Wassira: CCM Ikisimamisha Mla Rushwa Itapoteza Dola

Wassira: CCM Ikisimamisha Mla Rushwa Itapoteza Dola

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,576
Reaction score
28,497
WAZIRI wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira amesema iwapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitafanya kosa kumsimamisha mgombea mla rushwa, kitapoteza dola.

Akizungumza jana na waandishi wa habari baada ya kudhaminiwa katikaofisi za CCM Mkoa wa Dar es Salaam,Wassira alisema kamwe wana CCM hawatakubali kupoteza dola, badala yake atateuliwa mtu safi.

Mgombea huyo alisema Watanzania hawana nchi, ambayo iko sokoni na akaongeza kuwa kama Tanzania ingekuwa inauzwa, wangetangaza zabuni ya kuinunua, hivyo akawatakawagombea wenzake wanaotumia rushwa, kuacha.

Alisema yeye hatoi rushwa na anatafuta wadhamini mikoani kwa kutumia gari na sio kupanda ndege au helikopita.

Alisema hadi jana alikuwa ameshapata wadhamini kutoka mikoa 15 na akasisitiza kuwa atazunguka nchi nzima, kusaka wadhamini kwa kutumia gari lake.

Hata hivyo, Wassira aliwasihi wagombea urais wa CCM ambao wametangaza nia na wale ambao wamechukua fomu kuomba kugombea urais, wasigombane kwani kufanya hivyo kutawanufaishawapinzani.

Alisema ugomvi wa miongoni mwa wana CCM, uliwanufaisha wapinzani katika majimbo ya Kawe na Ubungo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, hali ambayo ilisababisha CCM kupoteza majimbo hayo kwa vile tu wagombea waliingia kwenye ugomvi."Mimi nagombea na sitaki kugombana na mtu na nawasihi wenzangu wengine pia tusiingie kwenye ugomvi kwani kufanya hivyo wapinzani watapita katikati yetu na kushinda uchaguzi," alisema Wassira.

Wassira alisema ana hakika atashinda na atakipokea kijiti kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete na akawataka wana CCM, waamua kwa haki na sio kwa rushwa. "Haki itapatikana katika mazingira tulivu na sio mazingira ya rushwa," alisema Wassira.

Chanzo :
Habari Leo
 
Ukiwafuatilia vizuri wagombea urais kupitia ccm, asilimia tisini (90%) ya Kauli zao zinatoa taswira ya kwamba, Edo ndiye TISHIO kuliko watangaza nia wote.

Na kila mmoja kati ya wale walio serious kuchukua dola (makongoro, membe, makamba, wasira, na Sita) wanaamini kuwa endapo Edo ataenguliwa basi yeye (kati ya hao niliotaja hapo juu) ataibuka kidedea.
 
huyu naye, afuate maelekezo, ameambiwa alitoa rushwa kwenye uchaguzi wa ubunge akashindwa kesi, nashangaa mpaka leo hajachapwa viboko 12 kama nyerere alivyosema kwa mtoa rushwa na mpokea rushwa? hukumu yake soma gazeti la jamhuri la jana.
 
mbona hata yeye nimtoa rushwa? na ushahidi wa kimahakama upo?ndani ya ccm lao ni moja. hakuna jipya. sera yao ni kulindana tu.
 
Sasa yeye wasira nani kamwambia nchi inataka watalii waje kushangaa ikulu!!!! Hahaaaa chipa
 
mtu ambaye mimi simtaki ni Lowasa wengine wanazungumzika ila Lowasa hafai kabisa.
 
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wassira amesema iwapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitafanya kosa kumsimamisha mgombea mla rushwa, kitapoteza dola.Wassira alisema kamwe wana CCM hawatakubali kupoteza dola, badala yake atateuliwa mtu safi.

Mgombea huyo alisema Watanzania hawana nchi, ambayo iko sokoni na akaongeza kuwa kama Tanzania ingekuwa inauzwa, wangetangaza zabuni ya kuinunua, hivyo akawataka wagombea wenzake wanaotumia rushwa, kuacha. Alisema yeye hatoi rushwa na anatafuta wadhamini mikoani kwa kutumia gari na sio kupanda ndege au helikopita. Alisema hadi jana alikuwa ameshapata wadhamini kutoka mikoa 15 na akasisitiza kuwa atazunguka nchi nzima, kusaka wadhamini kwa kutumia gari lake.

Hata hivyo, Wassira aliwasihi wagombea urais wa CCM ambao wametangaza nia na wale ambao wamechukua fomu kuomba kugombea urais, wasigombane kwani kufanya hivyo kutawanufaisha wapinzani.
Alisema ugomvi wa miongoni mwa wana CCM, uliwanufaisha wapinzani katika majimbo ya Kawe na Ubungo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, hali ambayo ilisababisha CCM kupoteza majimbo hayo kwa vile tu wagombea waliingia kwenye ugomvi.

“Mimi nagombea na sitaki kugombana na mtu na nawasihi wenzangu wengine pia tusiingie kwenye ugomvi kwani kufanya hivyo wapinzani watapita katikati yetu na kushinda uchaguzi,” Wassira.
Wassira alisema ana hakika atashinda na atakipokea kijiti kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete na akawataka wana CCM, waamua kwa haki na sio kwa rushwa. “Haki itapatikana katika mazingira tulivu na sio mazingira ya rushwa,” alisema Wassira.

chanzo habari leo
 
Ukiwafuatilia vizuri wagombea urais kupitia ccm, asilimia tisini (90%) ya Kauli zao zinatoa taswira ya kwamba, Edo ndiye TISHIO kuliko watangaza nia wote.

Na kila mmoja kati ya wale walio serious kuchukua dola (makongoro, membe, makamba, wasira, na Sita) wanaamini kuwa endapo Edo ataenguliwa basi yeye (kati ya hao niliotaja hapo juu) ataibuka kidedea.

Uko sahihi
 
Dah majanga kweli Sokwe mtu huyu. asa kama ivyo ndivyo mbona yeye aliyethibitika kutumia rushwa akahukumiwa na mahakama kwa kosa hilo anataka kugombea?Mleta mada hebu nisaidie kumuuliza.
 
Dah majanga kweli Sokwe mtu huyu. asa kama ivyo ndivyo mbona yeye aliyethibitika kutumia rushwa akahukumiwa na mahakama kwa kosa hilo anataka kugombea?Mleta mada hebu nisaidie kumuuliza.


Hahahaha, mkuu Mount Kibo mbona tutashuhudia vimbwanga vingi mwaka huu..
 
Last edited by a moderator:
mtu ambaye mimi simtaki ni Lowasa wengine wanazungumzika ila Lowasa hafai kabisa.

Ni nani aliye msafi ndani ya CCM hadi mlaruane katika kipindi hiki mbona hayo mambo hamkuyazungumza kipindi cha nyuma?
 
Back
Top Bottom