kwamba adhithi hizo zimehanza leo waliwahi kuleta trekta za Valmet kutoka Finland, Swaraj kutoka India, Fiat kutoka Italy yote hayo yaliletwa nchini nikiwa bado nasoma, leo hii wanaweza kutwambia yaliwahi kuleta mabadiriko gani ya kilimo nchini - tukiwekea maanani kwamba Mh.Wasirra aliwahi kufanya kazi katika Wizara hiyo zaidi ya mara moja - hivi Taifa letu lina kitu cha kujivunia katika sekta ya kilimo kweli?
 
Hata mimi nimemsikia, kazungumzia pia wakulima kutumia jembe la mkono na hili alilisema wakati akipiga kampeni za kuutaka urais, sasa nashangaa huyu ndo waziri mwenyewe yupo kwenye kiti (au nakosea?), hajaweza sasa anataka awe rais ndo aweze...
hata hivyo mimi huwa nashangazwa na washangiliaji zaidi, watanzania tujiongeze jamani
 
Back
Top Bottom