Wassira si msafi; achunguzwe!

Kumbe ana uzoefu,sasa rasimali za nchi ukimwachia mwizi asimamie unategemea nini
 
Duuuu, jamani mwishowe mtakuja na kashfa ya KUKOMBA MBOGA akiwa darasa la nne mwaka 1965. Kazi kwelikweli. Ukiwa kwenye nyumba yenye vioo usimrushie mwenzie jiwe.
 
CDM wana mafaili ya kila mtu!! Mtu akijipendekeza kifisadi anapewa file lake. M4C
 
"Msimuandame handsome wetu!!" Mpeni heshima yake au hamjui kwamba analiingizia Taifa pesa nyingi za kigeni kutoka kwa watalii wanaongia nchini!!? Kwa taarifa yenu yeye ndie kivutio cha watalii hapa Bongo ha Ikulu!! MUHESHIMUNI!!
 
Mwangalieni vizuri huyu jamaa anavyotetea Magamba wenzie, waswahili wamesema " aisifiae mvua imemnyea". Jamaa anaonyesha yuko pale Magogoni kimalengo na biashara zake haramu!
 
SIYO VIVYO TU MKUU. WASSIRA MWAKA 1995 akiwa NCCR-MAGEUZI alimtukana JAJI WARIOBA aliyekuwa mgombea wa CCM UBUNGE JIMBO LA BUNDA kwamba wanannchi wasimchague WARIOBA kwani anaumwa (1) UKIMWI, (na (2) TB hivyo atakufa baada ya uchaguzi. WASSIRA akachaguliwa MBUNGE kupitia NCCR. WARIOBA akapinga matokeo. Mahakama Kuu IKAFUTA MATOKEO KWANI WASSIRA (1) alitumia lugha ya ubaguzi, na (2) alitoa HONGO na kumzuia WASSIRA asijihusishe na siasa kwa miaka 5. TATIZO LA TANZANIA USAHAULIFU, WASSIRA HAFAI, BUSARA HANA (REJEA HUKUMU HIYO)

 
Wa kulaumiwa hapa ni RA aliyemrudisha Wassira wakati wanaunda mtandao wao haramu wa kukamata IKULU. Mzee huyu kabla Uchaguzi Mkuu mwaka 2005 alikuwa hoi bin taabani akivaa soksi vidole vinachungulia nje kama kichwa cha kobe na gamba lake. RA akamfuata akampiga jeki la nguvu akamwezesha kwa sana tu kugombea Ubunge Bunda. Kwa kuwa Mzee wetu huyu ni mshawishi, mfitini na mjenga hoja mzuri akafiti sana ndani ya Mtandao. Alipopita Ubunge Cabinet ya kwanza ya JK akaukwaa Uwaziri. Akaingia kwa nguvu sana kuzitafuna taasisi zilizokuwa chini ya wizara alizopitia. Ametoka. Ana miradi mingi tu sasa. Ana kahoteli kake kule Mbugani Serengeti pia. Hakufanya makosa safari hii.
 

Binafsi naikumbuka sana hukumu hii, kwa kuwa miaka hiyo nilikuwa nishaanza kujiingiza katika kushabikia siasa. Kimsingi jamaa hafai kuwa kiongozi mwadilifu
 
Aseee!!!!sasa hilo tairi alilifungua kwenye gari au aliliiba stoo?nafikiri alitoka nalo nduki ya kufa mtu,CCM haya mambo ya wizi wameanza nayo mbali sana.
 
ni mimi ndio nilianzisha uzi wa kutaka kufahamishiwa majukumu ya kisheria wa Waziri Wassira maana najua yuko 100% kinyume historically anayotakiwa kuyasimamia/kuyaongoza. Wakati wa utawala wa Clinton, alimteua mama fulani kuwa Waziri wa Sheria, ikaonekana katika historia ya yule mama alipata kuajiri housemaid ambaye ni illegal immigrant so akajiuzulu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…