Wassira: Nitagombea urais 2015

Yaani kila mtu "nimeombwa na watanzania" tutasikia mengi mwaka huu
 
Wananchi wanaozungumziwa hapa ni hawa Buku 7, pia wamewaomba hawa atakayefanikiwa kuingia Ikulu awaongezee Buku nyingine 14 ili wapate Buku 21 kwa sababu gharama za kuishi MUJINI zimeongezeka sana.

Mkuu naona sasa kila mtu anaweza kuwa raisi. Unaonaje tutangaze nia. Halafu hawa ccm kama miaka 50 wameshindwa kutatua hizo kero wanazozitaja ni kipi kinawasukuma kutaka uraisi?
 
Reactions: BAK
LoL! Tangaza Mkuu mie nitakuwa Mwenyekiti wa mtandao wako wa kukupigia debe la nguvu ili uingie Ikulu kwa makubaliano kwamba ukimaliza awamu zako mbili itakuwa zamu yako kuwa Mwenyekiti kwenye mtandao wa kunipigia debe kuingia Ikulu. Nchi imeoza hii Mkuu, Ikulu si mahali patakatifu tena sasa imekuwa ni nyumba ya mafisadi.

Mkuu naona sasa kila mtu anaweza kuwa raisi. Unaonaje tutangaze nia. Halafu hawa ccm kama miaka 50 wameshindwa kutatua hizo kero wanazozitaja ni kipi kinawasukuma kutaka uraisi?
 
Wasira hata bungeni hatarudi sasa izo ndoto za urais ni kujitafutia umaarufu tu wa mwisho mwisho
 
Ngoja nianze mchakato.
 
Reactions: BAK
Wasira hata bungeni hatarudi sasa izo ndoto za urais ni kujitafutia umaarufu tu wa mwisho mwisho

Wewe ni nani mpaka unawaza mtu anajitafutia umarufu? Wassira yuko serious katika jambo hili apewe nafasi atekeleze dira ya maendeleo.
 
Ana intellectual ability gani wasira ya kuongoza nchi zaidi ya ubabe na misuri? Upumbavu huo hatutaki. Ajaribu ccm wakione kinachowasubiri.
 
Tuombe Mungu kikombe hiki kituepuke. Pinda na wassira?? Bora january.
 
Si ajabu Nkamia na Lusinde nao wataombwa kugombea
 
watu makini kama sisi kina gogo la shamba tunasubiri mtu atakayekuja na maono yake kugombea urais sio anaekuja na mambo eti kasukumwa na watu,cha msingi hapa ni yeye mwenye aamue kuutaka huo urais maana atakuwa kisha jipanga
 
Ana intellectual ability gani wasira ya kuongoza nchi zaidi ya ubabe na misuri? Upumbavu huo hatutaki. Ajaribu ccm wakione kinachowasubiri.

Usiyemtaka ndie atakaye kua mkuu
 
Kwanza siamini kama maneno haya yamesemwa na Wassira. Kama ni kweli basi safari hii tutashuhudia Cabinet nzima ya kIkwete ikigombea Urais. Wassira? Msimsingizie mtu wa watu bure!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…