Usiyemtaka ndie atakaye kua mkuu
Nikwleli kabisa mkuu kwasababu kule kwenye pori letu kigoma tunahitaji mgombea mahiri kama wasiraWassira anazo sifa na ni kiongozi aliye tayari kuwatumikia wanyonge, Goo Wassira Gooo!
Wasira hata bungeni hatarudi sasa izo ndoto za urais ni kujitafutia umaarufu tu wa mwisho mwisho
KILA la HERI -Mungu awe nawe
Hata kwa dawa siwezi kumpa kura yangu! Mzee kama huyu anataka uraisi ili iweje? hana mawazo mapya kwanza uwezo wa kufikiri nao hana tena!
duh kweli 2015 ni shiiida mpaka huyu mzee anataka uraisi
Ni sheeedah....
1. Katika CCM Mzee wasira ndio kiongozi anayeweza kurudisha mshikamano na umoja ndani ya chama kwa kuwa hana makundi ya kisiasa.
2. Uadilifu wake ni sifa ya kiongozi tunayehitaji kwa sasa ili aweze kusimamia maendeleo ya nchi hii lakini pia kusimamia maadili ya nchi yetu ambayo yamepotoka kwa hali ya juu sana
3. Usafi wake dhidi ya ufisadi ndio silaha tunahitaji kwa kiongozi ajaye ili awe huru na jasiro kupambana na mafisadi na wala rushwa bila aibu kwani atakuwa hadaiwi na mtu na atakuwa hahitaji kumlipa mtu fadhira zozote.
4. Ujasiri wake ndio nguzo katika kutetea na kusimamia amani ya nchi yetu, hatakuwa legelege.
5. Uwezo wake katika masuala ya kiuchumi na mipango ndio tunachohitaji katika kuelekea katika uchumi wa gesi na jinsi ya kusimamia vizuri rasilimali za taifa katika kukuza uchumi.....
Mzee wasira ni mteteZi wa Taifa
Mzee wasira ni mtetezi wa Chama
Mzee wasira ni hazina ya Taifa
Akigombea uraisi atatufaa, tumuombee afya njema na umri mrefu.
Mkuu hiyo ni njia nyepesi ya kujitoa kiaina kwenye ubunge, maana ameshapima kabisa ndani ya chama hatatoboza kwenye kura za maoni! Kale kabinti kasagaji kamembana mpaka hapumui, huku nje nako Dr. Webiru anamtoa kamasi siyo kidogo, hivyo sokwe anatafuta mlango Wa kutokea!! "SIONGOZWI NA SOKWE MIMI"
Afanye plastic surgery kwanza!
Maneno ya hovyo yanayotoka kwa MTU hovyo. Alilopanga Mungu Mwanadamu hana nafasi WASIRA FOR 2015Basi hilo litakuwa jinamizi la hatari!. Na ili nisiote hilo lindoto, bora nisilale kabisa. WASSIRA HATAKUJA KUWA RAISI WA NCH YOYOTE DUNIANI!!!!. Take it from me. Hata akihamia chama gani, watakaomwinua lazima wapoteze!!!!!!!!!..
Wasira nae awe rais...hivi ccm mmesahau maneno ya nyerere..."kiongozi bora ni yule asiyetaka kuwa kiongozi"..kauli hii ina maana kubwa sana tofauti na hawa ccm wanavyogombea wenywe kwa wenyewe..nyerere alisema upinzani haupo nje ya ccm bali utakuwa ndani ya ccm sasa nimeanza kuona...yani wanasema kuhusu ukawa istoshe ukawa ipo ndani ya ccm wenyewe..embu wajipime vizuri sio kila mtu anatumia mgongo wa kusema kaombwa na watu wengi hicho sio kigezo cha kuwa kiongozi..tutajuaje waliokuomba ni ndugu zako na sio watanzania wote au ni wale wanaotaka ukiwa rais wapate cheo..embu jichunguzeni kwanza sio kila mtu anafaa kuwa kiongozi kwa kuombwa..halafu wasira mbona hizo sera zako ni weak sana kwa taifa hili yani sijaona kipya na wakati ulikuwa waziri wa kilimo mbona haya yote hukupendekeza zaidi ya kuwa kama waziri pazia tu..sijaona kipya mpaka sasa kwa wagombea wote zaidi ya purukushani na uchu wa madaraka..na wengine ndani ya ccm wanampiga vita lowasa maana wanajua akiwa rais watakiona cha mtema kuni walivyomchongea ajiuzulu uwaziri mkuu
.