Mwanasiasa jina lake tu ndo husema ukweli.
Mkuu naluunga mkono. Lakini kama ni bakora alipaswa achapwe siku aliyotangaza nia ya kugombea urais pale aliposema amedhamiria kuondoa kilimo cha jembe la mkono na akiwa rais ataliweka kwenye jumba la makumbusho. Hapo bakora zilipaswa zitembee maana alishindwa vipi japo kuliboresha hilo jembe la mkono angalau litumie batrii za tochi alipokuwa waziri wa kilimo? Licha ya hicho alichokisema kuliweka kwenye jumba la makumbusho....Kiuhalisia huyu mzee uwezo wa kufikiri umeisha yaani katika awamu zote za tawala za nchi hii yupo kama kiongozi ameshindwa kuchangia kuondoa umasikini wa watanzania halafu leo hii anasema wakichaguliwa atautokomeza umasikini kwa miaka mitano. kilichonisikitisha ni hao waliokuwa wakimsikiliza pasipo kuchukua hatua yeyote kwani walitakiwa wamtie bakora kwa kuongea ujinga kama huo.