Wassira ndani ya DK 45 ITV

Wassira ndani ya DK 45 ITV

Huyu jamaa ana sumu mbaya sana na kama ni mtu wako wa karibu anaweza kuiteka akili yako kwa jinsi anajua kufix mambo!!!!

Anakanusha kuwa hakuzomewa, eti wale walikuwa walevi!!!

Alafu anadai wale walevi waliomzomea walinyweshwa pombe na waandishi wa habari ili kupata story ya kuandika.. sumu tupu.
 
hahahaaaaa wasira bwana, anasema kulikua na watu elfu sita au elfu saba, amehutubia kuanzia saa tisa hadi saa 12 na amejibu maswali zaidi ya 10. . . . hahahaaaa huyu bwana!
yaaani kuanzia saaa tisa hadi saaa kumi na mbili halafu maswali kumi? na yule kijana nae kamweza kweli, sasa anazungumzia uchumi wa nchi, sijui hata kausomea wapi huko
 
ITV wamekosea. Wangempambanisha na Kamanda mmoja hapo kama Mh Mdee muone kama angekaa kwenye kiti dkk tano huyo!
 
Kama alipewa maswali vile mbona anasoma majibu?amekataa hakuzomewa!
 
Semunyu si size ya Wasira anashindwa kabisa kumuuliza maswali stahili,pengine anamuogopa

Ni kweli amempa nafasi kubwa kama kaja ITV kutangaza sera badala ya kujibu maswali, naona anatoa ufafauzi ni kwa nini uchumi unakua kwa kati ya 6% - 7%, ni kama walipeana maswali atakayoulizwa.
 
Kammeza kabisa presenter. Hili li sura lake naona linamtisha presenter kiasi kwamba anakosa chakuuliza

aaaah inaelekea jamaa ana kumbukumbu nzuri, unakumbuka kile kipindi cha kwanza alimuuliza swali flani kidogo achapwe vibao, wakati anaeleza sio yeye anaeleya mvua
 
Mwenye kumbukumbu sahihi naomba anisaidie, Wassira ni msemaji wa CHADEMA maana anaongea kuhusu CHADEMA tu?

CCM hana cha kuwaambia wananchi zaidi ya 'umbeya' kuhusu CHADEMA? Wassira na wizara yake wamefanya nini? ahadi za CCM zimekelezwa kwa kiasi gani?
 
huyu mzee wangemwacha apumzike tu jamani atapata kisukari buree maana hata sielewi anaongea nini, sasa anapingana na Bosi wake aliekubaliana na Lowasa kuwa ukosefu wa ajira ni bomu litakalolipuka anytime, anatoa irrelevant examples
 
ITV wamekosea. Wangempambanisha na Kamanda mmoja hapo kama Mh Mdee muone kama angekaa kwenye kiti dkk tano huyo!

Hata Masako angemtosha huyu gamba naona leo kapeta maana hajabanwa kisawasawa.
 
wasira hana sera eti anajaribu kupondea m4c kama njia ya kutakasa ccm, ina maana yeye hajui ccm hata wakipaka mafuta ya kuku haitavutia? Mimi naona wasira anajaribu kuzoa maji yaliyomwagika kwa kupondea maji yaliyoko mtungini jambo ambalo haliwezekani. au kujaribu kumsifia marehemu kwa kumpondea anayeishi jambo ambalo haliwezekani. Kama ulishindwa kumwokoa kumtetea ndo utaweza?
 
Kumbe huyu Mzee ndio yuko hivi!!! sijawahi kumuona kwa karibu jamani
 
Ndo maana tunasoma Amelaaniwa mtu yule amtegemea mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake. Jamaa nadhani anategemea fadhila za mtu kwa hiyo anaona bora amridhishe.
The unseen is illustrated by the seen.
 
Naona ya kuzomewa imekuna sana anahitimisha kwa kukandia tena vyombo vya habari, kweli kazomewa dingi wa watu, duh I wish kungekuwa na wakati wa kupiga simu, sijui ingekuaje
 
Ni kweli amempa nafasi kubwa kama kaja ITV kutangaza sera badala ya kujibu maswali, naona anatoa ufafauzi ni kwa nini uchumi unakua kwa kati ya 6% - 7%, ni kama walipeana maswali atakayoulizwa.

Ndio Comrade kwani muda mwingi ametumia ama kueleza habari ya CDM,hapana hawakupeana maswali isipokuwa Mwandish wa habari hana maswali mapya na ya msingi thus y,ukizingatia wasira kuwepo hapo si mara ya kwanza.
 
jamaaa n i so funnnnn... yaani kweli amezeeka anakwambia kuongezeka kwa vijana kutokuwa na ajira si tatitozo (bomu), anasema wanajenga viwanda ili vijana wapate ajira,
anasema semina za ma dc si tatizo wakirudi watapiga kazi, daaah huyu jamaa kweli kachoka, anakwambia habari za kuvaa gwanda za chadema ni mbwembwe tu, daahaaaaa
 
Back
Top Bottom